Dah! umenikumbusha mbali sana mkuu..1991/92 op. vyama vingi..Makutupora A-coy tulipangwa kumwagilia bustan.. Lakini baadae tukahamishiwa Bulombora, D-coy. Namkumbuka afande Mnzena, Mtekere, afande Sezero, coplo Ngoma, afande Mbewa na afande machachali mikwara mingii Stanslaus Makoba ''kadebra'' baiskeli yake iliandikwa ''sereuka mwana wa ndege..mnafiki hakosi sababu'' Kombania hii kulikuwa na vijana akina Robert Nyamhanga, Prudence Timanywa, Mongu Manumbu, Mpemba Francis, Safari Lucian, Redemtus Shoto, Privatus,Anterius Sostenes, Joe Kihampa (TBC1) na wengine. Akina dada kulikuwa na Kore Ally Sadick, Rose Manyama, Judith Schirima, na wengine wengi. Nakumbuka umoja, ushirikiano wa kusaidiana kuepuka visanga baina ya makuruta nk. Siku tukipokea ''kichele'' tulikuwa tunakwenda kijiji cha Kaseke kutumia. -J4 wa D-coy