Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nilikutana na Meena kwenye kisherehe fulani hapo Ruvu Secondary kwa Mwalimu Mkuu enzi hizo eti na mie nikiwa mmoja wa wafanyakazi wachache wa Serikali wanaoishi Mlandizi. Sherehe ilikuwa ya kumuaga Meena baada ya kupata uhamisho kutoka hapo Mlandizi kwenda sijui wapi, nimesahau.

Sikuamini macho yangu kumuona Meena na tena hadi ninaongea naye na nikikumbuka jinsi sifa alizokuwa akipewa za ukali.

Jamaa yangu alinipa pia sifa za Kitomali, lohhh!!!

Ruvu JKT sikuwahi kabisa kufika ingawa nilikuwa naishi si mbali sana na hiyo kambi.

Gone those Old good days.
Kazi kweli kweli hususan unapotaja RUVU JKT.

Nilipita hapo enzi CO akiwa Col Meena, Na Nilikuwa Kombania A iliyokuwa inaongozwa na Afande Capt Othman. na Sirmega Stuke, nawakumbuka pale akina Cpl Nyundo,Sahani, Mwambigu, Chenga, Sgt Mazani (mzee wa totoz), Urassa , Sgt Kitomali (ambaye wiki mbili nilipokuwa Dar nilikutana nae siku hizi ni kiongozi wa Mgambo wa jiji la Dar)na maafande wangu akina Lt Nyoni, Sylas na wengine.

Nimestuka sana mtoa mada alipokumbusha kwa BABU na vibwende. Bila kusahau mayai ya phase A na mashamba kule Phase B.

Kweli JKT tumejifunza mengi na tumetoka mbali

 
Mimi namkumbuka afande Bwire,Afande Masori na Lance corporal Mponda,bila kumsahau Mwakililo na Kaduga wa A-Coy hapo Mafinga jkt op miaka 25 ya jkt walivyokuwa wakituhenyesha sintasahau yale mashamba ya mahindi jina limenitoka na sintasahau zile bisi ambazo wakati huo zilikuwa kama almasi na sintasahau tulivyokuwa tukibast na kujongo asubuhi asubuhi kwenda john's corner kulifresh, pia lile winter la pale mafinga we acha!
 
Basi inawezekana huyu jamaa alikuwa COY nyingine au alihamishiwa sehemu kama Miyemba, kule bwawani nk.

Sikumbuki kabisa jina lake. Unajua wakati mwingine walikuwa wakifanya kosa, wanapelekwa sehemu ya mbali na Kambi.

Nakumbuka enzi zetu, Sajenti Wawa sijui (Mdogo wake Mwiru wa A-Coy) alikosana na nani sijui, wakamlima kwenda kulinda mashamba nyani wasile mahindi. Alikuwa kila siku na bunduki yake shambani.....
Lakini mimi nawewe tumepishana mwaka!..mimi 88-89!na jamaa alikuwa corporal
 
Nakumbuka kuchimba shimo la biogas kwenye eneo ambapo ni jiwe tupu pale oljoro,tulikuwa tunawasha moto kwanza jiwe likipata joto tunapiga nyundo kisha tunaondoa vipande kwa mataruma.Aliyekuwa msimamizi ni staff sgt Mgonja. Sgt major wetu alikuwa Maduma,CO major Mirudi.
 
Nakumbuka kuchimba shimo la biogas kwenye eneo ambapo ni jiwe tupu pale oljoro,tulikuwa tunawasha moto kwanza jiwe likipata joto tunapiga nyundo kisha tunaondoa vipande kwa mataruma.Aliyekuwa msimamizi ni staff sgt Mgonja. Sgt major wetu alikuwa Maduma,CO major Mirudi.
Katika hiyo picha unafahamu mtu maana ilichukuliwa oljoro GIUSEPE??...when was it??
 
Last edited by a moderator:
Keff,
Umenikumbusha Mafinga. Nilikuwa hapo kabla yako 1983-84. Afande Mpogolo ulumkuta?
Kwetu sote Jeshi bomba. Mchakamchaka na mwendo wa Kunyakua Nyakua, kushtua, kuchoma mahindi, na viazi(ving'amba) kwa Ulasi asubuhi! Vijana wetu cku hizi hawajui hii!
Uzalendo++
 
