Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Matangazo yalitolewa kama ORDER
Siku ya kwanza kuripoti, tukakuta skendo ya mauaji ! Kuna Sajenti taji, anakula wake za wenziwe kwa kitisho cha uchawi ! Mpaka C O anamuogopa ! Siku moja kaingia kwa jamaa ambae alikua lindo, jamaa alipopata taarifa akamzukia. Basi aligonga mlango afunguliwe, wakati wanajishauri jamaa akakimbilia dirishani, akiwa anamuona vizuri kutokea dirishani.......,..,...akampa 7 ! Kiuno kikajigawa
 
Mama jeni! Mama jeni, we mama jeni.
Nyimbo zenu hizo na ile ya
Iddi Amin akifa, mie siwezi kulia, nitamtupa kageqa, awe chakula cha mamba!
Lol. Hapo wote weusi kudadadeki dume ,jike hajulikani.




Zaina zaina......Zaina, mtoto wa Mafinga....Zaina, mbona sikuoni...Zaina lete raha Zaina. Hizo zilikuwa ndo zetu Mafinga. Ukibadilisha kidogo unapiga -Siku zinapanda milima siku zinateremka mabonde mama..
 
Huyu jamaa mimi nilikaa naye sero kwa zaidi ya wiki moja. Siku ya tukio tulijulishwa kwamba kuna afande amekula kichwa cha afande mwenzio na kulala msituni na SMJ na magazine yenye zaidi ya risasi kumi. Tukaambiwa baadae tutaenda mistuni kumsaka. Wakati matumbo yanatuuma itakuwaje, mara jamaa likajitokeza na silaha yake juu huku lina kitambaa chekundu na baadae wakamsweka ndani tukaishi wote na hatimaye kumuacha mahabusu. Inasemekana baadae alipelekwa mahakama za kawaida akahukumiwa kwa mauwaji ya bila kukusudia.
 
Nakumbuka mashamba ya Idetelo, detach ya mifugo,kina afande Kingu, john's corner, c ya matron, smart area...
Mi nilikuwa intake ya miaka 20 ya azimio la Arusha.
Tukipewa hotuba siku ya kugawiwa combania,
Nikiwa A-coy.
Hapa tutakufundisha kula mboga ya aina moja kwa mwaka; kushindia kikombe kimoja cha chai.
Nakumbuka tukiwa kitengo cha kupasua kuni jinsi tulivyoweza kuchoma bisi bila moshi kuonekana, na kila mmoja alikuwa na uwezo wa kula mahindi manane ya bisi kwa siku.
Nilimalizia Mlalakua makao makuu ya JKT, enzi za marehemu colonel Msonge aliyekuwa CPNS.


Huyu Rwekaza Lyakutununta si alikuwa mkuu wa Danger Coy katika operation ya vyama vingi? Alikuwa ni mbaya kwa watoto sana!
 
Ila pamoja na mikwala yote hiyo ya JKT nilistahimili kwani nilikuwa nimetoka Chuo Cha maafisa wa jeshi nimeiva yaani NYAKATO SEC. Bukoba hii nayo ilikuwa zaidi ya Jeshi, Koma ya msosi, Karakana kila siku usiku, kujificha Nyamushongoma, Mchakamchaka hadi Nyanga we acha tu. Waliosoma nyakato enzi hizo wanalijua hilo na wengi walioingia jeshi walikuwa maafisa ndio maana naiita Nyakato chuo cha maafisa.

nyakato-Bukoba ni kiboko yao,ile ni jeshi mkuu
 
Kwa wale waliokuwa RUVU JKT OPERATION OLJORO mwaka 1994 naomba tukumbukane.Mimi binafsi nilikuwa FCOY.Kilichonifurahisha nikiwa RUVU JKT.
.DISCO-mtu unaimba wimbo wowote hata kwa lugha ya kwenu.
.Kwa babu
.Kusimamisha minazi.
 
