Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupia tukumbukie enzi hizo compulsory tulivyokuwa tunagonga jembe,unaambaa na mraba takriban km 10.
nyahenge 841 ...Miaka ya zamani msimu wa nyahenge kozi ya awali JW Ilikuwa inafanyika hapo
Mkuu huyu nyambo alikua sio mtu mzur kabsa,,, Mimi nilipita pale nilimkuta amekua staff sagent, anapiga virungu hatar,,,Acheni kabisa,nakumbuka 92-93 nilikuwa kambi ya Maramba Op Vyama vingi, CO akiwa Col Lyaruu,nilikuwa zamu nikaacha lindo langu mimi na mwenzangu SM Eradius Temba tukaenda kugonga chupa kadhaa za boha nikamix na mnazi, kumbe MP wa zamu L/Cpl Mwankenja alipata taarifa kuwa kuna baadhi ya walinzi wameacha vituo vyao na kwenda kunywa BOHA na MDAFU, siku hiyo sitasahau sekeseke nililokumbana nalo, tukiwa njiani kurejea kwenye vituo vyetu kupitia uwanja wa mpira uliokuwa karibu na kilabu cha boha wakati tunaingia kwenye shamba la mikokoa ili tuibukie hangani kubadilisha nguo ghafla tulisikia sauti simamaa!! kucheki nikamuona Mwankenja na baka lake la MP, sio siri MP alikuwa anaogopwa vibaya sana, nilijaribu kulala mbele lakini kutokana na kinywaji nilichogonga alifanikiwa kunidaka nilijaribu kujipapatua lakini ilishindikana ikabidi nijijenge tukaanza kupiga mkono yeye anapiga combat karate, mimi napiga mchanganyiko wa Shotokan, Gojoryu na Kun fu nilimpa vitu vya uso na mbavu alivyoona namzidi alipuliza filimbi kuomba msaada kwa vile eneo la mapigano halikuwa mbali na kambi, walitokea MP wawili zaidi Cpl Nyambo na Sgt Amani masharubu, aaaah! nilikula doso la hatari pigwa virungu sana na kwata mchanganyiko ikiambatana na vichura, Pushups na kukwepa ndege kufika Q/gurd niko hoi, doso likaanza upya pigwa tifu sana, MP mmoja wa kike L/Cpl Rukia akanionea huruma sana, wakati suluba ikiendelea nikamuona Eradius Temba naye akiletwa mlangoni akiwa chini ya ulinzi wa MP Sgt Sambangula, wale waliokuwa wananisulubu wakahamia kwa Temba wakaniacha ndipo yule MP wa kike Rukia aliponitoa pale kimtindo na kunipa fatiki ya kukwangua nyasi eneo la Ofisi ya MP, nikamsikia Temba akilia kama mbuzi kwa kibano alichokuwa akikipata. Nikiwa naendelea na fatiki nikamuona 2i/c OC wa kombania yangu Lt Songela akiwa na CSM Mteule Meshi wakija mlangoni mzee Songela akiwa ameshika fimbo, nilipomuona roho ikapasuka paa!! alikuwa mzee mtata sana, baada ya kufika pale alipewa maelezo na L/Cpl Mwankenja jinsi tukio lilivyokuwa, Aisee yule mzee akaanza kunishushia tena kipigo cha nguvu na ile fimbo aliokuwa nayo.
[emoji23][emoji23] nimekutangulia kidogo 2015 OP kikwete ,821kj op Tanzania ya viwanda mko wapi tukumbushane ya bulombora ,babu wamaharage
[emoji23][emoji23][emoji23]yupo analisauti moja hatari sana kweli mkuu wee wa bulombora afande wezere pia yupo[emoji23][emoji23] nimekutangulia kidogo 2015 OP kikwete ,
Sabufa yupo kweli pale??
[emoji23][emoji23][emoji23]yupo analisauti moja hatari sana kweli mkuu wee wa bulombora afande wezere pia yupo
Wesere , boya ana mikwara yule na limwili lake..[emoji23][emoji23]
Afande Ambari naye na lisauti lake!
Mlale jkt oooooooooooh acha afande mkoka
[emoji23][emoji23]Daah Chokaa nilibanwa gogo nusu ya kufa kisha nikala stiki za Mjerumani..Ambari mzee wa kwata [emoji23][emoji23][emoji23] nakumbuka kutengeneza chokaa Na kumwagilia ziwani duuh kingine opp kikwete kunawengine bogi lilibaki walibaka sana mujibu washeria [emoji23][emoji23] yaani service man walikua wanaenda kula Serengeti wetu usiku wanavamia kama wasomali
Timamu???nyahenge 841 ...
Maafande Hawa bado Wapo? Luten Lukinga, Rissa, mazije, Kimaro. CO bado ni major maresa? Vipi Hawa Maafande kina Kevin, Hugo, stsgt makame stsgt kajimala??Wakuu mdogo wenu hapa nimepangwa MAKUYUNI ARUSHA mwaka huu tujuzane kidogo
afande ward, njovu, kapugi, captain nduguru, martin, na wengne weng
Wale waliopita kambi ya JKT Mlale, Operation Kujihami kiuchumi mwaka 1982/83 .... Tukutane hapa tukumbushane suruba tulizozipata na MM zilizotumika kuziepuka .... Hasa SM/SW wa B-Coy!.... Karibuni.