Hayo yote waliyoongea wakubwa hapo juu yamenifurahisha na kunikumbusha mbaali sana,,,,nakumbuka mwaka 1993(operation miezi sita) mie na rafiki yangu aitwae gwakisa tulianza safari tokea mbeya kwenda arusha kambi ya oljoro,,,tulifika njia panda ya oljoro hiyosehemu inaitwa mbauda, mie na jamaa yangu tukashauriana ngoja tupate bia hata moja moja pale,,eneo hilo lilikuwa linauzwa bia pamoja na mbege,, tukaagiza bia moja moja na kikopo cha lita moja ya mbege,,,,,,,kwenye kona kabisa kulikuwa na bwana mmoja amekaa anakunywa mbege huku akituangalia sana,,,,,na kwa kuwa stori zetu yule mhudumu dada alitusikia kwamba tunaelekea kambini oljoro,,,akamstua yule bwana aliekaa pale pembeni akatumaki sura zetu vizuri,,,,,kesho yake yule bwana alizunguka kombania zote akitutafuta kumbe ni corporal alikuwa anaitwa HEKAHEKA akatudaka wote tuko kombania moja E(eagle coy) saa meja alikuwa anaitwa maduma ,,,huyu bwana alisema kuruta unakunywa bia wakati hekeheka anakunywa mbege leo mtakoma,,,, tulipewa adhabu sitosahau.
 
Hivi kuna watu huku walikwenda JKT CHITA? Maana nasikia huku ndipo kulikuwa na jeshi haswa!! Tungependa kujua kulikuaje huko. Nasikia makuruta walikuwa wanavunwa sana na huwezi kutoroka (simba n.k).
Chita unapelekwa kwa bogi...tapeli mmoja ambaye hakusoma A level wala kwenda jeshini aliwahi kujisingizia kwamba jeshini yeye alipangwa chita..mpaka Leo nikiukumbuka uongo wake nacheka
 
Hayo yote waliyoongea wakubwa hapo juu yamenifurahisha na kunikumbusha mbaali sana,,,,nakumbuka mwaka 1993(operation miezi sita) mie na rafiki yangu aitwae gwakisa tulianza safari tokea mbeya kwenda arusha kambi ya oljoro,,,tulifika njia panda ya oljoro hiyosehemu inaitwa mbauda, mie na jamaa yangu tukashauriana ngoja tupate bia hata moja moja pale,,eneo hilo lilikuwa linauzwa bia pamoja na mbege,, tukaagiza bia moja moja na kikopo cha lita moja ya mbege,,,,,,,kwenye kona kabisa kulikuwa na bwana mmoja amekaa anakunywa mbege huku akituangalia sana,,,,,na kwa kuwa stori zetu yule mhudumu dada alitusikia kwamba tunaelekea kambini oljoro,,,akamstua yule bwana aliekaa pale pembeni akatumaki sura zetu vizuri,,,,,kesho yake yule bwana alizunguka kombania zote akitutafuta kumbe ni corporal alikuwa anaitwa HEKAHEKA akatudaka wote tuko kombania moja E(eagle coy) saa meja alikuwa anaitwa maduma ,,,huyu bwana alisema kuruta unakunywa bia wakati hekeheka anakunywa mbege leo mtakoma,,,, tulipewa adhabu sitosahau.
Unanikubusha Maduma,huyo alikuwa OC wangu kabla ya Lt na captains hawajawa wengi,ni mgogo mmoja mpenda vimwana (makuruta waoga).
 
Je wadau? Kulikuwa na sababu yoyote ya msingi ya kufuta huu utaratibu wa JKT, eti magreatthinkers?
Jeshi la kujenga taifa kwa sababu ya mfumo duni ya utawala na Uthibiti halikuweza kujiendesha. Lilifutwa/kuondolewa kwa sababu za kiuchumi. Malengo ya uanzishaji wake ndio yanayopelekea msukumo wa kulirudisha uliopo sasa.Kunatofauti kubwa Kati ya Mtu aliyepita jeshini na asiyepita mfano nidhamu na uvumilivu.
 
Na wale jamaa zangu wa Mgambo JKT kule Tanga hasa wa operation Nidhamu hebu tujikumbushe ya Kanali Mtono na binocular lake.Halafu vile2 tuwakumbuke BB(Boniface Bufumba-kula mavi) na Kazungu wa mwendo wa kunyakua nataka kusoma namba za viatu vyenu.
 
