Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Sitosahau kwa wale tulioanzia Mafinga JKT enzi za kanali MLAY, then baadhi ya vijana tuliosoma masomo ya sayansi tukachaguliwa kwenda JWTZ, pale Twalipo camp Dar, kwenye interview ya u pilot. Kwa wale ambao hatukutaka kujiunga na JWTZ si wakaamua kuturudisha makutupora JKT ili kumalizia mafunzo ya JKT. Bwanaaa wee pale Makutupora si wakaanza kutupiga drill na mazoezi ya kutukomoa?? Tuliotoka Mafinga tukaamua kutoroka pale Makutupora na kurudi zetu Mafinga, aisee siwezi sahau ile mission impossible. Tulitoroka kwa kutoka mmoja mmoja from kwenye hanga to the meeting point vichakani, then baada ya kuona tumetimia robo tatu (wengine walibadili mawazo hawakuja) tukaanza safari (hiyo ni saa 8 usiku!!) ya kwenda Dodoma mjini kwa mguu, kupitia porini kwenye mitunduru. All in all mwishowe tuliingia Mafinga JKT baada ya siku 2 au 3 kama sijakosea, na bahati nzuri tukapokewa vizuri tuu, daaah.
Hawakutumwa MP kweli kutoka makao makuu kuwafuata Mafinga ?
 
Hawakutumwa MP kweli kutoka makao makuu kuwafuata Mafinga ?
Hawakutumwa mkuu, in fact sisi watu karibia 25 tuliotoroka tuliwasaidia wengine waliobaki (kumbuka tulikuwa vijana zaidi ya 100 au 150 kutoka makambi mbalimbali ya JKT, ikiwemo na wa Makutupora, ambao wote tulimwagwa hapo Makutupora). Baada ya sisi kutoroka huku nyuma walipopiga roll call wakagundua hatupo. Hii iliwastua sana maana miaka ile waliokuwa wanatoroka JKT ni wale wanaojitolea na si wale wa mujibu wa sheria kama sisi. Kumbuka kwamba yale mateso yao ya kutukomoa ni issues za hawa maafande wa rank za chini, sasa taarifa zilipomfikia mkuu wa kambi na Mgt yake wakapaniki sana kwani kule HQ wakawachimba mkwala watoe majibu tumeenda wapi vijana wengi namna hiyo? Kwa hiyo ikawa mshike mshike kambi nzima, na wale wengine waliobaki ikabidi mazoezi yote yasimame. Eventually kanali Mlay wa Mafinga ndiye akatoa ripoti HQ kwamba vijana wake wako Mafinga na Amewapokea wote na angependa waendelee pale pale Mafinga,na ndivyo ilivyokuwa.
 
Hawakutumwa mkuu, in fact sisi watu karibia 25 tuliotoroka tuliwasaidia wengine waliobaki (kumbuka tulikuwa vijana zaidi ya 100 au 150 kutoka makambi mbalimbali ya JKT, ikiwemo na wa Makutupora, ambao wote tulimwagwa hapo Makutupora). Baada ya sisi kutoroka huku nyuma walipopiga roll call wakagundua hatupo. Hii iliwastua sana maana miaka ile waliokuwa wanatoroka JKT ni wale wanaojitolea na si wale wa mujibu wa sheria kama sisi. Kumbuka kwamba yale mateso yao ya kutukomoa ni issues za hawa maafande wa rank za chini, sasa taarifa zilipomfikia mkuu wa kambi na Mgt yake wakapaniki sana kwani kule HQ wakawachimba mkwala watoe majibu tumeenda wapi vijana wengi namna hiyo? Kwa hiyo ikawa mshike mshike kambi nzima, na wale wengine waliobaki ikabidi mazoezi yote yasimame. Eventually kanali Mlay wa Mafinga ndiye akatoa ripoti HQ kwamba vijana wake wako Mafinga na Amewapokea wote na angependa waendelee pale pale Mafinga,na ndivyo ilivyokuwa.
Kama CO wenu aliingilia hilo suala basi soo lenu liliisha kiutamu sana
 
Uzi huu murua kabisa, mimi operation vyama vingi 1992/1993. Nilikuwa sijui kuimba wakati wa disco. Siku afande akanigundua kwamba sijawahi kuimbisha. Akanisimamisha niimbishe tukaanza kupiga makofi ila wimbo sina tukapiga kama dk5 afande akakasirika, nikabuni wimbo nikawaambia wenzangu nikiimbisha mnajibu........ ana madoadoa.....!
Tukaanza.
Mimi: Kanga...
Wenzangu:...ana madoadoaaaaa
Fisi...
Anamadoadoaaaa....
Nikataja wanyama na ndege wengi tuuu ........mwisho nikasema
Afande.....
Wakajibu..ana madoadoaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
Nilitandikwa teke na disco likaisha mapema siku hiyo.
Jeshi raha nitawaletea kisa kingine.
[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Wazalendo;

Moja ya sehemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma.

Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss

  • Ugali na korosho mnapojongo kambini
  • Mihogo ya Vibwende kwa Babu
  • Wali na Maembe
  • Uji wa Mestin ya Jeshi
  • Bukta na Green Vest
  • Kuokota kuni
  • Bustani
  • Michezo
  • Disco
... Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn wa Tanzania. Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk...

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia.

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa. . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.


Je, wewe unakumbuka nini?

Mchakamchaka saa 10 za usiku toka Bulombora kambini hadi Mwakizega na siku niliyotaka kuliwa na mamba ziwani ( Ziwa Tanganyika).
 
Uwanja wa Damu..Dah..Kunja ngumi usiweke bata..
Mabio Itaga,Inonelwa,Yombo Mbola..
 
Mtanzania,

Mzalendo Mtanzania,

Umenichekesha sana juu ya kibali cha huyu bwana cha kuua watu . Na umenikumbusha Court Marsha moja Ruvu JKT ilimuhukumu afande moja kifungo kwa kuwa siku za nyuma alimwamuru kuruta ashike kinyesi. Jamaa alisota sana Lupango.

Du, huyu afande aliyefuatilia uraiani ndo kanimaliza sana. Hajui watu walikuwa wana namna zao za kupunguza makali ya jeshi. Kama unakumbuka ukiwa na C, unakuwa mlinzi wa Hanger.

Nakumbuka Jeshini nilibuni taaluma ya kuwa fundi wa kutengeneza vitanda vobovu mambo yanapokuwa magumu. Nilipokuwa Buhemba nikabuni kuwa Mimi ni Kocha wa Basket Ball. Jamaa wakanishtukia baada ya muda na kunipeleka Lwamkoma kulima Pamba. Ndugu yangu si mchezo, kuna mashamba yanaitwa EMBAKASI (Kwa maana ya Airport), unapewa tuta ukiwa katikati mwanzo huoni wala mwisho. Chakula mnaletewa huko huko.

Bro, nilitaka kutoroka jeshi kwa machungu. Kuna huyu afande wa Kimasai anaitwa Moreli akanidaka nilikuwa na mahindi ya kuchoma ya shamba la jeshi, alikuwa na kiboko cha kama chuma chembamba, jamaa alinipiga kama mwizi. Mkuu nilitaka nirudi home kwa miguuu nikagundua isingwezekana. Sasa hivi nikikumbuka naona raha tu. Someone should write a book of all these stories.
Hahahaha

Nilikuwa Rwamkoma miaka 10 iliyopita
 
Kuna mwana JF yeyote aliyesoma Kigurunyembe Seconadary 1981-1984? Ningependa sana kukumbuka enzi zetu za shule, wakati Head Master akiwa Mr. Magere na Second Master Mr. Betelo!!!
Francis wambura magere
 
uchungu%20wa%20utamu.jpg
 
Mmenikumbusha mbali sana.. Mimi nilukuwa Ruvu, halafu Mgulani (kwata la uhuru) halafu Mlalakuwa, miaka ya mwanzoni mwa 1990. Ruvu nilikuwa Fcoy (makondeko) na kina Afande kesi, simba, mohamed na salehe. CO alikuwa ni kanali urio (nasikia ni marehemu). Nakumbuka kulikuwa nafande mmoja alikuwa anaitwa Mizani na alikuwa mpenzi sana wa mabinti (alikuwa anawasubiri vichakani wakati wanatoroka).

Nyimbo ninazokumbuka ni kama !moto wayaka mama ..moto wayaka..wayaka wayaka", Zaina zaina..zainabu wangu usiku silali" na "canadia ee canadian ee.. (nimesahau maneno hapa). Nilifurahi sana jeshini kuliko hata shuleni (boarding).

Lidumu Jeshi La Kujenga Taifa!!
Mkuu umenikumbusha mbali sana, hasa huo wimbo wa Zaina Zaina…..kweli maisha hayarudi nyuma…
 
Back
Top Bottom