Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Oljoro na Mgulani - Operation vyama vingi 1991 - 1992.
Commanding Officer (CO), Major Miruddy (RIP)
Kombania D (Danger Coy). Mkuu wa kombania, sajenti Kinama.
Mgulani - CO, Colonel Sanga (RIP)
RSM, Warranty Officer I Kitomari (RIP).
Oljoro ilikuwa ni marufuku kula bila kachumbari. Nyanya zilikuwa kibao. Tulilima shamba 'dunia' na kuchonga tofari kwenye miamba. Tofali zilijenga nyumba za askari pale kikosini. Kuni tulifuata 'shimo la Mungu'. Mwanzo maisha yalikuwa magumu kwani tulitoka mjini. Baadae maisha yalikuwa safi mno mpaka tukanenepa. Chakula kingi, unapiga kazi mwili unajengeka. Hakuna unachowaza zaidi ya kula na kazi tu. Wasichana unawaona kama 'wanaume' wenzio tu. Matamanio hakuna kabisa. Tumeiba sana mahindi shambani kwa tajiri Lasseko na kuyakaanga bisi porini kwenye madebe. Kulenga shabaha tulitumia Semi Automatic Rifle (SAR), Sub Machine Gun (SMG) AK47, 'silaha ya msaada' Light Machine Gun (LMG), G3 na machine pistol (MP7). Wengine hizo mnaziona kwenye 'action movies' tu!
Kilimo kilivyochachamaa Oljoro 'nikatorokea' mjini Mgulani. Maisha ya mjini yakawa magumu mno. Chakula hakikuwa makini kama Oljoro! Maharage yana wadudu na ugali 'mchinjo' mpaka nilikonda! Kazi ilikuwa ni kukata michongoma mpaka unanukia 'majani'! Deal ya maana ilikuwa kwenda kwenye sherehe kufunga mahema hasa majumbani kwa VIPs. Nakumbuka mzee Kingunge alikuwa na sherehe kwake akaja kikosini kwa ajili ya mahema. Tukaambiwa twende kwake tufunge mahema kisha turudi kikosini mara moja. Kufika kwa mzee Kingunge (RIP), tukapiga kazi tukamaliza baada ya masaa machache tu. Tukaenda kumuaga mzee turudi kikosini. Mzee akatuambia tubaki kwenye sherehe tumsaidie kufanya doria wakati wa sherehe pale nyumbani. Tukapewa 'mtungi' wa kufa mtu! Sherehe ikaisha usiku wa manane mzee akaturuhusu turudi kikosini Mgulani tuko 'mchupa' mbaya! Kufika 'mlangoni' mzee MP akashtukia tuko pombe. Wacha tugaragazwe!
Haya ni machache tu! Sijuti kupitia JKT!
 
Op Vyama Vingi ilikuwa 92-93 mhenga mwenzagu, hiyo ya 91-92 nafikiri ni 30 ya Uhuru.
 
Aisee 821 jk op miaka 50 ya muungano
Combania A ya makamanda ambari, chacha na msafiri huyo ambari ni Fundi wa kwata hatar huyo chacha mnaa hatari akichafukwa nyongo
Ha ha ha msafiri yake matusi utaskia Ku......Ku.......kumaaaaaaae foleni c.o alikua mketo na-miss moments za mabio kwata chenja askwambie mtu
 
Tulikuwa pamoja mkuu, ego coy.
 
Afande Ntwa alifariki kumbe?? Dahh

Afande mamboleo alikua mnaa balaa..

Nimemiss sana 821 KJ .. Kwa mujibu wa sheria op miaka 50
 
American village noma sana [emoji1][emoji1]yale matofari ya wakimbizi yalikuwa mazito si mchezo.
 
Ww kweli ni wa Burombola
 
Dah aisee me nimepita, 823 kj msange pale tulikuwa mujibu na ilikuwa operation miaka 50 ya uhuru nilikuwa B coy na afande nae mkumbuka ni ng'ombe ilikuwa 2014
Ng'ombe kwenye Op miaka 50 ya JKT alikua A coy, ilikua hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…