Je Unakunywa Juice za Mixed Fruits?...

Je Unakunywa Juice za Mixed Fruits?...

kuna siku walisema kila kitu kina faida huku duniani eti wanashangaa mtu anachinja kuku anamnyonyoa anatupa manyoya wakati hayo manyoya yana juice nzuri sana
ulishaona juice ya manyoya ya kuku mkuu?
za kuambiwa?????????

umenichekesha sana mkulu, dah1
 
Wapi Mzizimkavu, njoo maliza ugomvi hapa.

Mkuu hapa umeniacha njia panda. Mi mchana huwa napiga hii makitu pia kwa imani ya kuuweka mwili imara kupambana na Nyagi nitakayomimina jioni. Sasa kama ndio hivi tena..... hebu Madaktari Riwa, MziziMkavu, na TIMING mkuje pande hii mturudishie imani yetu kwenye matunda.

Hapa mpaka aje MziziMkavu ndo kitaeleweka vizuri

nshasikia kitu kama hii kwa docta fulani hivi....kuna ukweli ndani yake...tusubiri MziziMkavu ,Riwa na wengine wakuje kutupa lecture hapa....

Uric acid ni end product ya digestion ya protein, sasa kula muda mwingi vyakula vya protein kwa ujumla wake ndivyo vinavyo sababisha uwe na uric acid nyingi. Lakini matumizi ya alcohol, antipain like paracetamol are the most causative of hyperuricemia. Na most protein ni zile first class kama meat, beans etc. Kwa msaada Google HYPERURICEMIA utapata majibu achanani na waganga njaa hao. Na ndiyo maana magonjwa ya gout ni common kwa wanywa pombe na wale wanaokula sana red meat.
Mkuu.@​PakaJimmymimi ninakubaliana na aliyoyasema Mkuu.@Mupirocin Uric acid ni end product ya digestion ya protein kula muda mwingi vyakula vya protein kwa ujumla wake ndivyo vinavyo sababisha uwe na uric acid nyingi.Lakini Sio kula Matunda kwa wingi ndio kuna sababisha Uric acid nyingi hilo hata mimi

sikubaliani nalo Huyo Daktari alikuwa anatangaza Matangazo ya Biashara mimi Mwenyewe nikiamka asubuhi

lazima nile tunda moja la Aple na Tango moja na juisi ya karoti kila siku na sina Uric acid huo ni uongo wa hali

ya juu musiamini hiyo kitu ila ninatoa ushauri muwe munatumia Juisi za Matunda ya kutengeneza nyumbani

fresh Juice sio Juice za Maboksi tafadhalini. Musinunuwe Juice za Maboksi zina Madhara jamani someni hapa

TUJIHADHARI NA JUNK FOOD NA JUICE ZA KUTENGNEZWA VIWANDANI

Kitu usichokijua kuhusu ‘juisi ya boksi’

attachment.php

Juice Feki ya boksi


BILA shaka unapoingia dukani au supermarket kununua juisi ya box, huwa unaamini kuwa iliyoandikwa ‘100% Puer Juice’ huwa ni halisi na ndiyo bora. Kwa kukuongezea imani zaidi, watengenezaji wameweka na neno ‘No Sugar Added’ au ‘No preservatives’ (haikuongezwa sukari wala dawa)!

Kuanzia leo elewa kwamba hayo ni maneno ya kibiashara tu, ukweli hauko hivyo! Umewahi kujiuliza kwa nini maboksi yote ya juisi hiyo yawe na ladha moja tu. Sote tunajua kwamba, kama ni juisi ya machungwa kwa mfano, ukila machungwa matano, yote hayawezi kuwa na ladha moja!

Lakini kwa juisi za maboksi imewezekana kuwa na ladha moja kwa sababu za kikemia zinazofanywa kiwandani wakati wa kuhifadhi juisi hiyo ambayo huweza kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika. Hivyo siyo kweli kwamba unachokunywa ni asilimia 100 ‘pure’.

NINI KINACHOTOKEA?
Ni kweli kwamba ‘100% pure juice’ hutokana na matunda halisi kama vile machungwa, mananasi, embe, n.k, lakini mchakato wake wa kukamua, kuhifadhi na hatimaye kumfikishia mlaji ndiyo wenye dosari za kiafya.

Kinachofanyika baada ya tunda kukamuliwa ni kuhifadhi juisi yake kwenye matanki maalumu makubwa ya viwandani. Ili juisi hiyo iweze kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika, wanalazimika kuondoa hewa yake asilia ya oksijeni (mchakato unajulikana kitaalamu kama ‘deaeration’), kitendo ambacho huifanya juisi hiyo kupoteza ladha yake ya asili.

