Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

832 KJ bhana duh ni atar...............doso la kufa mtu,bustani kwa sana, afande Best na mabio yake ya mchana yalikera sana, ila nilikuwa napenda kuwah sana kule officers mess ili nkachukue kijogooo....hizi lugha ni walopta huko tu ndo wanaelewa.
Yaani wewe ni mimi kabisa.
Jeshini sifa ni kijogoo alfajiri kabla ya mchaka mchaka mtu umeshiba tayari
 
Alafu tukienda bustani kitengo changu ni churaaa. Maana sikuwaga na ndoo kabisa na kila siku nachezea doso la maana kwa ukosefu wa ndoo
 
Kipindi hicho Kanali Mbuge alikuwa CO, mnaa atar yan KZ za kufa mtu kwa maafande.......saiv ndo mkuu wa JKT
 
Makutupora hapo nakumbuka CO alitoa ahadi ya matofali kijijini huko kama 3000+, nikakimbilia upande wa ubao nikijua ni kitengo asee walinikuta angani wakajua nimekufa
 
Tttttttx

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa miaka ya nyuma kidogo 1982/83 Kule Mlale JKT Songea.
Ishu pale ilikuwa ni muda wa kuamka ile alfajiri saa 9 kwenda route match ambapo wasichana walitakiwa kwenda kombania kwa wavulana bigula linapolia.
Kwa kuwa muda ni usiku sana wasichana tulikuwa tunakwenda kulala kule kombania kwa hiyo unapofika ni kuvamia tu kitanda bila kujua aliyelala hapo ni nani na ikizingatiwa ni usiku baada ya kumaliza kuimba na hanga/bweni halina taa. Na tuliweza kulala na wavulana hadi hiyo alfajiri lakini hakuna aliyeweza kugeuka wala kushtuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

832 kj Ruvu
 
832 KJ bhana duh ni atar...............doso la kufa mtu,bustani kwa sana, afande Best na mabio yake ya mchana yalikera sana, ila nilikuwa napenda kuwah sana kule officers mess ili nkachukue kijogooo....hizi lugha ni walopta huko tu ndo wanaelewa.

Intake ipi ulkua maiki
 
Duh mm nlisoma enzi hakuna jkt ila nlikuwa natamani sana kwenda huko hata kwa kufosi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali Sana mkuu, ile ni kambi yangu mwaka 2015. Napenda Sana maisha ya jeshi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawatafuta ndugu zangu wa Operesheni Kambarage Ruvu JKT mwaka 1990/91.
 
Nawatafuta ndugu zangu wa Operesheni Kambarage Ruvu JKT mwaka 1990/91.

Operesheni Kambarage 1990/91, 832KJ :CO-- Luteni Kanal Urio
F-Coy
OC-Luteni Mnyomole
Mteule - Sajini meja Sanga
Wakufunzi: Sajini Taji Juma Rajabu
Sajini Taji Omari Saidi
Sajini Liundi
Matron Sajini Maingu
Koplo .....Kupaza.....( jamaa hana shida na Makuruta, yeye ugomvi na Maafande wake kila siku kupigwa Adhabu ya Ulinzi tu)
Lance Corp. Kaumbu
Vumilia wa Kujitolea : Rocky na Batuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…