Asante sana kwa kumbukumbu yako nzuri iliyosheheni vituko zaidi kuliko mazuri uliyojifunza ikiwemo kilimo cha zabibu kwa wale waliokuwa Makutupora, ufugaji wa kuku wa mayai Ruvu, kilimo cha mahindi kule Mlale, mafinga, na kwingineko, bila kusahau matofari ya mawe Oljoro na kilimo cha maharage Makuyuni. Binafsi nakumbuka mraba wa zabibu Makutupora ambapo bila kufika mwisho hujakutana na uji+ugali. Nikuunge mkono kwa kalinyekalinye za maafande ambao wengi shule yao ilikuwa ni 10-3 =? anasema "usilete mambo ya kulosi polinesheni hapa bwana". Nimkumbuke Sir major Singira amabaye tulipambana sana katika kombania 'A' kiasi cha kunihamishia kila kitengo akidhani nitasalenda. Rafiki zangu akina Ivodius Chilipweli, Makarius Nkya, Mkumbo Mitura, Jackson Mwandiki aka nywele na wengineo mpo?.
 
Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.

Acha uongo huo mwaka uliotaja sio op vyama vingi ilikuwa ni op miaka thelathini ya uhuru acha kudandia.
 
Kwa wale waliokuwa RUVU JKT OPERATION OLJORO mwaka 1994 naomba tukumbukane.Mimi binafsi nilikuwa FCOY.Kilichonifurahisha nikiwa RUVU JKT.
.DISCO-mtu unaimba wimbo wowote hata kwa lugha ya kwenu.
.Kwa babu
.Kusimamisha minazi.
Sir Major wenu alikuwa nani? Mwaka 1990/91 alikua afande Sanga. Jamaa alikua poa sana.
 
Wengi mmeandika.............mengi tumekumbuka................kumbukumbu ni nyingi,...............................vituko ni vingi kwa kila kombania na kambi pia,............................. asanteni sana..........................ila kuna hawa kuruta waliopitia oljoro JKT..........kuna siku waliamua na kukutana,........................walifanya bonge la party.......ilikuwa maeneo ya mikocheni,......................hakika niliwaone wivu walivyokuwa wanajikumbsha mambo waliokuwa wakifanya wakati huo...............................hakika ni kitu kizuri sana.....................................hongereni kuruta wa OLJORO
 
Sanctus,

Mimi niliamua kukwepa kwenda Tabora na kuamua kwenda Oljoro kwasababu nilikuwa na kakangu mjini Arusha. Nikajua nikitoroka nitakuwa na sehemu kwa kubugia ugali.

Basi kufika Oljoro, tukamkuta afande Dauda, (sijui kama linaandikwa hivyo) alikuwa ndio mkuu wa mafunzo. Akasema mwaka jana alitoa kibali cha kuua kruta watano, akasema aligundua haikutosha, anawaamrisha maafande mwaka huu kuua kruta mpaka 15.

Kesho yake watu kibao wakatoroka na kwenda ku report kambi zingine. Isingelikuwa kuwa na brother hapo mjini na mimi ningelirudi kule Tabora usiku huo. Baada ya muda tukaja gundua kumbe Dauda ndiye alikuwa afande poa kuliko wengine wote.

Tulikuwa na afande mmoja Mhehe alikuwa anaitwa Mduda. Alikuwa anajifanya anajua jeshi kweli kweli. Akaopoa mtoto wa maana sana. Siku moja tumemaliza jeshi tuko mlimani, akaingia mlimani hall D na magwanda, kaja kufuata mtoto wake. Maskini yule msichana alikuwa terrified, akajificha. Jamaa akasubiri pale wee, mpaka akaamua kujikata. Alifikiri yale ya jeshini yanaendelea uraiani. Tulimsanifu kweli siku hiyo.

Looh! ni miaka karibu 20 toka wengine tuondoke JKT lakini naona michapo yake inakuja tu. Waswahili tungelikuwa tunaandika vitabu, tuna mengi ya kusimulia.

