Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Possibility ipo,lakini itategemea na uhitaji wa jeshi kwa wakati huo.Nijuavyo mimi,kwa sasa jeshi linahitaji sana wataalamu wa afya,kilimo,uhandisi na wasanifu majengo na marubani na wapiganaji(wale darasa la saba na form four)

Kimsingi ,usiende jeshini kusaka ajira..Utateseka,utaumia na utajutia..Kamaa unalipenda jeshi kutoka moyoni,nenda,lakini kama unaenda kwa sababu kitaa hapasomi,utatoroka depo
Umemaliza kila kitu MTU asipoelewa hayo maelezo basi atakuwa na matatizo ya akili
 
Wakuu kwanza nashukuru kwa thread hii..Mimi Nina swali kwenu mliopita jkt,je Mara MTU unapokuwa umeapply kujiunga jkt kwa wilaya yako,je no utaratibu gan hutumika kuwaita watu kwenye interview?msaada tafadhar wakuu,
"Kama huwezi chezaa katafute refa wa kukubeba " by DARASA
 
Wakuu kwanza nashukuru kwa thread hii..Mimi Nina swali kwenu mliopita jkt,je Mara MTU unapokuwa umeapply kujiunga jkt kwa wilaya yako,je no utaratibu gan hutumika kuwaita watu kwenye interview?msaada tafadhar wakuu,
Dodoma interview tarehe 5 watu wanaambiwa njoo siku ya interview
 
Naam tulijengewa mioyo ya Uzalendo,tofauti zetu ziliwekwa kando (ukabila,udini,utajiri,umasikini) Wote tulikuwa kitu kimoja.

Kama hii JKT ya zamani ingeendelezwa na humo ukaongezwa mfumo wa taaluma mbalimbali za kujiajiri na ujasiriamali Cum VETA,........CUBA na China wasingelitupata.

Bado namkumbuka Col.Mlay , Ndani ya Mafinga.

Au VOP!!
 
Umenikumbusha mbali sana mie niliudhuria ile miaka ya mwishoni ya themanini (1989/90) Pale kambi ya Ruvu kombania ya B kuna afande alikuwa anaitwa Nyundo. Huyu afande hatukubahatika kumuona akiwa amefurahi kila siku sura yake ili kuwa ya kazi kazi. Mwenyewe alikuwa anajiita ndio handsome wa kwao.
Nakumbuka moja ya wimbo ambao alitufundisha muda wa disco ulikuwa wa Malela.... na mwingine ulikuwa nadhani wa kishona kama sijakosea unaitwa Kule kule kwa chinoma....
Kitu kingine nakumbuka ni ufugaji wa kuku kule phase 2 pamoja na kusimamisha minazi serengeti muda wa jioni.

(bold) ngoja nikuimbie: maaleee malela malela maale malela wangu namtafuta..... Maaale nasikia uko Visiga Maalee malela wangu namtafuta........ hahahahahahahahhah chezea 832 KJ wewe
 
Kwa wale waliokuwa 832 KJ Ruvu nasikia afande Meena alishafariki, aliokuwa ndio CO. mwe mleta mada umenikumbusha mbali sana! Nakumbuka siku ya range, mie nilikuwa detail ya kwanza, sasa afande alivyotoa demo hakusema kuwa ganda la risasi linadondokea hapo hapo, tulitumia njia ya kulala, sasa mie ile kukamua risasi ya kwanza si ganda likaniangukia kichwani weeeeeeeeeee nilinyanyuka ghafla kutaka kukimbia halafu mbaya zaidi bado nimeshikilia traiga kwa maana naendelea kumimina risasi, halafu hapo nyuma ndio askari wote wamekaa chini! Ilikuwa bahati kwamba afande Meena (Commanding Officer) ndio alikuwa amefika eneo la range, alichofanya aliruka kwenye gari ( si alikuwa komandoo) akaja akanishika akaniigandamiza chini hadi nikamaliza risasi zote kwenye magazine, halafu akawaambia wale makoplo nijaziwe risasi 30 kwenye smg nikapiga zote, akasema nipewe pistol, hahahahah yaani alichotaka ni kwamba hadi nizoee.
 
Naam tulijengewa mioyo ya Uzalendo,tofauti zetu ziliwekwa kando (ukabila,udini,utajiri,umasikini) Wote tulikuwa kitu kimoja.

Kama hii JKT ya zamani ingeendelezwa na humo ukaongezwa mfumo wa taaluma mbalimbali za kujiajiri na ujasiriamali Cum VETA,........CUBA na China wasingelitupata.

Bado namkumbuka Col.Mlay , Ndani ya Mafinga.

