Ilikuwa operation vyama vingi,tulikuwa pamoja mkuu,huyo Sgt mlimbila alikuwa akiwaingilia makuruta na wake Wa mastaff kimiujiza,Bubu Msema Hovyo, kisa chako ni kizito na kimenigusa sana . . .
I am starting to think sijui tuandike kitabu cha "VISA VYA JKT" . . . very interesting
nimepita hapo OP MUUNGANO hatari sanaaaaWale wa 823kj msange tabora mpo? Siku hizi ni kuangushia tu hamnaga hata mkesha. Dah maisha yanaenda kasi sana nikipakumbuka hapa hakukuwa na amani hata kidogo na ukiwasimulia vijana wanaona unatania au unawatisha
Duh sina mbavu!Mkuu sijakupata, unatunyima raha, kama ni blue print fafanua kwa lugha ya uungwana tuelewe.
Umenikumbusha mambo ya kuoga na Mestin pale maji yanapokosekana na bado unatakiwa utakate. Ni kweli watu hawakuwa na aibu ya utupu.
Siku moja kamanda moja mwenye nyota mbili sikumbuki jina, alikuwa na binocular wakati tunakata kuni. Akaniambia " Kijana tunajua mambo mengi sana mnayo fanya ila tunamezea wakati mwingine" nilipomwuliza kwa nini akanipa binocular na kulielekeza wapi niangalie, huwezi amini, kulikuwa na askari kuruta wa jeshi wa kike na kiume wakifanya kamchezo kabaya . . . baada ya kukata kuni. Du, nilibaki hoi sana
umenikumbusha mbali nkya na alloys ni noma hasa kipindi cha pori mlima nguruwe na kuzima moto msitu sao hillDah nakumbuka 841kj pale mafinga .... Jkt ya zaman ilikuwa na mafunzo mazur sana... Sitawasahau makamanda hawa. Lt nkya, Lt liundi, Lt alloys, na wiliam Sagala... Mpaka leo nina alama mgongon na mkono wa kushoto... Nilichimba handak kwa sahan na panga
Dah poleni sana mkuu,lile eneo la E coy na F coy nalikumbuka sana lilivyokuwa lipo hovyo mno.Mimi nilikuwa B coy ila wale wa E na F coy tulikuwa tunawaonea sana huruma.Mimi nilipita juzi juzi tu sio miaka mingiMim sitasahau jkt .nakumbuka nilijiunga jkt nikapangwa jkt mgambo kabuku 835kj ilikuwa noma sana sitaweza kumsajau capt laiza alikuwa akionekana kombania watu wanalia hata bado mazoez hajatoa.nakumbuka siku moja kulikuwa na mvua sana usiku wakat wa mkesha makamanda wa E coy na F coy waliungana wakatufanyia kitu ambacho hadi leo ninapokumbuka nakuwa mpole sana walikuwa na upupu wakaumwaka lile eneo tunalofanya mazoez wakawa wa wanatuambia tulale chin na stik nyingi tu roll zile tope zilikuwa zinawasha sana tulijikuna sana hadi asubuhi ule usiku ulikuwa wa mateso coz uwasho na stick za kutosha.sitaweza kusahau jkt(mwana ukome)
Kaka usipasahau na muyobozi au ilagala gerezaniDah! umenikumbusha mbali sana mkuu..1991/92 op. vyama vingi..Makutupora A-coy tulipangwa kumwagilia bustan.. Lakini baadae tukahamishiwa Bulombora, D-coy. Namkumbuka afande Mnzena, Mtekere, afande Sezero, coplo Ngoma, afande Mbewa na afande machachali mikwara mingii Stanslaus Makoba ''kadebra'' baiskeli yake iliandikwa ''sereuka mwana wa ndege..mnafiki hakosi sababu'' Kombania hii kulikuwa na vijana akina Robert Nyamhanga, Prudence Timanywa, Mongu Manumbu, Mpemba Francis, Safari Lucian, Redemtus Shoto, Privatus,Anterius Sostenes, Joe Kihampa (TBC1) na wengine. Akina dada kulikuwa na Kore Ally Sadick, Rose Manyama, Judith Schirima, na wengine wengi. Nakumbuka umoja, ushirikiano wa kusaidiana kuepuka visanga baina ya makuruta nk. Siku tukipokea ''kichele'' tulikuwa tunakwenda kijiji cha Kaseke kutumia. -J4 wa D-coy
Tupo Mlale Tupo. Afande Nguvu ya Nyani, Rweikiza. Sabuni, Mande, Chuma, Matron Grace na MWajuma Magagula na Lusonga sitaenda tena. Maafande wa Mlale watanisurubu! Dah Shamba la Embakasi. Ukarimu wa Wangoni watani zangu! Jamani ni kumbukumbu nzuri. Wimbo wangu daima ulikuwa ' Nimeuona mpilipili na maua yake nselema......' Ile nyumba ya mbao iliyokuwa ikihamishwa na Kuruta Dah!Naona Mlale tupo wachache sana huku ww utakua mtoto wa Mpuku.hahahaa
Nguvu ya Nyani ( mwaliko) anapanda juu ya Mti asome namba ya kiatu wakati wa kwata......Msambaa yule.....Matron Grace alikuwa Mzuri kweli....... 1989/90 Program ya ChamaTupo Mlale Tupo. Afande Nguvu ya Nyani, Rweikiza. Sabuni, Mande, Chuma, Matron Grace na MWajuma Magagula na Lusonga sitaenda tena. Maafande wa Mlale watanisurubu! Dah Shamba la Embakasi. Ukarimu wa Wangoni watani zangu! Jamani ni kumbukumbu nzuri. Wimbo wangu daima ulikuwa ' Nimeuona mpilipili na maua yake nselema......' Ile nyumba ya mbao iliyokuwa ikihamishwa na Kuruta Dah!
Umemsahau afande Matiku.. MamaeeeMlaleee Songea kwa afande kitomary na Mahmoud ni shida.
Wow Sawa kabisa sawa kabisa! Yaani I wish kama tungekutana woooote tuliopitia Mlale na Maafande wetu. Dah Nguvu ya Nyani atakuwa Mtu mzima sana sasa na Grace naam She was Beautiful and Humble!Nguvu ya Nyani ( mwaliko) anapanda juu ya Mti asome namba ya kiatu wakati wa kwata......Msambaa yule.....Matron Grace alikuwa Mzuri kweli....... 1989/90 Program ya Chama
Kwa kweli nimesisimka sana kwa yote; kwani limepelekwa mbali sana na kila mchangiaji.
Mimi nilianzia mgombo-kabuku tanga na kumalizia maramba; 1989\90.lamsingi kwa wadau wote ili historia isipotee; ni vyema ifanyike documentation na hatimaye itayarishwe video series\film.
Hapo tutakuwa tumejitendea haki wadau wote na jkt kwa ujumla.
Napendekeza iundwe team ya kukusanya matukio na habari zote zilizotokea; ili iandikwe healthy script itakayotoa best and exciting picture of what really happened in those camps.