Waniibia nilivoenda kuchajisha simu, si unajua kule ukiibiwa kitu unasema nimesogezewa, kauli ya kuiba ilikuwa n marufuku kuitumia, et wanajeshi siyo wezi wamekusogezea tu wakitumia watakurudishia.
Na ukweli wa Mungu nikiwa pale, siku moja tumepewa utawala wahuni wengne wakalala, sisi tukaenda ziwani kuoga na kufua, tulivyorud nguo hazijakauka tukazianika, yani naingia tu hangani na kutoka nakuta nguo hazipo mashuka na blanket, yani kama vile naota, kuangalia vzr sioni aliyeiba alafu wahuni waliokuwa wamekaa pale wala hawaonyeshi dalili yoyote kama kuna swala limetendeka. Niliwaza sasa nitafanyaje wameiba bukta, na boxer zote nne, nilikuwa nimevaa pitshort bila boxer coz nmezifua zote[emoji16], niliwaza nifanyajeee? Nikajisemea tu moyoni kuwa inabidi nijiongeze tu hakuna namna. Ule muda wa kufoleni kwa ajiri ya msosi nikamtanguliza rafk yangu na vyombo mm nikabaki hangani mwanaume nataka kufanya jambo[emoji1], walivyotoka wote nikachungulia ule upande C coy walikuwa wanaanika nguo zao nikaona zipo nyingi alafu hakuna mtu bc mwanaume nikaenda nikajichukulia singlendi mbili, boxer tatu za watu tofaut, mashuka mawili na blanket nikarud hangani mwetu nikatandika vzr blanket nikalikunja kaseti style nikaenda kufukuzia msosi. Jioni nilisikia C koi watu wanalalamika kule, eti D coy tunawaibia.
Muda wa uck C coy wakapewa doso la adabu et kwanini wakisogezewa nguo wanalia lia inamana mbinu za kivita hawajazielewa[emoji16]
But nilikuja kubabuka mwili nahis kat ya wale niliowaibiaga kuna mmojawapo alikuwa na maradhi ya ngozi, mpk now kuna ugonjwa wa ngozi huwa unanisumbua, nimetembea hospital nying mpk nikachoka, nmekunywa dawa nying mpk ndani nikawa kama muuza madawa yalivyokuwa mengi. Tiba asili wamenipga hela nao balaaaa.
Mpk saiz najuta kuiba zile nguo. Sema nilikuwa sina chaguo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]