Jamani, wale wa maramba 838KJ, mpo?
Tukumbushane tulivyokuwa tunakula rojo la kakao.
mimi ni member wa program ya chama June 1989-june 1990. nilihenya JKT NIKIANZIA HQ MLALAKUWA NA KUSAFIRISHWA KWA TRENI KWENDA MGAMBO JKT. KWANZA SAFARI YENYEWE TOKA DAR TULIKUWA KAMA MATEKA, HALAFU TULIKAA KWENYE MAUNGIO YA TRENI HADI KOROGWE SABABU HATUKUBUKIWA TICKETS. HAMNA NOMA TUKAINGIA KOROGWE NA MLORI KUTOKA MGAMBO JKT. HAO SEGERA THEN KABUKU KUELEKEA MGAMBO ABOUT 15KMS TOKA JUNCTION YA KABUKU. TULIPOFIKA MGAMBO HAKIKA NILITAMANI ARDHI IPASUKE. TUKAGAIWA VIFAA VYA KIJESHI NGUO PITSHOT, GREEN TSHIRT, BLANKET, MESTINI NA SAHANI NK. NIKAPANGIWA KOMBANIA B. WAKATI HUO CO WA KIKOSI ALIKUWA LUTENI KANALI CHALE, PANDE LA BABA.
HAPO MGAMBO VIKAANZA VITUKO, MWENDO WA KUNYAKUA NCHI KUMI NA TISA TOKA ARDHINI AFANDE KAINAMA KUANGALIA UNAVYORUSHA MGUU. KALI ZAIDI NI UWANJA WA DAMU SIKU TUNAANZA HAKIKA TULIKIONA CHA MTEMA KUNI MGUU PANDE TOKA SAA TATU HADI SAA NANE MCHANA. TULIKOMAA KWELIKWELI NA KUKIMBIZWA ILE MBAYA. A FEW DAYS LATTER TUKAENDA DEPOT KUSOMBA MCHANGA KWENYE MTO MMOJA PANDE ZA MAGHARIBI, BWANA JONAS ATANIKUMBUSHA. KULE TULIKAA FOR ALMOST ONE WIKI. TUKAACHANA NA PARADE NA KUHENYA KWA MUDA. MGAMBO NAKUKUMBUKA KWA MACHUNGWA MENYU ZOTE NI MACHUNGWA TU HATA UKIJONGO NI KULA MACHUNGWA KWA KWENDA MBELE. BAADA YA MWEZI 1 TULIKATWA BOGI TUKAPELELKWA MARAMBA 838KJ USIKU KWA USIKU TUKAAINGIA MARAMBA ASUBUHI NA MAPEMA. NAKIKUMBUKA KIWESE. ALMOST WALE WOTE WALIOKUWA MASELULE WA MALARIA KALI TULIPIGWA BOGI, RAFIKI YANGU SWAI ATANIUNGA MKONO. AT LEAST LIFE AT MARAMBA WAS A LITTLE BIT BETTER TUKAENDELEA NA MSOTO FOR ALMOST THREE MONTHS TULIPOPASS OUT DESEMBA 1989. LAKINI PARADE LA AFANDE, MAJOR MWAKISYALA LILINIMALIZA MZEE HUYU ALIKUWA HACHEKI AKITOA AMRI ZAKE AMAENINU KAMA MVUA ZA RADI. HALI YA KAMBI VIFAA DUNI NA VITANDA DUNI VYA KARNE YA 6 BC HASA KULE MATEMBONI KOMBANIA C NA D TULILALIA. NAKUMBUKA SIKU MOJA NILIPATA B BAADA YA KUMEZA PILTON KUPUNGUZA ICTCHING YA CHLOROQUINE. TUKAENDA BUSTANINI CHINI YA SERVICE MEN JACKSON SAMUEL (BWANA SHAMBA) KULE NIKASEPA NIKAKIMBILIA BWENINI. MITAA YA SAA 3 HIVI AFANDE SGT MWITA CHACHA AKAJA KUKAGUA WALE WENYE VYETI VYA RUHUSA MIMI SINA YOU KNOW WHAT I DID. NILITOKA CHUMBANI NIKASIMAMA NYUMA YA KIAMBAZA CHA UKUTA WA STORE NIKASOGEZA MPINI WA JEMBE KUMPOTEZEA AFANDE ASIJUE PALE KUNA MTU NIKAMINYA PUMZI KIMYA. AFANDE AKACHEKI MPINI WA JEMBE ULISOGEZWA MBELE KIDOGO AKAAMINI HAKUTA KITU. NILIBANA PUMZI HADI ALIPOPOTEA THEN NIKARUDI BWENINI KUENDELEA NA STORI NA JAMAA WALIOKUWA NA VIBALI. HAKIKA WALE WOTE WALIOPITIA JKT WANAJUA NINI KINGENIPATA SIKU ILE, MUNGU MKUBWA ALNIOKOA.
 
Uchaka.........that was the real part of JKT man.....sio siku hizi kuuza matrekta

camp+001.jpg
 
Back
Top Bottom