Tutafutanewa oljoro jkt operation okoa tujuane
Wewe Ruvu ulikuwa transit tu. Ulipelekwa ChitaWale wa 832 KJ ~ RUVU JKT wapo? Operation miaka 30 ya uhuru?
Hapo ni ngumu kutofautisha kuruta wa kike au kiume.Uchaka.........that was the real part of JKT man.....sio siku hizi kuuza matrekta
Ulikuwa Operesheni ipi?Dogo huku-miss kitu:
I hate that d@mn thing JKT. Dakika za mwisho nilikuwa Ruvu JKT. Unavaa nguo zinazofanana na mtoto wa waziri au Brigedia wa jeshi na wewe unaisi mko kwenye ligi moja. Lakini ngoja Jeshi limalizike uone wenzako wako wapi na wewe huko wapi?
Tarama yupo wapi siku hizi? jirani yangu kule Suca kwenye bomoa bomoaHapo nitapenda kuwakumbusha wale tuliokuwa wote pale Mafinga JKT Kombania F chini ya OC Rweikaza na yule afande invisible aliye julikana kwa jina la Master Follow-up. Tutamkumbuka afande kijana aliyeitwa Mwakyosi. Nakumbuka siku moja tuliamshwa saa kumi alfajiri kama ilivyokuwa kawaida kukata mifagio wakati tukielekea huko porini kukata mifagio kwa mchaka mchaka tuliambiwa twende tukiimba, nikaanzisha wimbo "...Siasa yetu hapana mbaya. Isipokuwa maafande ndiyo wabaya..." Jamaa kusikia mistari ile akaamuru wote kuchuchumaa chini na kuruka kichura chura.
Upande wa Afande Master Follow-up au Afande Mlimbila ambaye sasa ni marehemu, nakumbuka siku moja alimuuliza kuruta mmoja kwamba alipataje kovu lililo katika paja karibu na nyonga. Tamko lile lilizua kilio kwa binti yule na binti alikwenda moja kwa moja kwa CO T N Mlay kutoa taarifa kuhusu mauza uza aliyoyaona usiku ambapo alisema alikuwa akiota kuna mtu amevinjari naye usiku kucha na iweje afande atamke kuhusu kovu wakati ni kweli analo na alijuaje wakati hajawahi kuwa naye kwa makubaliano.
Kifo cha Master Follow-up: Siku hiyo kulikuwa na mkutano mkuu wa wakuu wa vikosi Ma-CO nchini wakati huo Mlimbila alipangiwa kulinda kituo kidogo cha JKT kilichoitwa Sao Hill ambako kulikuwa na mradi wa kuchoma mkaa. Jamaa akakaimu kazi hii kwa mtu mwingine yeye akabaki kikosini. Pale kikosini kulikuwa na afande mmoja Mngoni aliyekuwa na mkewe dogo dogo aliyeishi karibu kabisa na apartment au hanga la Mlimbila. Na afande huyu Mngoni alipangiwa kulinda geti dogo karibu kabisa na nyumbani kwake na inaelekea alishapata fununu za mtoto (Mkewe) kuvinjari na Mlimbila. Muda wa saa mbili usiku bwaloni kukiwa na dance la kumalizika kwa mkutano afande Mngoni akaaga kwenda nyumani kwake "kukagu". Inasemekana alifika akagonga mlangoni bila kufunguliwa, kisha akaenda kuchungulia dirishani na kumuona Mlimbila akiwa ameketi kitandani akiwa mtupu na mke wake afande Mngoni. Alilenga SMG kupitia upenyo wa dirisha na kumkuta Mlimbila katikati ya paji la uso kuona vile binti alikimblia sebuleni na kufungua mlango na kukimbia. Mngoni aliingia na kuuchakaza mwili kila sehemu kwa risasi. Alibakiwa na risasi kama tisa tu. Mwili wake ulipelekwa Mafinga Hospital kujazwa pamba ili angalau uso wake uweze kutambulika. Haya ndiyo nayakumbuka sana ninawakumbuka kuruta wenzangu akina Tarama Mamkwe, Ndubula Msaki, Rachel Mapande, na wengineo.
