Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Du nilimsahau super koplo Thomas wa mafinga JKT

Huyu koplo Thomas, si alikuwa B coy (commonly known as uncle Tom), ndio ambaye mkewe alikuwa matron wa C coy? Kama ni yeye, nasikia alishafariki. Nakumbuka huyo mkewe aliwahi kuja kutuambia kuwa, eti alisema jana yake kuwa tumwagilie maua kuzunguka 'hanga'. Sisi tukamwambia kuwa, siyo kweli labda kama alisahau kutupa hayo maelekezo. Basi akasema, 'Mimi si nilisema kimoyomoyo, mlipaswa kusikia'! Yaani nilicheka, sitasahau kamwe....
 
Wanataaluma mnanikumbusha mbali sana tena . . .

Nakumbuka wakati wa kwata na kunyakua, kuna afande alikuwa analala chini kabisa akidai anataka kuhakikisha kuwa miguu yote inaenda na kushuka pamoja bila kupinda.

Ilikuwa balaa . . . Kunywa uji mwendo wa kunyakua, kula mwendo wa kunyakua nk.

Jamani tunatoka mbaaaaali kweli kweli. Sijui kama watoto wetu watakuja kupata hii experience . . . .

Very funny, halafu anaweza akawarudisha mkaanze upya wakati tayari mko usawa wa gudulia!
 
Kwa mafunzo niliyoyapata JKT natamani tungeruhusiwa kuingia msituni na SMG,G3 au AK47 ili kuanzisha vita dhidi ya MAFISADI PAPA.
 
Nilikuwa Ruvu 1983/84 operation Nguvu kazi wakati wa ukuruta. Nikahamia Ruwa kule Sumbawanga kupitia Mbeya. Nikakaa Ruwa u service miezi minne nikarudishwa tena Ruvu kumalizia pale.

Sikumbuki majina mengi tena. Lakini nakumbuka sereka sereka za kupewa dakika moja kunywa uji wa moto. Nakumbuka tunapewa kujenga misingi usiku na kisha tembo kupita juu yake huku tukipata adhabu kali kwa kutomlinda tembo asipite juu.

Nakumbuka chape chape ile ya mguu kupanda mpa usoni ili upate chakula.
Nakumbuka jamaa alikuja na kitambi chake kikaisha baada ya wiki tu.
Nakumbuka disko pale chini ya mti wa coy A.
Nakumbuka jinsi nilivyokuwa natoroka na kupanda juu ya mkorosho nikikwepa kwa wakati chini ya mkorosho huo huo wenzangu wanapigishwa kwata. Maafade bwana huwa hawaangalii juu😀

Sintasahau wenyeji wale wazaramo pale Ruvu walivyokuwa wakinasa kitimoto pori na kutuuzia kwa shilingi tano tu kwa huyo mtamu akiwa mzima shimoni na sisi tunajongo na kwenda kumshughulia porini huko.

Sisahau jinsi nilivyokuwa ninabeba panga na shoka wakati najongo na nikikutana na afande au MP anadhani kuwa nakwenda kusaka kuni kumbe niko kwenye harakati za kujongo.

Nakumbuka jinsi tulivyokuwa tunajongo kwenda Dar kwa kuamka saa 8 usiku kupitia Vibwende, tunachanja mbuga hadi mbele ya Mlandizi sikumbuki jina la vimji hivyo asubuhi saa 1 bila kuogopa simba na wanyama wakali wengine, bali tukiogopa ma MP. Mara nyingi nilijongo hivi mwenyewe na sikuwa naogopa.

Lakini nakumbuka jinsi nilivyokuwa naona moto mbele yangu usiku ninapojongo lakini siufikii hadi asubuhi.
Sintasahau jinsi afande mmoja anaitwa Helena alivyokuwa akimchukia Bwana mmoja anaitwa Aldin Mtembei na alimwandama sana mpaka akatoroka baada ya kuwa amejongo kwenda Dar na kujulikana. Ni ajabu alipata cheti cha jkt akiwa nyumbani na kwenda mlimani🙂

Sintasahau jinsi tulivyokuwa tunafuatwa na wadada waliokuwa wanataka kujongo na kuja kulala kwenye mahanga yetu ili tuwahi kujongo pamoja. Nakwambia hakuna aliyekuwa na hamu na naniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ya wakina dada hawa kwa uchovu wa mwili na akili.

Lakini sintasahau jinsi maafande walivyokuwa wanawalazimisha wadada kwa kila hali ili wafanye nao ngono na asipokubali atapata ngalambe kweli kweli na kuna siku tulipata suruba sana kwa sababu dada mmoja wa kiarabu aliitwa Salima alitokea chuo cha uhazili kama sisahau alimkataa afande mmoja na akatusurubu coy nzima hadi akakubali na mchezo ukaisha.

Kilichoniudhi jkt ni jinsi tu dada zetu wanavyochezewa na maaskari na hapa tu ndipo panafanya nilione halifai bali ni sehemu ya wadada kuwa starehe ya wakubwa fulani. Mungu naomba lipishie jeshi hili mbali kwa ajili ya wadada wetu. Na huu ukimwi sasa sijui watarudi wangapi! au wakirudi wanetu tutakaa kuwauguza maana miafande kwa uzinzi ndiyo yenyewe haiogopi kitu hii!🙁Maana viumbe hawa wa kike wakipata suruba hawana uvumilivu hata angekuwa nani anaaachia akiananiiiiiiiiiii nawambia!
 