NINI HUFANYIKA KUREJESHA LADHA YA MATUNDA?
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Food Renegade’ wa nchini Marekani unaojishughulisha na masuala ya lishe na kuhimiza ulaji wa vyakula asilia, makampuni yanayozalisha juisi hukodisha makampuni yenye ujuzi wa kutengeneza ladha mbalimbali za matunda na manukato.

Makampuni hayo husimamia utengenezaji wa maboksi ya kuhifadhia juisi ambayo huwekwa ladha na harufu ya matunda husika. Inaelezwa zaidi kuwa makampuni hayo ndiyo yanayotengeneza pia manukato (perfumes) maarufu duniani, kama vile Dior na Calvin Klein.

Lakini cha kushangaza, virutubisho vinavyotumika kutengenezea ladha hiyo bandia haviorodheshwi kwenye boksi na wenyewe wanajitetea kwa kusema kuwa ladha hiyo haiwezi kuorodheshwa kama sehemu ya ‘ingredients’ kwa sababu hutengenezwa kutokana na tunda lenyewe, ingawa wataalamu wengine wanadai utengenezaji wake huhusisha kemikali zingine ambazo siyo za asili.

Mtaalamu mwingine kutoka Taasisi ya Sera ya Kilimo na Biashara nchini Marekani, Bi. Alissa Hamilton J. D (PhD), ameelezea kwa undani jinsi juisi ya machungwa inavyotengenezwa kiwandani. Undani huo umo kwenye kitabu chake cha; ‘Squeezed: What You Don’t Know About Orange Juice’. (Kitu usichokijua kuhusu juisi ya machungwa).

Katika kitabu hicho, mwanadada huyo anasema kuwa ni muhimu kila binadamu kujua kwa undani jinsi chakula chake kinavyoandaliwa, kwa sababu maelezo au lebo inayowekwa kwenye boksi, siyo tu haisemi ukweli, bali pia hailezi ukweli wote.

Anasema kwamba, kama kweli ‘pure orange juice’ tunayokunywa ilipatikana baada ya kukamuliwa chungwa peke yake na kuwekwa kwenye boksi, basi bila shaka ladha ingekuwa tofauti kati ya boksi moja na lingine, kwa sababu chungwa moja linatofautiana ladha na chungwa lingine. – mengine matamu, mengine makali.

Mbali na hilo, kila kampuni inayotengeneza juisi ya machungwa ina ladha yake. Juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Tropicana ina ladha tofauti na juisi ya machungwa inayotengenezwa na kampuni ya Ceres, sababu ya tofauti hiyo inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu.


 

Attachments

  • juice feki.jpg
    juice feki.jpg
    40.1 KB · Views: 1,251
Aidha, Hamilton anaendelea kueleza mchezo mchafu unaochezwa na watengeneza juisi viwandani kwamba ladha ya juisi hiyo ya machungwa hutofautiana pia kati ya nchi na nchi, kwani viwanda huweka aina ya ladha kwenye chungwa kulingana na vile ambavyo wanapenda watu wa eneo inakokwenda.

Juisi inayotengenezwa kwa ajili ya nchi za Amerika Kaskazini huwa na kiwango kikibuwa cha kirutubisho aina ya ‘ethyl butyrate', ambacho ni moja ya kemikali inayotumika sana kwenye utengenezaji wa manukato na ladha. Mbali ya kirutubisho hicho kuwa na uwezo wa kutengeneza aina mbalimbali za ladha za matunda, lakini pia hakina gharama (cheap).

HATUA GANI ZA KUCHUKUA SASA?
Kama makala haya yatakuwa yamekushitua na kukushangaza, jua hauko peke yako. Hata hivyo, lengo kubwa la makala haya ni kukufumbua macho ujue juisi unayokunywa siyo salama kiasi gani na uwe na uamuzi wa kuicha au kuendelea kuitumia kwa hiyari yako mwenyewe, lakini siyo kwa kudanganywa na maelezo ya uongo ya kibiashara yanayowekwa juu yake.

Kama ambavyo mwandishi wa kitabu hicho Bi. Hamilton anavyosema: "Lengo la kitabu changu siyo kukataza watu kunywa juisi, isipokuwa kuwafanya wakijue vizuri wanachokinywa. Watu wana haki ya kujua ni kwa kiasi gani utengenezaji wa juisi hivi sasa umekuwa wa kibiashara zaidi, hii itawafanya wawe na maamuzi sahihi kuhusu afya zao."

