[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna kamanda wetu mmoja, alikuwa na mambo ya kipuuzi sana huyu bwana.......kuna cku akatukuta mi na wenzangu kama watano hivi akaanza kusema:- yani leo mwili wangu una hamu sana ya kupigwa pigwa, nyie kuruta hebu njooni hapa mnipige......tukabaki kushangaa....tumpige tena...... ghafla kwa ukali akasema pum**fu mnakataa amri ya kiongozi wenu subirini mtakiona cha mtema kuni...... tukaangaliana usoni tukasema tumuwahi kabla hajafika mbali tumpige ili kuondoa huo uzia....... tukamvaa na kuanza kumkung'uta.......weeeeeeeee........jamani hapo ndo ilikuwa balaa kwetu jamani hata huwa ctaki kukumbuka adhabu tuliyopewa kwa kosa la kumshambulia kwa kipigo kamanda wetu
Afande molel yupo kimbiji jkt nowMzalendo Mtanzania,
Umenichekesha sana juu ya kibali cha huyu bwana cha kuua watu . . . . Na umenikumbusha Court Marsha moja Ruvu JKT ilimuhukumu afande moja kifungo kwa kuwa siku za nyuma alimwamuru kuruta ashike kinyesi. Jamaa alisota sana Lupango.
Du, huyu afande aliyefuatilia uraiani ndo kanimaliza sana . . . Hajui watu walikuwa wana namna zao za kupunguza makali ya jeshi . . . Kama unakumbuka ukiwa na C, unakuwa mlinzi wa Hanger.
Nakumbuka Jeshini nilibuni taaluma ya kuwa fundi wa kutengeneza vitanda vobovu mambo yanapokuwa magumu. Nilipokuwa Buhemba nikabuni kuwa Mimi ni Kocha wa Basket Ball. Jamaa wakanishtukia baada ya muda na kunipeleka Lwamkoma kulima Pamba . . . Ndugu yangu si mchezo, kuna mashamba yanaitwa EMBAKASI (Kwa maana ya Airport), unapewa tuta ukiwa katikati mwanzo huoni wala mwisho. Chakula mnaletewa huko huko.
Bro, nilitaka kutoroka jeshi kwa machungu. Kuna huyu afande wa Kimasai anaitwa Moreli akanidaka nilikuwa na mahindi ya kuchoma ya shamba la jeshi, alikuwa na kiboko cha kama chuma chembamba, jamaa alinipiga kama mwizi . . . Mkuu nilitaka nirudi home kwa miguuu nikagundua isingwezekana. Sasa hivi nikikumbuka naona raha tu . . . . Someone should write a book of all these stories.
sisi CI alikuwa mwanamke ana kiherehere kuja ngorongoro kuamsha wavulana ikabidi siku moja tulala uchi alikimbia mno baada yakukuts pipe zimeamka ilealfajiri[emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
Siri za jandoni zinabakia jandoni. Msiwafanye watoto wakaogopa kujiunga na mafunzo ya awali ya kijeshi wakihofia hizi stories.Kwa kweli nimesisimka sana kwa yote; kwani limepelekwa mbali sana na kila mchangiaji.
Mimi nilianzia mgombo-kabuku tanga na kumalizia maramba; 1989\90.lamsingi kwa wadau wote ili historia isipotee; ni vyema ifanyike documentation na hatimaye itayarishwe video series\film.
Hapo tutakuwa tumejitendea haki wadau wote na jkt kwa ujumla.
Napendekeza iundwe team ya kukusanya matukio na habari zote zilizotokea; ili iandikwe healthy script itakayotoa best and exciting picture of what really happened in those camps.
Ni kweli kabisa maiki tango.Siri za jandoni zinabakia jandoni. Msiwafanye watoto wakaogopa kujiunga na mafunzo ya awali ya kijeshi wakihofia hizi stories.
Kuna mengine yako so exciting unapojikuta unakabiliana nayo bila kuwa na Intel yoyote "KUNYWA MAJI MENGI MOYO UELEE"
Ok hizi ni stories za JKT ila hutakuta waliopita RTS/ walioko chomboni wakisimulia haya.
