Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nimekumbuka mbali wakuu! Op. Vyama Vingi- 91/92; Kikosi 836KJ, OLJORO JKT, MAKUYUNI subdetach Arusha, Force No XXXX. Mashamba makubwa ya Mahindi Oljoro, Dunia na Embakasi. Sehemu ya kujongo: korongoni.

intake hiyo kuna kuruta walichukuliwa kwenda Dar ili wakasomee upailoti zaidi ya watu 20 tukawa tunawaita mapailot, baadae walianza kurudi mmoja mmoja kwa kushindwa mazooezi ya huko na tukawa yunawaita 'unfit' nadhani alifanikiwa jamaa mmoja tu toka Oljoro jina lake Ali Ruga.... sikumbuki vizuri, nadhani sasa yuko kikosi cha anga Ngerengere.
 
Nakumbuka niliimba wimbo huu "Siasa yetu hapana mbaya isipokuwa maafande ndiyo wabaya" Afande aliposikia hivyo akatuamuru kuruka kichura akiwaamuru wenzangu wamtaje aliyeimba wimbo ule hawakunitaja. Jeshi lazima uwe msiri.
 
hiyo picha hapo juu kasoro ninayoiona ni hao jamaa waliovaa saa. ilikuwa hairuhusiwi kuvaa saa. ukivaa saa afande anakuuliza 'unavaa saa ili ujipangie ratiba zako?'
 
Umemsahau Mkini na SCUD, huyu scad alikuwa balaa huyu mnyiramba alinipiga drill siku mbili nipo kitandaani, ila HuyoLT Mohd alikuwa mtu wa totoz sana. mimi sitasahau kilimo cha tumbaki kilivyo kigumu kuanzia kuotesha mbegu kiangazi kupandaa kugrade na kukausha kwenye bani, acha mchezo, cchini ya usimamizi wa Nuru Wema Lori.
 
intake hiyo kuna kuruta walichukuliwa kwenda Dar ili wakasomee upailoti zaidi ya watu 20 tukawa tunawaita mapailot, baadae walianza kurudi mmoja mmoja kwa kushindwa mazooezi ya huko na tukawa yunawaita 'unfit' nadhani alifanikiwa jamaa mmoja tu toka Oljoro jina lake Ali Ruga.... sikumbuki vizuri, nadhani sasa yuko kikosi cha anga Ngerengere.
Basi tulikuwa operesheni moja mkuu,maselule wengi walikatwa bogi kwena Makuyuni.Hao mapailot wengi waliogopa medical test ya kuchunguliwa ndani ya 'masaburi' na mchina kuangalia kama una magonjwa/maambukizi huko nyuma.
 
Uchaka.........that was the real part of JKT man.....sio siku hizi kuuza matrekta
camp+001.jpg
Lusajooo.....and other people I know. Those were the days when boys were boys and girls were girls.
 
JKT enzi hizo ilikuwa siyo mchezo nakumbuka nilikuwa operation Kambarage Masange JKT mwaka 1990/1991 kombania A OC- Mohammed huyu afande alitembea karibu na mademu wote wa kombania A dada zetu walichezewa sana na hawa maafande nasikia JKT imerudi tena kama ningekuwa na mtoto wa kike nisingependa mtoto wangu aende JKT.
 
O'level - Airwing Sec. School ; Hapa kulikua na Afande Mwamasika, Afande Chacha, Afande Ndeki ... thanks mateso yote na nidhamu tulipata, fimbo, push-up, ukakamavu, kwata, kichurachura, kuchimba mashimo na kufukia, adhabu za kupanda ndege, kuita mvua na kunyonya mafuta ... mbona tulikoma!

A'level - Kigonsera High School; Hapa tulikua na wehu wa kutosha, Mwl.Ntandu, Second Master Mr.Mlasu, Head Master Mr.Shilimo ... Ugali, Maharage, Kuchunga ng'ombe, kilimo, Heartburn ndo usiseme. Usafr mwendo wa malori ama mandolina..

