Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

NimependaSana Uzi huu Pamoja na mrejesho ya "maafande ".Muhimu tunashukuru serikali kwa kurudisha mafunzo ya JKT.JKT ni mwalimu wa maisha ya uvumilivu,Upendo,Ushirikiano,Uzalendo ,Ukakamavu na ubunifu. JKT NI ZAIDI YA CHUO hasa kwa baadhi yetu tuliokulia getini na kuishi maisha legelege..JKT iboreshwe zaidi na iwe ya kudumu.
.
 
Uzi huu murua kabisa, mimi operation vyama vingi 1992/1993. Nilikuwa sijui kuimba wakati wa disco. Siku afande akanigundua kwamba sijawahi kuimbisha. Akanisimamisha niimbishe tukaanza kupiga makofi ila wimbo sina tukapiga kama dk5 afande akakasirika, nikabuni wimbo nikawaambia wenzangu nikiimbisha mnajibu........ ana madoadoa.....!
Tukaanza.
Mimi: Kanga...
Wenzangu:...ana madoadoaaaaa
Fisi...
Anamadoadoaaaa....
Nikataja wanyama na ndege wengi tuuu ........mwisho nikasema
Afande.....
Wakajibu..ana madoadoaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Nilitandikwa teke na disco likaisha mapema siku hiyo.
Jeshi raha nitawaletea kisa kingine.
 
Duuh aseeh inabidi tuheshimiane humu mtu mwaka 70 kamaliza form six [emoji23] [emoji23]. Mimi nimeshajitoa kuwa na heshima ya hali ya JUU humu tupo na baba zetu.
Afadhali umelijua hilo!
 
Du zamani sana!, Enzi hizo Baba wa taifa JKN ndio POURT, waziri mkuu ni Edward Moringe Sokoine,Gen Musuguri ndio Kinara pale juu majeshini. Kambi yangu ya ni uzalishaji mahindi JKT Mlale,Operation 'kujihami kiuchumi baada ya vita', Mkuu wa kambi ni Luteni kanali Kajembe, Meja Mandwa mkuu wa operation zote kambini, B-Coy ndio ilikuwa kombania yangu, platoon ya kwanza section ya demo ya kina Nkayamba Abeid,Nko,Solomon,Mwasha mim na kina Nyihirani, Makamanda akina Bahati, Sondora mutini kalikaka, na afande Before!, chini ya Sir major Ndaga na Lt Ndangura. Kama niliowataja wamo humu tujikumbushe jinsi tulivyohenya wakati huo. Najivunia sana kuwa katika jeshi la akiba hadi leo.
Huyo Mwasha ni R.J Mwasha aliyekuuja kuwa headmaster Mzumbe sec au!?
 
Uzi huu murua kabisa, mimi operation vyama vingi 1992/1993. Nilikuwa sijui kuimba wakati wa disco. Siku afande akanigundua kwamba sijawahi kuimbisha. Akanisimamisha niimbishe tukaanza kupiga makofi ila wimbo sina tukapiga kama dk5 afande akakasirika, nikabuni wimbo nikawaambia wenzangu nikiimbisha mnajibu........ ana madoadoa.....!
Tukaanza.
Mimi: Kanga...
Wenzangu:...ana madoadoaaaaa
Fisi...
Anamadoadoaaaa....
Nikataja wanyama na ndege wengi tuuu ........mwisho nikasema
Afande.....
Wakajibu..ana madoadoaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Nilitandikwa teke na disco likaisha mapema siku hiyo.
Jeshi raha nitawaletea kisa kingine.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Makutupora operation NIDHAMU sijawasoma humu!!
 
Jamaa yangu mmoja alikuwa SELULE kila siku[emoji23][emoji23]
 
Very Interesting.
Wale waliopitia Oljoro hatutaweza kulisahau "Shimo la Mungu" mahali ambapo tulikuwa tunaenda kutafuta kuni kuna umbali wa km 4 -5. Na yale mashamba ya mahidi likiwemo Dunia yaani ukiwa mwanzo wa shamba huoni mwisho.
Vituko vya maafande vilikuwa ni hatari. Kuruta ilikuwa unapata ujanja kulingana na mazingira yalivyokuwa.
Jikoni ilikuwa ni rotation ole wako upike chakula kibichi utapigwa drill la kutisha.
 
Tulipigwa route march danger coy nzima baada ya kuimba "Zaina Zaina mtoto wa kitanga Zaina lete raha Zaina..."

Pia kuna mwenzetu alipelekwa lupango kosa lake ilikuwa "kujongo" kazi akapewa extra drill kumbe alikuwa ana malaria kali akilalamika MP anaongeza adhabu mpaka akaanguka... akafia njiani akikimbizwa hospitali ... John's coner
 
Duuh aseeh inabidi tuheshimiane humu mtu mwaka 70 kamaliza form six [emoji23] [emoji23]. Mimi nimeshajitoa kuwa na heshima ya hali ya JUU humu tupo na baba zetu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
70 sio mchezo ata mama yangu hajazaliwa
 
Back
Top Bottom