Ingawa ni vigumu sana kuepuka ‘kuingizwa mkenge', lakini unaweza kujiepusha na madhara ya kiafya yatokanayo na unywaji wa juisi hizi ‘feki' kwa kupendelea kunywa juisi uliyoitayarisha mwenywe nyumbani na kuacha kununua vyakula au vinywaji ‘ready made', hasa kwa vile ambavyo vinapatikana kwa wingi sokoni.

TAHADHARI
Kwa ujumla matunda na juisi zake zina virutubisho vingi muhimu kwa ustawi wa afya ya binadamu, lakini tahadhari inatolewa kwa wanaopenda kunywa kiasi kingi cha juisi za matunda, hasa juisi ya machungwa ambayo inaelezwa kuwa na sukari nyingi.

Kiasi cha glasi moja ya juisi ya machungwa ina wastani wa gramu 25 za ‘fructose', (sukari), kiwango ambacho ni cha mwisho kabisa anachotakiwa mtu kutumia kwa siku moja. Hii ina maana kama utakunywa zaidi ya glasi moja pamoja na vinywaji vingine vinavyotumia sukari, kama vile chai, tayari utakuwa umezidisha kiwango kinachopendekezwa kwa siku.

Iwapo utakuwa na tatizo la unene na unahitaji kupunguza uzito, ni vyema ukapunguza sana au ukajiepusha kabisa na uywaji wa juisi za matunda, kwa sababu kiwango cha sukari kilichomo ni zaidi ya wastani unaotakiwa.

Ili upate faida za virutubisho vinavyopatikana kwenye matunda, yakiwemo machungwa, unashauriwa kula matunda hayo kama yalivyo kuliko kukamua juisi na kutupa makapi yake. Inaelezwa kwamba sukari iliyomo kwenye chungwa inapoliwa pamoja na nyama zake (fibre), sukari hiyo huwa haina madhara kwani huweza kujichanganya kwenye mfumo wa damu bila kuleta athari zozote kwa mlaji.

Hivyo ushauri wa ujumla unatolewa kwamba pendelea zaidi kula matunda na mboga za majani kama zilivyo kuliko kunywa juisi zake. Kwa kufanya hivyo utajiepusha na uwezekano wa kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Iwapo utakunywa, basi kunywa nusu glasi au isizidi glasi moja kwa siku. Asanteni.

TENGENEZEENI JUICE MAJUMBANI MWENU MUSINUNUWE JUICE ZA MABOKSI ZINA MADHARA KWA BINADAMU.
 
Squeezed: What You Don’t Know About Orange Juice

by Alissa Hamilton
“Most know that Tropicana Pure Premium is not from concentrate. Few know what it is.” That’s what Toronto-based author Alissa Hamilton says in Squeezed, her examination of the evolution of Florida’s orange juice industry.

For anyone who has never given a thought to the origins of their second-favourite breakfast drink (after coffee), Squeezed may come as

an eye-opener. Beneath its “aura of golden goodness,” Hamilton argues, orange juice is a great big corporate sham: processed and re-processed, with flavours leached out and re-added, then
the final product is trucked off to a grocery store near you.


It wasn’t always like this, says Hamilton. Travelling from Toronto to Lakeland, Florida, she looks back on the good old days when freshly squeezed Florida orange juice was actually fresh and actually from Florida (the majority of the juice consumed today is concentrate from land-rich, environmentally lax Brazil).

During her research, Hamilton stumbles upon the transcripts of the FDA’s 1961 trial hearings, “Matter of Orange Juice and Orange Juice Products: Definitions and Standards of Identity.” Despite her legal enthusiasm (“The script read as if written for the theatre …

multiple subplots, lead characters”)
, differentiating pasteurized from concentrated from reconstituted orange juice is just as exciting as it sounds. With some exceptions – Can simple housewives understand food labels? Will they successfully follow directions to add water? – the explication drags.


Although the FDA foresaw a shift from small to big business, they couldn’t predict the power of advertising. Hamilton cuts to the present, when the word Tropicana has become synonymous with orange juice; “not from concentrate” has slyly replaced the more off-putting

term “pasteurized”; Tropicana has been bought by Pepsi, and its competitor, Minute Maid, is owned by Coke.

