Jamani ni vizuri kujikumbusha mambo yaliyopita na ni kujifunza vilevile.
Nilipomaliza Form six nilichaguliwa kwenda Bulombora JKT Kigoma, tulifika Kigoma stasheni saa 12 jioni tulikuwa kama 30 hivi, gari la jeshi lilikuja saa 4 usiku ilituchukua mwendo wa karibu masaa 3 kwenda kambini. Tulipofika tukakuta chakula kipo tayari tulipouliza maji ya kunawa namkumbuka afande aliyekuwepo anaitwa Nusu Mungu akatujibu unaulisa maji yakunawa jeshini akatuambia tunawe kwenye umande sikuamini.
Baada ya chakula ilikuwa mida ya saa 9 usiku tukapelekwa kwenye hanga kulala, kabla ya kuingia afande akatuambia kwenye hili hanga kuna vitanda vitano tu kwa hiyo atakayewahi ndiye atakayelalia kitanda, kwa vile mimi niambiwa ukifika jeshini lazima uwe shapu shapu sikujivunga,
ukachorwa mstari umbali wa kama hatua hamsini kutoka kwenye hanga filimbi ilipopulizwa nikawa mtu wa tatu kuingia tulipotimia watano afande akafunga mlango nikawa na uhakika nimepata kitanda, cha ajabu akasema sasa nyie ndio mnajifanya ki-fowadi fowadi yaani kimbelembele inabidi mlifagie hili hanga na ku-lideki, kweli tuli deki hadi kukapambazuka wakati wenzentu wakiimba tu mapambio pale nje. Hii ni experience yangu tu kama unayo ya kwako tuletee.