823 kj msange ,op miaka 50 ya JKT ,D-coy
kuna siku nlikua naenda duka la kikosi kukanunulia zawadi ka crush kangu kalinielewa sana kale kadada adi kakatuma washkaji,sa sku iyo tumepata mwanya kombania nikapanga nikaone kwa iyo nkasema ngoja nienden duka la kikosi nipo na mzuka hatari kunanunulia zawadi nkakuta foleni ya mstari, nkasema tu kwa sauti ya kawaida tu 'asee kuna foleni sana ntarudi bdae' pembeni kulikua na private mfupi kavaa half combat na ilikua mida ya jioni kumbe kaniskia bana, nikasikia mtu kanishika kwa nyuma nikala fingerprints za mgongo, mara kibao, nkakaa attention kupambana maana tulikua katikati ya kozi na nlikua najiweza sana tu, kugeuka nakuta ka private flani hvi kapenda sifa hakana hata mwili, nlitaka nikachote ila nkakumbuka mahabusu ukizingatia pia ni senior wangu nkavunga, basi nkala doso pale! kakaniacha, na hamua ya kumuona yule manzi ikaisha hapo nkarudi kombania
siku nyingine ya gwaride na drills zote za kurudia rudia , mnakosea mnapewa ruti, nlikua naumwa kifua kipindi hcho lakini kazi kazi watu hawaelewi, tukapewa ruti kuzunguka kikosi alafu wanakaa baadhi ya maeneo wanakata kibangala cha watano wa mwisho hao ruti yao ndo imeishia hapo wanapigwa doso balaa, tumemaliza mda wa lunch tumefoleni tunasubiri msosi tukaambiwa moto umewaka pori la kikosi tukazime kwanza , tumeenda tumezima tunarudi kambini jioni jua linazama tukapewa chakula cha mchana na usiki hapohapo me nlishindwa kula kabisa nkanywa maji tu na tonge 3, lakini cha ajabu sikuskia njaa mpaka kesho yake mda wa chai
kuna pisi moja hivi ya mzabuni ilikua inatugawia chakula kombania yetu, siku nimeenda na plate yangu akanipakulia chakula alafu akaanita jina langu 'flani' uku ananipakulia chakula mpaka leo sijui alijuaje jina langu, hata kwenye platoon yangu wengi tulikua hatujuani majina, hatukua na mda wa kusocialize sio siri ila sura tu ndo tunajuana