Au VOP!!
Unakumbuka Enzi za JKT kamanda kikosi ndie alikuwa mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo, kwa hiyo kuna siku mnakaa naye kama mwenyekiti wa chama hahahahahahahah
 
japo cc 2likaa miez 3 tu, ila kuna kisa ctakisau kamwe, ilikua 2013 pale msange tabora. kamanda we2 mnyakysusa alituita wote nje ya bwen nakuuliza nan kanya knyes kwenye viunga, wote kmya akasema wote lazma tuzoe kwa mkono kwa bit akaanza yeye akashka kwa mkono kdog akaweka kwenye koreo wengne fasta 2kagusa kdogo 2kaweka kwenye koreo, mabnt wa4 na jamaa 1 wakakataa et knyaa, afande akamalizia yeye. Adhabu yao alienda kufunua chemba ya mav akawapa ndo akawambia wachote mav zen akawamwagia mwilin wakae nayo kwa mda wadk 30 ndo wakaoge, ctasau cku ile mtu anamwagia mav ndo nzma.
 
Wale wa Makutupora na Ol joro.....
Oljoro nakumbuka mashamba ya Dunia na Embakasi. Siku moja tukaenda kulima miraba shamba la njiani kama unakwenda Farm, tukiwa na A Coy. Uji ukaletwa na tata la jeshi. Bravo Coy wakashusha uji wakanywa wote na A coy. Tifu baada ya hapo lilihamia hadi kwa maafande. Kulikuwa hakuna namna maana uji ushanyweka [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Sanctus,

Mimi niliamua kukwepa kwenda Tabora na kuamua kwenda Oljoro kwasababu nilikuwa na kakangu mjini Arusha. Nikajua nikitoroka nitakuwa na sehemu kwa kubugia ugali.

Basi kufika Oljoro, tukamkuta afande Dauda, (sijui kama linaandikwa hivyo) alikuwa ndio mkuu wa mafunzo. Akasema mwaka jana alitoa kibali cha kuua kruta watano, akasema aligundua haikutosha, anawaamrisha maafande mwaka huu kuua kruta mpaka 15.

Kesho yake watu kibao wakatoroka na kwenda ku report kambi zingine. Isingelikuwa kuwa na brother hapo mjini na mimi ningelirudi kule Tabora usiku huo. Baada ya muda tukaja gundua kumbe Dauda ndiye alikuwa afande poa kuliko wengine wote.

Tulikuwa na afande mmoja Mhehe alikuwa anaitwa Mduda. Alikuwa anajifanya anajua jeshi kweli kweli. Akaopoa mtoto wa maana sana. Siku moja tumemaliza jeshi tuko mlimani, akaingia mlimani hall D na magwanda, kaja kufuata mtoto wake. Maskini yule msichana alikuwa terrified, akajificha. Jamaa akasubiri pale wee, mpaka akaamua kujikata. Alifikiri yale ya jeshini yanaendelea uraiani. Tulimsanifu kweli siku hiyo.

Looh! ni miaka karibu 20 toka wengine tuondoke JKT lakini naona michapo yake inakuja tu. Waswahili tungelikuwa tunaandika vitabu, tuna mengi ya kusimulia.
Mduda [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]. Anajifanya anaujua mpiraaa [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38].
Jeshi hadi raha......mweeee
 
Oljoro nakumbuka mashamba ya Dunia na Embakasi. Siku moja tukaenda kulima miraba shamba la njiani kama unakwenda Farm, tukiwa na A Coy. Uji ukaletwa na tata la jeshi. Bravo Coy wakashusha uji wakanywa wote na A coy. Tifu baada ya hapo lilihamia hadi kwa maafande. Kulikuwa hakuna namna maana uji ushanyweka [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
Unaikumbuka kauli hii
''Leo chakula mtakula MBAUDA''
 
Unaikumbuka kauli hii
''Leo chakula mtakula MBAUDA''
Nakumbuka sana. RSM anakuja usawa wa kombania na mpo kwenye pilika za kwenda usawa wa gudulia saa saba mchana lakini mnalifikia gudulia saa tisa wakati kutoka kombania hadi usawa wa gudulia ni 70 au 80 [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38].

Afande anakwambia mmeacha magunia mangapi ya mahindi kwenu unakimbilia ugali wa jeshi, halafu anamalizia na tusi: Deemkuuk [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Mita 70 au 80
 
enzi zile makamanda hawakuwa na shule kabisa na walijitahidi kukariri maneno machache ya kingereza na kuyatumia kila mara.....nakumbuka ile adhabu ya push up!!!!!afande atakwambia ....haya...chini!down!chini!down....akimaanisha juu ..chini sasa ujifanye hujamuelewa!!!cha moto utakiona kwa kujifanya msomi!!!
Hahaa mkuu umenifanya nicheke kwasauti sana asee
 
Back
Top Bottom