Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

usinikumbushe mambo ya mraba pale makutu, ilikuwa ni balaa.
 
Yale mabio ya kabla ya chakula cha mchana, Una njaa ile kinoma, halafu mnapewa route, na kukwepa kwake labda uahirishe kula
 
Unazungumzia JKT ya wakongwe au hii ya vodafasta?
Huyu anaongelea hii ya watoto.
JKT ilikua miaka ya 88 kurudi chini.
Enzi za afande Sanga, afande Mlay afande Mtono. Meja Jenerali Mkisi na tabia zake za ajabu.
Kwenye mbuzi alikua anakula Figo tuh. Sasa niambie Figo za mbuzi ngapi anaweza kushiba Jenerali?
JKT ya zile kambi nane.
Oljoro
Mgambo
Makutpora
Msange
Bulombora
Mafinga
Ruvu
Mlale.
Enzi zile kila kitu unakikuta kule kuanzia
Bukta
Green vest
Kombati
Buti
Mess tin Tena mbili
Blankerti
Yaani wewe unakwenda na mwili tu.
 

🀣🀣Duu so powa wanakwambia mwili wa jeshi roho yangu
 
Msange JKT walinikera sana.
Vyoo having partition. Yaani kijumba kina matundu kumi au zaidi na nyote mnaonana mnapofanya hiyo shughuli yenu.
Wako mawaziri na makatibu wakuu nilikua nao jkt na Jambo hili ukiwakumbusha wakiwa kwenye v8 wanajifanya hawakumbuki.
Kuna huyu waziri mpenda sifa na totoz ambaye kwa Sasa Yuko bench huyu nanihii huyu ambae hapendi kuvaa suti.
 
Kazi ya watu kumi wenzako wote wakidoji ukabakia mwenye(kwa uwoga wako kukwepa msala) utaifanya wewe pekeyako
 
Disco. Kusimama mbele za watu unaanza kuimbisha nyimbo(sio za kisiasa) niliona michosho. Mengine ya kawaida tu
 
Binafsi nilipita JKT miaka hiyo... 833 KJ OLJORO hiyoooooo. NILICHOGUNDUA NI KWAMBA JKT NI AINA FULANI YA CHEAP LABOUR ILIYOJIFICHA KWENYE MWAMVULI WA UZALENDO.
OVA.
I see hatari tupu, bilashaka utakuwa unakumbuka vizuri "Shimo la Mungu"
Na yale mashamba ya Dunia na ....
 
Nilikuwa napenda kila kitu, yaan ile kuanzia mabio hadi doso la usiku, danger coy,, kuna siku afande katupigisha doso saa 1 had saa 5, anataka kutumwaga platoon number mbili section number tano tukaanza kuimba

"afande afande tunaomba doso afande" [emoji23][emoji23][emoji23]
Serengeti walitukana kinoma,, Serengeti anakutukana unabak unashangaa tuu,,

Af unamskia coplo,,,, babaa yanafarakana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Binafsi nilipita JKT miaka hiyo... 833 KJ OLJORO hiyoooooo. NILICHOGUNDUA NI KWAMBA JKT NI AINA FULANI YA CHEAP LABOUR ILIYOJIFICHA KWENYE MWAMVULI WA UZALENDO.
OVA.
Watu na reasoning zao bana, Kama inakujakuja vile!
 
Mamaee hiyo lazima wanunee πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…