Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Week nzima mnajificha mlikua mnakula wapi, kuoga...
 
Magesa huyu ndo yule alipata ajali??
 
Saluti kwa masoldier wote wanaozijua hizi sehemu
Mlima nguruwe
Idetero
Kwa Balali (yule gavana wa BOT)
Airport
Kawawa
Njia ya kwenda mgororo
Kitundu hall
Mwamunyange recreation

Bila kumsahau
Afande pilato (Mhenga)
Captain nkya

From kambi ya ubaridini....yaani ilikuwa ikifika night unavaa nguo zote zilizopo kwenye tranka na asubuhi maafande wanawakomoa hamrudi bwenin (angani) so mnakimbia kuifuata chai na manguo yote mwilini.

Kunakipindi kama snow inashuka maafande wanaiita "nyahenge" kwa kihehe.

Kuna siku baridi kali alfajiri kuna kuruti akajificha jalalani akalala usingizi wa pono. Kimbembe muda wa usafi watu kuchoma jalala alitoka mtu kama mzimu akazua kataharuki.

Vile vyoo vya mabanzi ambavyo hakuna kitu kinachozuia wa shimo moja asimuone mwingine. Aliwahi kuja demu akanikuta nimechutama pale akashusha kombati akashusha mzigo hakujisafisha akavaa kombati akaondoka alinifunza kuivua aibu pale kambini.

Kuna siku tunaenda kumwagilia miparachichi. Wakati tunashuka mteremko wa kutoka kambini kuingia mafinga mjini gari IVECCO ilikimbia hadi tukaacha kuimba kwa morali cha ajabu dereva afande akatoa kichwa akawa anasema kumamayo nimesema imbeni kwa morali na hapo one week before kuna ajali ilitokea ikaaua maafande.

I mic good moment una bust wali unaficha kwenye kofia ya komboti.

Kuvaa kama afande kisha mnacheki pamoja game ya EPL pale kitundu hall.

Shall out kwa maafande wangu wote mtakaopita hapa.
 
Enzi zangu pale Maramba jkt(838),Nlikua nadodge mpaka maafande wakanipa u ST wao wenyewe.

Kuna siku siwezi kusahau aisee,Nlikula shumbwela mpaka nikawa naichukia kambi,Hiyo siku nakumbuka nliiba zile gwanda za ma services man ili nkacheki game ya arsenal bahati mbaya asa wakanigundua kua ni kuruti.Aloo..[emoji22] nlikula maovyo ovyo mpaka nikadata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeee,,,,kwanza sipat picha sura ilivyokushuka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Harafu nyie mlipendelewa usafi mkaongoza ile siku ya passing off the square [emoji23] mlikua na yule Simba wa Yuda (mzee wa shambani) achana na Ngutanyi fala sana nyie D-Coy.
Mwamba hajastaafu ,kuna siku yule mzee alikua kwake na familia kwa bahati mbaya Chalii Oscar akawa anapita pale usawa wa ile kota ya ngutanyi 'mwamba aliisimamisha familia yake kijeshi adi mke na watoto ili amsalimu afandeCO
 
Kupiga mzinga
Unatembea na gogo kubwa begani ukifika mahali unaambiwa uchuchumae upige mzinga na kuruka nalo kichurachura
 
Ruvu, 90/91. E coy.
Nakumbuka kuna watu walikuwa wanalinda daraja la ruvu. Walimpiga mwizi, alieenda kuwaibia hifadhi ya chakula chao, wakamfunga kamba, asubuhi akawa amefariki. Sijui kesi yao iliishaje masikini.
 
Mwamba hajastaafu ,kuna siku yule mzee alikua kwake na familia kwa bahati mbaya Chalii Oscar akawa anapita pale usawa wa ile kota ya ngutanyi 'mwamba aliisimamisha familia yake kijeshi adi mke na watoto ili amsalimu afandeCO
Ngutanyi mzee wa IMEEEEEEELEWEEEKAAAAAAA
 
Kapteni Mbenje si Mberenje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…