Umenikumbusha mbali sanaaaa.wale wa Operation Okoa Oljoro JKT kombania A kwa afande Dauda, John Matondo,Msambaa mmoja jina simkumbuki na afande mmoja mtu wa kusini alkuwa anapenda sana kuimba disko wa kombania C,kuokota kuni shimo la mungu majitambo ya maafande kuwa kuruta 10 wa jeshi kazi yao ni sawa na trekta moja la valmet na tela lake,kwata ya nguvu drill,mchakamchaka kula kwa foleni kimbembe ni pale unapozira chakula cha jeshi au mboga ni sangara au nyama kwata inakuwa kali kuliko0,wengine walipigwa bogi kwenda mgambo tanga waliotoroka na kurudi wanasimulia unyama wa afande Mtono,service wengine tulikatwa bogi kenda Itende nakumbuka ile siku tulipoimba disko kusherehekea kifo cha mtoto wa Meja ...... baada ya kughadhabishwa na matendo yake ya kutufanya wote pamoja na maafande kama kuruta,mtoto mwenyewe alishika waya wa umeme wakati wa greda likifanya cut&fill karibu na nyumba ya afande Rest House,kutulazimisha kuchimba mabwawa ya samaki katika makaburi ya wazungu walikuwa wamezikwa pale, kwa ujumla mwaka mmoja nilijifunza mambo mengi na nashukuru sana kuwa yananisaidia hadi leo hasa MM na ukakamavu.
 
Mie nilianzia Msange JKT na kumalizia hapo - OPERATION program ya chama. Tulikuwa na Afande Mohamed, Mrope, Odo, Mandevu, Matron Gwimo, Magege, na wengine kibao ila majina yashaanza kunitoka. Hii ilikuwa mwaka 1989/90.
Leo ntaweka kituko kimoja tu kutoka kwa jamaa mmoja aliyekuwa akienda kwa jina la Ukunu au Pepo. Huyu Matron Gwimo alikuwa na tabia ya kuja na kuingia bweni la wavulana na kuamsha bila ya kutoa warning. Hiki kitendo kilituudhi sana na siku ya mkutano watu wakapania kumsemea. Wengi wakawa wanalalamika ila wanaogopa kumtaja Matron huyo ni yupi. Ukunu alisimama na kusema Matron huyo ni Gwimo. Hapo niliona sura za Ma-afande zikianza kuwa nyekundu kwa hasira na nikajua kuwa wakitoka hapo watauwa mtu. Jamaa akaendelea ".. huyu afande alishasababisha mgomo kumbaini B watu wakakataa kula. Huyu alifanya ..... na afande unajua kuwa sisi wanaume tukilala, asubuhi tunapoamka huwa tunakuwa na MIGOGORO........" Lohhh, watu walicheka hadi wakalala na mkutano ukawa umefia hapohapo maana hata afande mwenyewe machozi yalikuwa yakitoka kwa kucheka. Mkutano ulifungwa na Sajenti Manyilizu na luteni Mohamed alijikaza kwa shida kupigiwa saluti. Alipovua tu kofia akaangua tena kicheko.
Ikawa kila siku wasichana wakimuona asubuhi wanamuuliza ".. kaka Manara, vipi leo mgogoro ulikuwaje?". Ila maajabu yalikuwa kuona wanawake na wanaume wakioga UCHI katika umbali wa mita kama 5 hivi. Na unapatwa na mshangao unapochota maji, vilikuwepo vi-plastic sijui vilikuwa vya nini, basi watu wakawa wanatekea maji kisimani. Sasa anakuja dada na kusema "..... na mimi naomba hicho kikondom cha tembo nichotee maji......" Kweli wanawake wakimaliza JKT huwaambii kitu. Tofauti yao na wanaume tuseme ukweli haipo.
Mkuu unakumbuka embakasi...Namkumbuka afande sijali??afande masabila,Kuna afande kafupi kalikuwa sijui kanaitwa nani kalikuwa kajamaa ka Dom kabila linaloongea kwa kusonya!! Sikonge..It was so fun guys!!
247893_10150197159372013_2417811_n.jpg
 
Sijali namkumbuka kwa mbaali sasa. Huyu jamaa alikuwa B au D-Coy kama sikosei.

