Je unakumbuka ulipokua shule ulikua na cheo gani? Na faida ya hicho cheo ni ipi?

Je unakumbuka ulipokua shule ulikua na cheo gani? Na faida ya hicho cheo ni ipi?

Nilikuwa academic prefect ambapo kwa shule yetu ilkua ni nafasi ya tatu uongozi wa wanafunzi.Imenisaidia kwanza kuvaa badge ya ACADEMIC prefect totozi ni kuzichukua tu😋😋 pia ilinipa mwanga kuandaa tathmini na ripoti mbalimbali🔨
 
Food prefect/ kiongozi wa chakula
1. Nilikuwa nakula kwa wakat
2. Nilikuwa nasave chakula cha usiku nikiamka kusoma
3. Nilipata mke kupitia cheo hicho na tuna watoto wawili
4. Kilinifanya nijifunze kidhungu maana nilihitajika kujieleza infront of mass
5. Nilipata marafiki wengi kupitia food

Hasara
1. Nilikuwa baada ya break time lazma nilale sababu ya uji
2. Nilichukiwa sana na wazembe wasiotaka kusomba maji au kuni kwenye zamu zao
3. Nilijiona mwalimu kunipelekea kuwa mnoko
 
Nakumbuka wakati nipo sekondari nilikuwa na cheo cha uwaziri mkuu wa ulinzi.

Basi ikawa nikichelewa nafika karibia na shule then najifanya nakamata wanaochelewa kumbe na mimi natafuta upenyo niende zangu,nilienjoy sana kile cheo aisee
ahaaa hongeraaaa lakini ulikua hushtukiwi
 
Nilikuwa academic prefect ambapo kwa shule yetu ilkua ni nafasi ya tatu uongozi wa wanafunzi.Imenisaidia kwanza kuvaa badge ya ACADEMIC prefect totozi ni kuzichukua tu😋😋 pia ilinipa mwanga kuandaa tathmini na ripoti mbalimbali🔨
apo ni good
 
Food prefect/ kiongozi wa chakula
1. Nilikuwa nakula kwa wakat
2. Nilikuwa nasave chakula cha usiku nikiamka kusoma
3. Nilipata mke kupitia cheo hicho na tuna watoto wawili
4. Kilinifanya nijifunze kidhungu maana nilihitajika kujieleza infront of mass
5. Nilipata marafiki wengi kupitia food

Hasara
1. Nilikuwa baada ya break time lazma nilale sababu ya uji
2. Nilichukiwa sana na wazembe wasiotaka kusomba maji au kuni kwenye zamu zao
3. Nilijiona mwalimu kunipelekea kuwa mnoko
hongeraaaa wengine waliitafuta chance ya msosi walikosa na kunung'unika
 
Primary nilikuwa monitor darasa la 3 kwa kuteuliwa. Huwezi amini nilikuwa nachapa wapiga kelele na nilikuwa naona ni sahihi kabisa. Kuna muda nilikuwa naamuru walale wakikosa la kusoma (shule ya vidumu na mifagio)

Darasa la 4 nikawa kiranja nikapelekesha wasumbufu vilevile. La 5 mwishoni nikawa HP

Form 1 nikawa monitor kwa vile nilisoma vizuri sana pre-form one na nilikuwa najua. Form 2 nikawa store keeper, ni kazi inataka uaminifu na record keeping, then nikawa environmental prefect. Form 3 HP

A Level kiongozi flani hivi badge ya rank ya mwisho. Chuo nachezea kamati ya uchaguzi. Kwanza uku wanapitishwa watu kabla ya kupiga kura. Mimi ni adui wa siasa

Dini nimeshika nafasi kadhaa na kuwa kaka wa madogo kibao, nina vyeti vya dini kuliko kwingine. Viongozi wengi wa dini wanafeli au huwa wanasoma Edu
 
'O' level sikuwa na cheo chochote ila Advance nilikua health prefect Kilinisaidia sana sababu nilikua mhusika pekee wa kusindikiza wagonjwa hospitali na shule ilikua ni boarding so ilikua haipiti wiki mimi niko mjini... napeleka mgonjwa hospitali afu naenda mjini kukata mitaa.
 
Nilichaguliwa umonitor na mwalimu wa darasa kwa sababu ya kufanya vizuri somo lake.

Noma ikaja nilikuwa ndo naongoza kwa kupiga kelele darasani, kwa hiyo nikawa na mimi najiandika kwenye majina baadhi ya siku.

Nikaondolewa.

Faida siikumbuki.

Hasara: watu wakigombana class monitor pia unachapwa eti hukuwaamua.
 
'O' level sikuwa na cheo chochote ila Advance nilikua health prefect Kilinisaidia sana sababu nilikua mhusika pekee wa kusindikiza wagonjwa hospitali na shule ilikua ni boarding so ilikua haipiti wiki mimi niko mjini... napeleka mgonjwa hospitali afu naenda mjini kukata mitaa.
Usinikumbushe mademu zetu tulikuwa tunapanga waumwe kisha sisi uboizini tunatoroka kwenda hospitali kuwaona.
 
mimi nlikuwa naongoza tu darasani na faida yake nadhani mnaijua nmekula sana mabaki ya vyakula vya walimu na kupewa vijisenti
 
Nilikuwa monitor na kusafisha ofisi ya mhasibu toka niwe sikuwahi lipia Karo zababu daftari za waliolipa kilikuwa humo kwenye ofisi ya mhasibu Sasa ulikuwa unapeleka slip ya benki unatikiwa mie nilikuwa najitick tu mpka namaliza Shule ada nilikuwa naitafuna kwa raha rim pepper naiba humo humo darasani nilikuwa nawaandika majina walikuwa wakijua kabsa nasema tu leo flan utacheza no 4 wakianza kusomwa wanajijua kabsa Olevel sikuwahi rudishwa home kwa adhabu yeyote
 
Back
Top Bottom