Sent using Jamii Forums mobile app
838 kj,op kikwete c coy838 kj, maramba
OP kikwete
A COY
Mkuu wee ndio tulikuita mlinzi wa kudumu? Wait fulani hici au sio? Afande Erick alikuwa anakapenda ka chenja "shebele zanjaro"Mkuu tulikuwa wote asee mm kama unanikumbuka nilikuwa napenda kulinda sana anga la chini uku nilikuwa nipo karibu nakitatanda cha Ahazi na Mpepo maisha yameeenda kwa kasi sana
Nakumbuka samwel mzena alijifanya kudoji jumamosi kisa sabato alikula doso hatari la afande Erick
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu wee ndio tulikuita mlinzi wa kudumu? Wait fulani hici au sio? Afande Erick alikuwa anakapenda ka chenja "shebele zanjaro"
Mimi ndio nilikwepa kombati alizonichagulia ahaz akanirushia zikaanguka chini nikaenda kuchukua nyingine kwa afande mgeni ,mkaanza kumzomea ahaz halafu mkala doso kipind nishakimbilia michungwani
Namkumbuka ngereza alikimbia akawa anatafuta kinoma.Kumbe alihamiaga f coy bhana.Yule matron msela hivi alikuwa anafungwa sana anaitwa laida unamkumbuka?Haha yule mwingine alikuwa mweupe anaitwa kev mm ni anga la chini
Unamkumbuka ciprian ngereza kama sijajosea jamaa alikuwa analala f coy ila ni b coy alikuwa doja kinyamaa
Sent from my iPhone using JamiiForums
dah mkuu umenikumbusha afande nusu mungu ...yesu na maria noma sana..tulikua nae msange jkt huyo MTU ..anamikwala mizito sana nakumbuka siku yakupangiwa kombania walijipanga ma sir meja watano watu wakawa wanafolen nyuma yao ndo kombania yako..bas jamaa akawa anapiga mikwala sana ye kashamsulubu kawawa ..anaweza kukubadilisha vyovyote kashindwa roho tu ukimix na sula yake kama nduli amini...watu wakawa wanakimbia kufolen kwake ..dah wengne tukafolen ivo ivo kwake kinyonge ..mwisho wa siku tukaja kujua kumbe ni mtu poa t sana ...ana mikwala tu mingi..Du mmenikumbusha mbali sana.
nilikuwepo Mafinga Danger coy wakati wa ukuruta na Sir major Mulembo na afande Nusu mungu (Daniel Muungwana) alikuwa anadai eti mama yake alalamika kwa mwaka mzima alikuwa hajampelekea kichwa cha kuruta.
Baadaye nikamalizia Itende JKT na detach yake ya itaka kwenye mashamba ya mahindi yaliyoitwa mbuga. Itende alikuwako afande Bokassa siku moja tulikuwa tuweka mbolea kwenye mikahawa basi kukawa na dalili zote za kunyesha mvua. Tukamwambia hali ya hewa ni mbaya afande; akasema hapana hali ya hewa ni nzuri endeleeni lazima ng'ombe atue A coy. maana CO alishatangaza kombainia itakayoshinda kwa kilimo itapata ng'ombe. Basi mvua ikaanza kunyesha wakati mifuko iliyojaa mbolea ikiwa shambani, akaanza kumalisha chukueni mbolea mpeleke kwenye kibanda isilowane tukamwambia hapana afande hali ya hewa ni nzuri. ilibidi aanze yeye kubeba kwa kuogopa adhabu kikosini. tukamwambia hatutaki ng'ombe sisi. tulipofika kikosini tukatuta order ya CO- Bokasa amehamishwa kombania.
