Mie nilianzia Msange JKT na kumalizia hapo - OPERATION program ya chama. Tulikuwa na Afande Mohamed, Mrope, Odo, Mandevu, Matron Gwimo, Magege, na wengine kibao ila majina yashaanza kunitoka. Hii ilikuwa mwaka 1989/90.
Leo ntaweka kituko kimoja tu kutoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa akienda kwa jina la Ukunu au Pepo. Huyu Matron Gwimo alikuwa na tabia ya kuja na kuingia bweni la wavulana na kuamsha bila ya kutoa warning. Hiki kitendo kilituudhi sana na siku ya mkutano watu wakapania kumsemea. Wengi wakawa wanalalamika ila wanaogopa kumtaja Matron huyo ni yupi. Ukunu alisimama na kusema Matron huyo ni Gwimo. Hapo niliona sura za Ma-afande zikianza kuwa nyekundu kwa hasira na nikajua kuwa wakitoka hapo watauwa mtu. Jamaa akaendelea ".. huyu afande alishasababisha mgomo kumbaini B watu wakakataa kula. Huyu alifanya ..... na afande unajua kuwa sisi wanaume tukilala, asubuhi tunapoamka huwa tunakuwa na MIGOGORO........" Lohhh, watu walicheka hadi wakalala na mkutano ukawa umefia hapohapo maana hata afande mwenyewe machozi yalikuwa yakitoka kwa kucheka. Mkutano ulifungwa na Sajenti Manyilizu na luteni Mohamed alijikaza kwa shida kupigiwa saluti. Alipovua tu kofia akaangua tena kicheko.
Ikawa kila siku wasichana wakimuona asubuhi wanamuuliza ".. kaka Manara, vipi leo mgogoro ulikuwaje?". Ila maajabu yalikuwa kuona wanawake na wanaume wakioga UCHI katika umbali wa mita kama 5 hivi. Na unapatwa na mshangao unapochota maji, vilikuwepo vi-plastic sijui vilikuwa vya nini, basi watu wakawa wanatekea maji kisimani. Sasa anakuja dada na kusema "..... na mimi naomba hicho kikondom cha tembo nichotee maji......" Kweli wanawake wakimaliza JKT huwaambii kitu. Tofauti yao na wanaume tuseme ukweli haipo.