Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 702
unapakuliwa ugali, mchuzi wa nyama mwepesiii, na bonge ya fupa halina nyama, unauliza mbna umenipa mfupa mtupu? Unajibiwa kaumbe ng'ombe wako asiye na mfupa umlete tumpike
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kazi kweli kweli hususan unapotaja RUVU JKT.
Nilipita hapo enzi CO akiwa Col Meena, Na Nilikuwa Kombania A iliyokuwa inaongozwa na Afande Capt Othman. na Sirmega Stuke, nawakumbuka pale akina Cpl Nyundo,Sahani, Mwambigu, Chenga, Sgt Mazani (mzee wa totoz), Urassa , Sgt Kitomali (ambaye wiki mbili nilipokuwa Dar nilikutana nae siku hizi ni kiongozi wa Mgambo wa jiji la Dar)na maafande wangu akina Lt Nyoni, Sylas na wengine.
Nimestuka sana mtoa mada alipokumbusha kwa BABU na vibwende. Bila kusahau mayai ya phase A na mashamba kule Phase B.
Kweli JKT tumejifunza mengi na tumetoka mbali
Nimemkumbuka kalikuwa kanaitwa afande Msagati... Sikonge!!
Lakini mimi nawewe tumepishana mwaka!..mimi 88-89!na jamaa alikuwa corporalBasi huyu enzi mie nipo hapo hakuwepo. Sikumbuki kabisa na kama ningelikuwepo basi ningelimkumbuka maana hilo jina limekaa Kinyamwezi sana. Kama sikosei ni jina la Chief wa Wanyamwezi kwa sasa.
Lakini mimi nawewe tumepishana mwaka!..mimi 88-89!na jamaa alikuwa corporal
Katika hiyo picha unafahamu mtu maana ilichukuliwa oljoro GIUSEPE??...when was it??Nakumbuka kuchimba shimo la biogas kwenye eneo ambapo ni jiwe tupu pale oljoro,tulikuwa tunawasha moto kwanza jiwe likipata joto tunapiga nyundo kisha tunaondoa vipande kwa mataruma.Aliyekuwa msimamizi ni staff sgt Mgonja. Sgt major wetu alikuwa Maduma,CO major Mirudi.
Chita unapelekwa kwa bogi...tapeli mmoja ambaye hakusoma A level wala kwenda jeshini aliwahi kujisingizia kwamba jeshini yeye alipangwa chita..mpaka Leo nikiukumbuka uongo wake nachekaHivi kuna watu huku walikwenda JKT CHITA? Maana nasikia huku ndipo kulikuwa na jeshi haswa!! Tungependa kujua kulikuaje huko. Nasikia makuruta walikuwa wanavunwa sana na huwezi kutoroka (simba n.k).
Unanikubusha Maduma,huyo alikuwa OC wangu kabla ya Lt na captains hawajawa wengi,ni mgogo mmoja mpenda vimwana (makuruta waoga).Hayo yote waliyoongea wakubwa hapo juu yamenifurahisha na kunikumbusha mbaali sana,,,,nakumbuka mwaka 1993(operation miezi sita) mie na rafiki yangu aitwae gwakisa tulianza safari tokea mbeya kwenda arusha kambi ya oljoro,,,tulifika njia panda ya oljoro hiyosehemu inaitwa mbauda, mie na jamaa yangu tukashauriana ngoja tupate bia hata moja moja pale,,eneo hilo lilikuwa linauzwa bia pamoja na mbege,, tukaagiza bia moja moja na kikopo cha lita moja ya mbege,,,,,,,kwenye kona kabisa kulikuwa na bwana mmoja amekaa anakunywa mbege huku akituangalia sana,,,,,na kwa kuwa stori zetu yule mhudumu dada alitusikia kwamba tunaelekea kambini oljoro,,,akamstua yule bwana aliekaa pale pembeni akatumaki sura zetu vizuri,,,,,kesho yake yule bwana alizunguka kombania zote akitutafuta kumbe ni corporal alikuwa anaitwa HEKAHEKA akatudaka wote tuko kombania moja E(eagle coy) saa meja alikuwa anaitwa maduma ,,,huyu bwana alisema kuruta unakunywa bia wakati hekeheka anakunywa mbege leo mtakoma,,,, tulipewa adhabu sitosahau.
Jeshi la kujenga taifa kwa sababu ya mfumo duni ya utawala na Uthibiti halikuweza kujiendesha. Lilifutwa/kuondolewa kwa sababu za kiuchumi. Malengo ya uanzishaji wake ndio yanayopelekea msukumo wa kulirudisha uliopo sasa.Kunatofauti kubwa Kati ya Mtu aliyepita jeshini na asiyepita mfano nidhamu na uvumilivu.Je wadau? Kulikuwa na sababu yoyote ya msingi ya kufuta huu utaratibu wa JKT, eti magreatthinkers?
mimi ni member wa program ya chama June 1989-june 1990. nilihenya JKT NIKIANZIA HQ MLALAKUWA NA KUSAFIRISHWA KWA TRENI KWENDA MGAMBO JKT. KWANZA SAFARI YENYEWE TOKA DAR TULIKUWA KAMA MATEKA, HALAFU TULIKAA KWENYE MAUNGIO YA TRENI HADI KOROGWE SABABU HATUKUBUKIWA TICKETS. HAMNA NOMA TUKAINGIA KOROGWE NA MLORI KUTOKA MGAMBO JKT. HAO SEGERA THEN KABUKU KUELEKEA MGAMBO ABOUT 15KMS TOKA JUNCTION YA KABUKU. TULIPOFIKA MGAMBO HAKIKA NILITAMANI ARDHI IPASUKE. TUKAGAIWA VIFAA VYA KIJESHI NGUO PITSHOT, GREEN TSHIRT, BLANKET, MESTINI NA SAHANI NK. NIKAPANGIWA KOMBANIA B. WAKATI HUO CO WA KIKOSI ALIKUWA LUTENI KANALI CHALE, PANDE LA BABA.Jamani, wale wa maramba 838KJ, mpo?
Tukumbushane tulivyokuwa tunakula rojo la kakao.
Wale wa Makutupora na Ol joro.....
mmenikumbusha mbali wakuu 1983/4 Makutupola.