haahaa jmn mmenikumbusha mbali wale wa mgambo jkt Tanga waliokuwa B.coy afanfe Magela alitutesa sana duuuTarama yupo wapi siku hizi? jirani yangu kule Suca kwenye bomoa bomoa
Ndoa ya Urio na Makame ilikaa miaka kadhaa nafikiri. Nilikuwa Ruvu Operesheni Miaka 30 na Urio alikuwa CO, nikahamia Mlalakua baada yakuwa Serviceman na Makame ndio alikuwa Mkuu wa JKT.Maarifa,
Umenikumbusha mbali aisee. Nilikaa Mlandizi kama mwaka mmoja niki-pump maji kwenda Dar (Siku hizo NUWA). Nilipofika hapo siku moja boss wetu Mhandisi Kasiga, alikuja akatuambia tuvalie vizuri na twende kwenye sherehe ya WAFANYAKAZI wasomi kwenda kumuaga URIO. Basi sherehe ilifanyika Ruvu Secondary kwa mwalimu mkuu. Ndiyo siku nilikuja kumuona Urio. Jamaa likuwa charming wala huwezi amini kuwa ndiyo huyu mtu huwa nasikia kuwa mkorofi. Nasikia walikuwa hawapikiki na Makame. Wakati Makame anahamishiwa Mbeya na kumuacha Urio Ruvu, akasema mbele yake "... sintafuata chochote alichokuwa akifanya huyu Raia mla panya - Makonde...". Baada ya miaka kadhaa, Makame akaitwa Dar. Wakati akienda, akaamua kwenda Ruvu kuomba mayai. Urio kuona gari zuri akauliza nani huyo, wakamwambia Makame. Akaagiza MP waende wamtimue Raia aliyevamia Kambi ya Jeshi. Kumbe kufika Dar ndiyo anapewa cheo cha Mkuu wa JKT Tanzania. Nasikia cha kwanza kufanya ni kumpigia Urio simu kuwa "nakuhamishia hapa makao makuu..." Urio nasikia akacombine haraka sana na akarudi TPDF.
Unamkumbuka yule afande (Mtu wa Mbeya) aliyekuwa akishughulikia fedha pale Ruvu? Nasikia alikuwa akizika sana makuruta fedha. Watu wakizamia pale, anawapa form wajaze kuomba fedha za nauli. Mkikatwa bogi basi fedha anatia ndani. Ukimaliza JKT na kwenda kudai fedha, anakuitia MP wakutimue kwani wee ni raia. Huyu jamaa alikuwa TAJIRI baadaye na nasikia alikuja pata ajali na kufa kama sikosei Visiga? kama waenda Dar, akiwa ndani ya Pajero. Alikuwa akitamba kuwa kazika hadi fedha za marehemu waliokufa vitani Uganda, itakuwa nyie makuruta?
Mwamasangula aliletwa C Coy... F mlikuwa na warembo wengi...nakumbuka...Hebrew,
ha! ha! ha! ulikuwa RUVU combania F, kombania ya Mahepe, kombania ya Wajanja!! basi F kulikuwa na OC Luteni Mwakatumbula, Sir Major Babwetega "Mwiba", Staff Surgent Kinyaruhama "Kibuyu", Surgent Salamba, Volunteer Koplo Mwamasangula "Kamanda Mizinga", Afande Monica. pia alikuwepo Surgent mmoja Mhaya nimemsahau jina. Surgent Mwambingu pia alikuwa anakuja kubangaiza. F COY ilikuwa na watukutu wote na wasichana wote wazuri. Maafande waliamua kukomoa makuruta wa F COY lakini badala yake makuruta wakawa wagumu. lilikuwa linapigwa kwata la mfano na kufa mtu. Maafande walikuwa wanatoka maofisini kuja kuangalia kwata. Baadaye F COY ilihamishiwa Mgulani kupiga gwaride la miaka 30 ya uhuru. Afande Kitomari RSM wa Mgulani alitukoma makuruta toka Ruvu kwasababu ya utoro.
CO alikuwa Luteni Kanali Kanaeli Urio, 2IC Major Chotta, CI Major Nakuchema, Adjutant Captain Balala, RSM Warrant Officer II Situke.
JESHI LILIKUWA NI KUPOTEZA MUDA TU. SIKUONA FAIDA YAKE.
Hivi F ndio walikuwa wanakaa kule jirani na kiwanda cha nguo au wale walikuwa Special Coy? Nyundo alikuwa kwenu au B? OCwenu alikuwa poa sana...C tulikuwa na Mama Moshi lakini mambo yote yalikuwa nawarrant officer Sanga.. Mnamkumbuka afande Filipo alikuwa anacheza handball? Merdad alikuwa C Coy. na yule korokoro mwingine MmasaiKijana Kombania yenu ilikuwa ya wanyonge wa Vibwende. Mambo yote yalikuwa Alfa.