Hamilton’s analysis is interesting and her research thorough, but she skims over key industrial issues (migrant Mexican labour

populations, Florida’s growers selling out to condo developers)
and disregards the green movement toward local and organic foods. Moreover, Hamilton assumes that her readers, much like that 1960s housewife, have little knowledge or agency, despite the fact that most of them are likely health buffs already. Or, more succinctly, we already know there’s pulp in our juice.

Reviewed by Rosemary Counter (from the July 2009 issue)

Review of Squeezed: What You Don
 
Mimi mwezi wa nne mwaka huu nilipima uric acid 420micromole/L, nikapunguza kula first class protein nikawanakula beans fish kwa kiasi kidogo laikni muda mwingi nakula mboga za majani na juices na matunda as whole, matokeo yake nimepima two weeks ago uric acid ni 270. iko normal kabisa. na normal range kwa male 400, kwa female 360. Acheni kufuata waganga wa kienyeji kama mtu unashida please contact mzizimkavu au mupirocin kwa msaada ili usaidiwe.
 
kiruuu,kama ni hivyo nyumba yangu tunakufa wote,aarrrrgggghhhh
In case you die, RIP my friend!(source Preta)

fabinyo, kama umesoma vizuri uzi huu kuna wadau wanaicrash idea hii, kwa hiyo na wewe jitahidi ufanye utafiti kwa kupitia maandishi na matoleo ya wataalamu.
 
In case you die, RIP my friend!(source Preta)

fabinyo, kama umesoma vizuri uzi huu kuna wadau wanaicrash idea hii, kwa hiyo na wewe jitahidi ufanye utafiti kwa kupitia maandishi na matoleo ya wataalamu.

i wil let u know wen we r riping!pamoja nimekusoma
 
Yaani ninavyopenda ile juice ya mchanganyiko wa nanasi, embe na passion itakuwaje? Dah sawa wataalam, tumewasikia!!
 
Na wizara ha Afya imekaa kimya kulitolea ufafanuzi ili suala ingekuwa ARV fake faster na watu wangetimuliwa
Sasa mtoa mada fruit salad mpaka 5 star hotel huwa wanaserve ambako am sure wanakuwa na competent nutritionist kama sijakosea you mean nao wameingia choo cha kike?
 
Shukamoo Dr. Mzizi Mkavu, heshima tu hii kwa elimu nzuri mkuu wangu!! Juice is home made kwa hakika na huwa hata kwa mtu nisiyemwamini sipendi juice yake!!! Pia kwa matunda kula yalivyo ni tiba nzuri na kwa upande wangu naheshimu sana!!
 
Wakubwa,

Jana nilikuwa nasikiliza RFA kulikuwa na kipindi cha Afya, kuna jamaa wa dizaini kama ya Dr Ndodi, wanapima magonjwa kwa kutumia mashine inayoitwa Quantum ambayo ina uwezo wa kuainisha magonjwa mengi yanayomsumbua mtu, kwa kushika handle fulani kama 'mouse' inayoingia kwenye computer hiyo. Baada ya hapo wanauza dawa za aina ya vyakula ili kutibu magonjwa yaliyoonekana kwa mgonjwa.

Kilichonishitua ni kwamba walifika mahala wakawa wanataja vitu vinavyopelekea mtu kuwa na Uric acid nyingi mwilini, wakasema kuwa ulaji wa matunda mchanganyiko KWA MUDA MMOJA ni source kubwa na mbaya sana ya Uric acid!

Walisema wale wauzaji wa matunda wanaokata chungwa, embe, papai, pesheni, avocado, tango, ndizi etc, na kukuzia kwenye sahani waogope kama ukoma, maana wanakuletea sahani ya kifo.
Walieleza kuwa kinachotakiwa ni kula tunda la aina moja lililopo kwenye msimu, basi na si kula matunda mchanganyiko.

Najiuliza, kuna packed juice za mixed fruit, aidha huko majumbani tunablend na kunywa juice za kuchanganya matunda, je ndio tunajimaliza?

Hii dunia sasa ishakuwa tabu kila unachogusa unaambiwa hatari tena hatari mbaya, sasa sijui tule nini, yaani mpaka matunda mix now ni hatari mbaya eeeh, yaani tukiorodhoshesha hapa vitu tunavotumia kila siku ni hatari tupu.
 
Hivi mpaka vijoti vya bakhresa vinausika hapa???
Na hata zile zake kubwa???au juice za ulaya tu
 
Dawa ni kumkimbilia Mungu tu. Dunia hii si salama so kwa akil zako tu huwezi kuwa salama.
 
Back
Top Bottom