Uhuru Peak, Mt.Kilimanjaro - Hapa ndo wengi ntaacha, tulienda 30 kileleni tukafika 7 tu. In short, siku ya 3 ya safari hamna rangi tuliacha ona, mvua, theluji, baridi, uchovu na majaribu yote ya kuupima mwili na utu wa mtu i.e Higher Altitude Desease ... thx GOD at last nilishinda!

Nimatumaini yangu japo kuwa JKT ilinikosa lakini ningeiweza vilivo, na pengine ningekuwa na mengi zaidi yakuongea kama si kuwa jela kwa kumkata kichwa Afande ... teh teh
 
Ndugu zangu

Naenda kambi ya Mgambo Kabuku Tanga kwa mafunzo ya jeshi la Kujenga Taifa. Ninaomba waliopita kambi hii wanijulishe mambo ya ndani ya kambi hii, historia yake na mazingira yake. Nataka nione maisha ya jeshini haswa na kama itawezekana nifanye kazi ya kujitolea kufundisha shule ya kata ya jirani kama ipo.
 
Mkuu Zitto; I hope mafunzo ya JKT yalienda vizuri. Kuna habari zozote za kusisimua za kushare?
 
Last edited by a moderator:
Fellows!
Kitu kinachonikumbusha Jeshi ni afande mmoja alikuwa anaitwa afande Kashandago kambi ya Msange Tabora alikuwa bonge la ---- huyu jamaa lakini duh! Alikuwa anatuenyesha kweli huyu jamaa na alivyo tu alikuwa anac

hekesha. Good experience.
 
Mkuu Zitto; I hope mafunzo ya JKT yalienda vizuri. Kuna habari zozote za kusisimua za kushare?
inaonekana vijana wa siku hizi wanakula shushi kwasababu sijawasikia wakisimulia stori za kusisimua kama enzi zetu. hata wanaojiunga ktk majeshi yetu ya ulinzi na usalama,mafunzo yao yamekua laini sana na nidhamu imeshuka sana.
 
Last edited by a moderator:
inaonekana vijana wa siku hizi wanakula shushi kwasababu sijawasikia wakisimulia stori za kusisimua kama enzi zetu. hata wanaojiunga ktk majeshi yetu ya ulinzi na usalama,mafunzo yao yamekua laini sana na nidhamu imeshuka sana.

Ni kweli vijana wa sasa wanakula shushi.mimi nilikuwa oparation niaka 20 ya azimio la Arusha hapo oljoro.Hii moment ilikuwa moment nzuri si ya kusahau.Wakati huo,jeshi lilitujenga,kiakili,kikakamavu na uvumilivu.ilibidi mtu atumie akili ya ziada ili uweze kuishi maisha yote ya shida,ambayo yanakuwa mchana kutwa.usiku watu wanakwenda kuimba disco.baada ya disco.kunywa chai ya kununua kwa mama Asha.hukuti kijana wa wakati huo anachukuwa uamuzi wa kujiua anapopata shida kama ilivyo sasa.Vijana wa sasa hawana uvumilivu,wamekaa kidijitali zaidi.
 
Swala la JKT limekua compulsory kwa wale wote tunaosubiri nafasi za professionals za jeshi kwani ni lazima kwanza tu serve jkt for four months then ndio miezi sita ya officer cadet. Mimi naomba kwa wale ambao mmepitia huko (hususan walioapa juzi juzi) mtu habarishe nini cha ku expect huko, na since day 1 mlivowasili kambini ilikuaje etc. Hii itasaidia wengi kujiandaa psychologically and physically kwaajili ya mafunzo. Kwani huku mtaani speculations ni nyingi sana, wengine wanasema wiki sita za kwanza hamna kuvua mabuti wala kulala na rumours nyingine kama hizo hivyo kwa ambaye hatojali basi tungefurahi kama ata share na sisi hapa.

Regards,

Don Lucchese cc xir jyerphy
 
Back
Top Bottom