Mie nilikuwa A-Coy na Afende Moddy na Boss wake Mwiru. Enzi hizo kulikuwa na Odo, na MKurya mmoja mwenye Korokoro Mkononi. Daah, majina wengi nimeanza kuwasahau.

Huyu afande wa Dodoma, simkumbuki. Ila enzi zetu wasumbufu walikuwa Afande Wera? (sijui nimepatia, Muha wa Kigoma), Afande Magwega (sijui jina lake lilikuwa nani?), alikuwepo mtu anaitwa NGOMA, alikuwa akitesa sana watu.

Enzi hizo kweli UBONGO ulisimama kufanya kazi.
Mkuu unakumbuka embakasi...Namkumbuka afande sijali??afande masabila,Kuna afande kafupi kalikuwa sijui kanaitwa nani kalikuwa kajamaa ka Dom kabila linaloongea kwa kusonya!! Sikonge..It was so fun guys!!
247893_10150197159372013_2417811_n.jpg
 
Sijali namkumbuka kwa mbaali sasa. Huyu jamaa alikuwa B au D-Coy kama sikosei.

Mie nilikuwa A-Coy na Afende Moddy na Boss wake Mwiru. Enzi hizo kulikuwa na Odo, na MKurya mmoja mwenye Korokoro Mkononi. Daah, majina wengi nimeanza kuwasahau.

Huyu afande wa Dodoma, simkumbuki. Ila enzi zetu wasumbufu walikuwa Afande Wera? (sijui nimepatia, Muha wa Kigoma), Afande Magwega (sijui jina lake lilikuwa nani?), alikuwepo mtu anaitwa NGOMA, alikuwa akitesa sana watu.

Enzi hizo kweli UBONGO ulisimama kufanya kazi.
Kajamaa kalikuwa kashortii hivi sijui alikuwa anaitwa nani???hivi nitamkumbuka...Afande wera..dah!!!Niliamka usiku kwenda kufagia msituni shida aina adabu..leo hii hawa mabishoo wanaosoma hizi shule za fm academia wataweza???Kubeba mtulinga wa maji kutoka shamba la mdarasi hadi jikoni???Dah..nimekumbuka nilikuwa nikijipendekeza officers mess kula ubwabwa!!nilikiwa na kishtobe wangu kule basi mimi nagongelea misosi ya officers mess!!!
 
Kajamaa kalikuwa kashortii hivi sijui alikuwa anaitwa nani???hivi nitamkumbuka...Afande wera..dah!!!Niliamka usiku kwenda kufagia msituni shida aina adabu..leo hii hawa mabishoo wanaosoma hizi shule za fm academia wataweza???Kubeba mtulinga wa maji kutoka shamba la mdarasi hadi jikoni???Dah..nimekumbuka nilikuwa nikijipendekeza officers mess kula ubwabwa!!nilikiwa na kishtobe wangu kule basi mimi nagongelea misosi ya officers mess!!!

KK hiyo enzi imepita,hata wakirudisha JKT itakua siyo ya enzi zetu. Enzi zile hata ukiwaangalia askari unaona ni mtu anayependa kazi yake. Siku hizi wengi wanajiunga na jeshi kutafuta ajira!
 
Kazi kweli kweli hususan unapotaja RUVU JKT.

Nilipita hapo enzi CO akiwa Col Meena, Na Nilikuwa Kombania A iliyokuwa inaongozwa na Afande Capt Othman. na Sirmega Stuke, nawakumbuka pale akina Cpl Nyundo,Sahani, Mwambigu, Chenga, Sgt Mazani (mzee wa totoz), Urassa , Sgt Kitomali (ambaye wiki mbili nilipokuwa Dar nilikutana nae siku hizi ni kiongozi wa Mgambo wa jiji la Dar)na maafande wangu akina Lt Nyoni, Sylas na wengine.

Nimestuka sana mtoa mada alipokumbusha kwa BABU na vibwende. Bila kusahau mayai ya phase A na mashamba kule Phase B.

Kweli JKT tumejifunza mengi na tumetoka mbali

 
Back
Top Bottom