Ha ha haa...na kuoa je?Bila cheti cha JKT Hakuna ajira
Section ya mananga wa demo[emoji23] [emoji23]Du zamani sana!, Enzi hizo Baba wa taifa JKN ndio POURT, waziri mkuu ni Edward Moringe Sokoine,Gen Musuguri ndio Kinara pale juu majeshini. Kambi yangu ya ni uzalishaji mahindi JKT Mlale,Operation 'kujihami kiuchumi baada ya vita', Mkuu wa kambi ni Luteni kanali Kajembe, Meja Mandwa mkuu wa operation zote kambini, B-Coy ndio ilikuwa kombania yangu, platoon ya kwanza section ya demo ya kina Nkayamba Abeid,Nko,Solomon,Mwasha mim na kina Nyihirani, Makamanda akina Bahati, Sondora mutini kalikaka, na afande Before!, chini ya Sir major Ndaga na Lt Ndangura. Kama niliowataja wamo humu tujikumbushe jinsi tulivyohenya wakati huo. Najivunia sana kuwa katika jeshi la akiba hadi leo.
Kumbe wazee wengi humu JF!Mwanzo wa kwenda JKT:
Ni mwaka wa 1975, Jumapili. Naamka nikiwa na hangover kali baada ya kukesha Disco la Sansui pale Sea View Hotel. Nakumbuka kuwa leo ni siku ya kwenda jeshini baada ya kumaliza Mkwawa, kidato cha sita. Nachukua mfuko wangu, na kwenda Makao Makuu ya JKT, Upanga. Hapo tunapakizwa kwenye malori na kupelekwa Mgulani. Kufika tu Mgulani, foleni. Naulizwa,'Askari, kwa nini hujanyoa nywele?' Nashangaa kwa vile mimi sio askari na sijapata muda wa kunyoa Afro langu. Tunapelekwa mess, chakula ni mkate na maharage. Najaribu kula, nashindwa. Tunapakizwa kwenye malori tena, usawa wa Ruvu. Kabla ya kuingia kambini, kuna kilima, tunashushiwa hapo. Foleni. Tunaambiwatuimbe wimbo, mchakamchaka. Mie ulimi nje. Baadae tunagawwiwa kombania, yangu F Coy. Tunapewa green vest za kijani na bukta. Wasichana wanakazana kushusha bukta zao, kwani mapaja yako wazi. Usiku disco, tunaamshwa saa tisa usiku. Unazinduka, unaamka huku bado umelala. Maisha gani haya jamani? Baadae mchana namuuliza rafiki yangu ambaye ni service anipe mbinu za ku jongo. Ananieleza kuwa huwezi kumfundisha mtu mbinu.Unajifunza mwenyewe kutokana na mazingira yako. Baadae nagundua kuwa alisema kweli tupu.
Mikasa na matukio baada ya kujifunza mbinu za ku survive jeshini baadae.
Nilikuwa Makutupora Danger Coy wakati wa Canal Matingas. Nilikuwa nakula sehemu mbili 812 na makutu. Naanza 812 ujenzi narudi kumalizia makutu. Siku moja nikiwa 812 nikijulikana kama wa huko ikaitwa foleni bila kujua tukapelekwa madenge kupakua sementi, sikuweza kukataa kwasababu siri ingeifichuka, nilirudi makutu 6 usiku nikapambana na kibano cha kukosa disco siku iliyofuata nilikuwa taabani, nikakoma double share!
Siku nyingine nikapangwa kwa Dr Salim.A kurudi asubuhi nikakuta bogi limekatwa chita, duh bahati, nikapigwa bogi mbweni kwa captain mawazo. nilikuwa nakwenda mgulani kukiwa na magwaride.
Wimbo ninaoukumbuka, makutu mbali........, Kasimbago kaabuka.....
Lah nakumbuka ilikuwa raha. Mnakumbuka kichele! makutu upepo lazima uwe na kikopo cha rays kwenye kombati midomo isikauke ha ha ha.
Nipo mie unamkumbuka CO Thomas, Kaguo na Musira?Hivi Humu Kuna Operesheni Maisha Bora Wa 821 Kj Burombola?