Maramba pale nlifanya msala mmoja wa hatari sanaAcheni kabisa,nakumbuka 92-93 nilikuwa kambi ya Maramba Op Vyama vingi, CO akiwa Col Lyaruu,nilikuwa zamu nikaacha lindo langu mimi na mwenzangu SM Eradius Temba tukaenda kugonga chupa kadhaa za boha nikamix na mnazi, kumbe MP wa zamu L/Cpl Mwankenja alipata taarifa kuwa kuna baadhi ya walinzi wameacha vituo vyao na kwenda kunywa BOHA na MDAFU, siku hiyo sitasahau sekeseke nililokumbana nalo, tukiwa njiani kurejea kwenye vituo vyetu kupitia uwanja wa mpira uliokuwa karibu na kilabu cha boha wakati tunaingia kwenye shamba la mikokoa ili tuibukie hangani kubadilisha nguo ghafla tulisikia sauti simamaa!! kucheki nikamuona Mwankenja na baka lake la MP, sio siri MP alikuwa anaogopwa vibaya sana, nilijaribu kulala mbele lakini kutokana na kinywaji nilichogonga alifanikiwa kunidaka nilijaribu kujipapatua lakini ilishindikana ikabidi nijijenge tukaanza kupiga mkono yeye anapiga combat karate, mimi napiga mchanganyiko wa Shotokan, Gojoryu na Kun fu nilimpa vitu vya uso na mbavu alivyoona namzidi alipuliza filimbi kuomba msaada kwa vile eneo la mapigano halikuwa mbali na kambi, walitokea MP wawili zaidi Cpl Nyambo na Sgt Amani masharubu, aaaah! nilikula doso la hatari pigwa virungu sana na kwata mchanganyiko ikiambatana na vichura, Pushups na kukwepa ndege kufika Q/gurd niko hoi, doso likaanza upya pigwa tifu sana, MP mmoja wa kike L/Cpl Rukia akanionea huruma sana, wakati suluba ikiendelea nikamuona Eradius Temba naye akiletwa mlangoni akiwa chini ya ulinzi wa MP Sgt Sambangula, wale waliokuwa wananisulubu wakahamia kwa Temba wakaniacha ndipo yule MP wa kike Rukia aliponitoa pale kimtindo na kunipa fatiki ya kukwangua nyasi eneo la Ofisi ya MP, nikamsikia Temba akilia kama mbuzi kwa kibano alichokuwa akikipata. Nikiwa naendelea na fatiki nikamuona 2i/c OC wa kombania yangu Lt Songela akiwa na CSM Mteule Meshi wakija mlangoni mzee Songela akiwa ameshika fimbo, nilipomuona roho ikapasuka paa!! alikuwa mzee mtata sana, baada ya kufika pale alipewa maelezo na L/Cpl Mwankenja jinsi tukio lilivyokuwa, Aisee yule mzee akaanza kunishushia tena kipigo cha nguvu na ile fimbo aliokuwa nayo.
Acha tu mkuu, op jiajiri pale ngoja nikipata wasaa nitapostUtupie hapo tuusome Mkuu
Mimi operation Kambarage 1990/1991. Oljoro/Makuyuni. Naomba niandikie mistari yote ya wimbo wa kulekule kwa chinoma/chinova! nimeusahau. Namkumbuka sana Afande Kunesa/Salum wa jikoni. Ukimwambia chakula kidogo anakujibu, mwaga kanywe maji kalale.Umenikumbusha mbali sana mie niliudhuria ile miaka ya mwishoni ya themanini (1989/90) Pale kambi ya Ruvu kombania ya B kuna afande alikuwa anaitwa Nyundo. Huyu afande hatukubahatika kumuona akiwa amefurahi kila siku sura yake ili kuwa ya kazi kazi. Mwenyewe alikuwa anajiita ndio handsome wa kwao.
Nakumbuka moja ya wimbo ambao alitufundisha muda wa disco ulikuwa wa Malela.... na mwingine ulikuwa nadhani wa kishona kama sijakosea unaitwa Kule kule kwa chinoma....
Kitu kingine nakumbuka ni ufugaji wa kuku kule phase 2 pamoja na kusimamisha minazi serengeti muda wa jioni.