Cola, unamsema Rwegasira yupi yule aliyekuwa fundi Bomba?

Tiba

Sikumbuki hasa alikuwa ktk kitengo gani kwa vile sisi tulikuwa tukishinda bustanini. Nakumbuka jamaa alikuwa mahiri wa kuimbisha disco na anaimba huku akicheza tena kwa hisia kweli kweli.hiyo ilikuwa burudani tosha.

Jeshini watu walikuwa wakipangwa kwenda kuchunga mbuzi walikuwa wanahesabiana kujua wametoka na mbuzi wangapi, Ee bwana ee baada ya miezi minne tu mbuzi wote wakageuka vitoto. Kisa?

kuruta walikuwa wakiwabadilisha mbuzi mmoja mkubwa kwa vitoto viwili vya mbuzi, kisha wanachukua mbuzi mwingine mkubwa kundini wanachinja na kujinafasi kwa kula nyama. Jioni wakirudi wanakuwa na idadi ile ile walopewa.Akili kichwani jeshini ni lazima zicharge.
 
Huyo jamaa(bold) kwa sasa ni Reverend fulani hivi sijui kama akikumbuka mikasa ya JKT anasemaje? haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Ni kweli kwa sasa anajihusisha na mambo ya uchungaji. Uzuri wake hakuwa na tabia mbaya bali alikuwa mchekeshaji ile mbaya na mara nyingi alikuwa sharp wa kuokoa jahazi pale alipoona jamaa wametutight. Alikuwa ktk kundi la sanaa na alikuwa bingwa wa kucheza ngoma japo kuliwahi kutokea mashindano ya kucheza ngoma kombania yetu ikashinda kutokana na usharp wa huyu jamaa kwani alienda ktk stoo ya kikosi akakwapua sare ya ngoma ya kikosi wakashangaa wakati wa shindano watu wameyavaa. hata maafande walishangaa na wakashindwa kutuchukulia hatua kwa maneno yake kuwa mengi.
 
Jamani ni vizuri kujikumbusha mambo yaliyopita na ni kujifunza vilevile.

Nilipomaliza Form six nilichaguliwa kwenda Bulombora JKT Kigoma, tulifika Kigoma stasheni saa 12 jioni tulikuwa kama 30 hivi, gari la jeshi lilikuja saa 4 usiku ilituchukua mwendo wa karibu masaa 3 kwenda kambini. Tulipofika tukakuta chakula kipo tayari tulipouliza maji ya kunawa namkumbuka afande aliyekuwepo anaitwa Nusu Mungu akatujibu unaulisa maji yakunawa jeshini akatuambia tunawe kwenye umande sikuamini.

Baada ya chakula ilikuwa mida ya saa 9 usiku tukapelekwa kwenye hanga kulala, kabla ya kuingia afande akatuambia kwenye hili hanga kuna vitanda vitano tu kwa hiyo atakayewahi ndiye atakayelalia kitanda, kwa vile mimi niambiwa ukifika jeshini lazima uwe shapu shapu sikujivunga,

ukachorwa mstari umbali wa kama hatua hamsini kutoka kwenye hanga filimbi ilipopulizwa nikawa mtu wa tatu kuingia tulipotimia watano afande akafunga mlango nikawa na uhakika nimepata kitanda, cha ajabu akasema sasa nyie ndio mnajifanya ki-fowadi fowadi yaani kimbelembele inabidi mlifagie hili hanga na ku-lideki, kweli tuli deki hadi kukapambazuka wakati wenzentu wakiimba tu mapambio pale nje. Hii ni experience yangu tu kama unayo ya kwako tuletee.
 
Facts1,
kaka pole, ila hongera hanga lenu lilikuwa hata na sakafu sementi ya kudeki? vipi madekio mlipata wapi? ndo za kudekia na maji jee mlichotea kwenye nini?

hilo ndiyo JKT mzee.
 
yule afande alichofanya ni kutuonyesha maji yanapopatikana basi ndoo madekio fagio ilibidi tuhangaike wenyewe, najua kuna wengi hawataamini lakini ndivyo ilivokuwa.
 
"Disco", mchakamchaka saa 11:45 asubuhi (na 841 KJ, JKT Mafinga muda huo sio mchezo!! Kiwinter sio cha kawaida!), miraba Idetero, mboga za majani ya kombania Dubliganga......

Ngono......
 
Vipi watu Ruvu mpo mnayakumbuka mayai, kuna siku tulienda Ruvu kwa michezo sisi wageni tukapendelewa kulinda mabanda ya kuku usiku, nilijaza trey kama mbili za mayai kwenye mifuko ya kombati ili nitoke nayo, sasa kumbe asubuhi yake kabla ya kukabidhi lindo kuna ka gwalide na mazoezi kidogo pushapu, uvingike mayai yote yalipasuka ilikuwa soo ndugu yangu.
 
Uzinzi mtupu
mtu akikupenda;kamnda akimpenda si wako maisha gani kuumizana ni hilo tu sito nasema sitolisahau
 
842 KJ, hapo ni Mlale JKT, Kuna shamba linaitwa embakassy, na kitu inaitwa bigula, hupigwa saa nyingine mpo kwenye foleni ya msosi inabidi muache, hapo ni afande Mtono (RIP) Kaanzisha kamoto makusudi ili mkazime
 
Back
Top Bottom