Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Very Interesting.
Wale waliopitia Oljoro hatutaweza kulisahau "Shimo la Mungu" mahali ambapo tulikuwa tunaenda kutafuta kuni kuna umbali wa km 4 -5. Na yale mashamba ya mahidi likiwemo Dunia yaani ukiwa mwanzo wa shamba huoni mwisho.
Vituko vya maafande vilikuwa ni hatari. Kuruta ilikuwa unapata ujanja kulingana na mazingira yalivyokuwa.
Jikoni ilikuwa ni rotation ole wako upike chakula kibichi utapigwa drill la kutisha.
Mashamba dunia!![emoji23] [emoji23] [emoji23] umenikumbusha mbal sana!!
 
Danger coy 835kj Mgambo OP siri yangu [emoji23][emoji23][emoji23] mpoo
 
duuuh mmenikumbusha pale ruvu nilipojifanya fundi wa tv baadaye afande akanikuta ndani kwake na mgegeda mwanae kilichotokea nakijua mwenyewe lkn nashukuru nipo hai had I sasa
 
Ruvu JKT tulikuwa tunatoroka thru Vimbwende. Nikamalizia Mlale. Nilikatwa bogi. Shamba lilikuwa linaitwa Dunia. Magu rudisha hawa vijana kabla ya kuanza waanze JKT,adabu ilikuwa inapendeza
 
Basi na wewe utakuwa mdogo wangu mama 70 hajazaliwa.

Ila humu kuna watu wazima aiseeh heshima inatakiwa.

Mtu 70 yupo form six hapungui 68 min.
Inabidi wawe wanatusimulia na hadithi kabisa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Jayfour kumbe ni wewe? Wewe si ulikuwa ujenzi na akina Edward Nzigula na yule Engineer mwingine mjita mlikuwa mmetoka naye Mbeya Technical, alikuawa anaitwa Ngosi kama sikosei! Kole Sadiki yuko wapi?
Aisee mbona hujanitaja aisee babaangu? Au kwa vile niliwaacha kombania nikahamia chokaa kwa afande Mayila? Kazi inaisha saa 4 halafu tunaanza kuogelea ziwani, afande Jogoo na Makere wakija hatuelewi kitu.
Kule tulikuwa na akina Reuben Nkori, Busagala Masale, Haule, Mbuna, Chambo.
Wakati niko kombania mimi ndiye nilikuwa natangulia pale mbele ya mstari tukiwa na Karume Mbulwa ambaye baadaye alikuja kuwa ni RP, halafu wanafuatia wengine kama akina MC Nyamhanga, Commandoor Katani. Nawakumbuka sana wasichana wa Danger Coy akina Winifrida Bita, Eda (mnapata kichere mnakwenda kaseke), Esther Koroti, Yasinta John (kasheshe yake na afande Pima kwenye chenja unaikumbuka?, alirudia kutaja jina kama mara mia pale mbele ya hanga la wavulana D-coy).
Siku moja nikaokota filimbi. Niko na jamaa alikuwa anaitwa Mbogo Mnubi usiku katikati ya mahanga ya D na C, kule nyuma, nikawa napuliza filimbi "fiii" halafu Mbogo akawa anasema "ruka, ruka", halafu mimi naruka kichura na buti zangu pwaaa pwaaa, mahanga yote yakatimua mbio usiku chaga za vitanda zinadondoka chini watu wakadhani ni ma MP wako around. Baadaye na sisi tukakimbia kuogopa kibano sababu watu waligundua kuwa tumewachezea akili.
Mabigula ya usiku kwenda kuzima moto, tumeingia uchaka sana unaondoka na Blanketi mbili, kurudi majaliwa.
Mimi ndiye niliyekuwa naigiza sauti ya yule afande giant msukuma coplo alikuwa anaitwa Bujiku wa uvuvi. Akikukamata push-up una kosa anakwambia, "nipe zangu mbili, OC, Sir Major wa kombania naye tatu, OC naye nne,.... yaani we acha tu".
Halafu siku moja tunapiga kwata uwanja wa damu, mzee wa kadebula a.k.a commandoor Makoba akaingia ghafla halafu lisichana limoja la D-coy likaropoka "Cock up", mama yangu, kumbe amesikia! Akaanza, " nani amesema cock-up hapa, eeh nai,....jenga reli,... yaani ilikuwa ni issue, choka mbaya! Jeshini we acha tu, hadi nilitaka kuwa kujiunga nikasomee u-Rubani wa ndege szile ndogo za jeshi, Mungu hakujalia!
nimecheka sana mkuu, hasa hapo kupiga filimbi na kuruka kichura
 
Nakumbuka nilikuwa Ruvu. Coy B. Nilipata kitengo cha kufuga kuku phase 2. Asubuhi lazima ubugie mayai mabichi km matatu hivi. Ukipata nafasi siku unachoma takataka unaficha mayai kwenye moto. Moto ukiisha linatokea yai km limechemshwa. Kuruta mwenzangu alikuwa A-Coy. Alikuwa anatuibia sana kuni zetu B-Coy. 93 to 94. Sasa hivi ni Dr. Dr Kipingu upo? Nasikia upo Dar
 
Hii thread bado tu ipo hai hadi leo tokea Mwaka 2008? 😉😉
Amka na badilika. Hivi ndiyo wewe ulianzishaga hii thread? Kipindi hicho nilikuwa bado sijakufahamu. Mzee uko safi sana, naona vitu vyako kwenye Jassons TV, pamoja na kwenye Tamthilia. TV inaonekana imetulia sana pamoja na Tamthilia pia. Hongera sana mzee
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Em kama kuna watu humu waliopitia JKT kuanzia op Miaka 50 ya uhuru/ya JKT op sensa na uzalendo.
Naomba mje tupige swaga kidogo kama atakuwepo aliepita 821 itapendeza zaidi.
Mimi ni op Uzalendo.
Karibuni.
 
Mimi nimepita 821 KJ kwenye OP Miaka Hamsini ya JKT.Nilikua kombania F chini ya sargeant major Abednego na O.C wetu alikua Lt Ntwa (RIP) baade Lt. Sheng'oma Wakati huo C.O alikua Major Mrosso ambae alistaafu mwaka uliofuata.

Namkumbuka private mwenye visa na vituko sana anaaitwa John a.k.a Wezele Wezele ,namkumbuka matron Manento ,namkumbuka Lt. Minzi na Mwakibinga na private mnaa wa kwata kikosi kizima anaitwa Tarimo

Moments za bustani,shamba la mahindi na mkesha pale uwanja wa damu.Mbio za cross country na mazoezi ya pori na kupiga risasi bandia kule kwenye vijiji vya raia

Kikubwa kuliko vyote nakumbuka chenja aisee

Namkumbuka afande RSM Mundeba E.B[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ana mikwara ni hatari
 
Back
Top Bottom