Godfrey- denis
Member
- Aug 26, 2022
- 64
- 124
Je, unalenga nini katika uwekezaji wako: Ongezeko la mtaji (Capital Gain) au Gawio (Dividends)?
Watu wengi huingia kwenye soko la hisa bila kuwa na malengo ya wazi. Lakini ukweli ni kwamba malengo yako ndiyo dira ya uwekezaji wako. Kabla hujaweka hela yako, jiulize: Nataka kupata faida kwa njia ipi?
Faida Kubwa Mbili Kwenye Soko la Hisa
■ Ongezeko la Mtaji (Capital Gain) – faida unayopata pale thamani ya hisa inapopanda na ukaamua kuuza kwa bei ya juu zaidi.
■ Gawio (Dividends) – faida unayopokea moja kwa moja kutoka kwenye kampuni pale wanapogawa sehemu ya faida kwa wanahisa.
Kwa hiyo, malengo yako ya uwekezaji yanaweza kuzunguka aidha kwenye:
■ Kutafuta gawio la uhakika,
■ Kutafuta ongezeko la mtaji, au
■ Kufurahia vyote viwili kwa pamoja.
Aina za Makampuni Kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam
Kwenye DSE kuna makampuni zaidi ya 20. Kila moja lina ubora na fursa zake.
Makampuni ya Gawio (Dividend Stocks)
■ Haya hutengeneza faida kubwa na za uhakika.
■ Mara nyingi hayana madeni makubwa.
■ Historia yake ya kulipa gawio ni ya kuaminika.
👉 Yanafaa kwa wawekezaji wanaotafuta mapato ya mara kwa mara.
Makampuni ya Ongezeko la Mtaji (Growth stocks).
■ Bei zake za sasa bado zipo chini ya thamani halisi (undervalued).
■ Yana nafasi kubwa ya kupanda bei kadri muda unavyokwenda.
👉 Yanafaa kwa wawekezaji wanaotaka faida kubwa baadaye.
Jinsi ya Kutambua Fursa
Kwa Gawio:
■ Angalia ripoti za kifedha: faida kubwa na madeni madogo = uwezo mzuri wa kulipa gawio.
■ Historia ya kampuni: je, imelipa gawio mara kwa mara?
Kwa Ongezeko la Mtaji:
Angalia viashiria vya thamani (Valuation Ratios):
■ P/E ratio (Price to Earnings)
■ P/B ratio (Price to Book Value)
》 Viashiria hivi vitakuonyesha kama hisa imeuzwa kwa bei nafuu kuliko thamani yake halisi.
Kumbuka
👉 Kila uwekezaji unahitaji mpango. Malengo yako ndiyo yatakuongoza: kampuni gani uwekeze, muda gani uingie sokoni, na muda gani utoke.
👉 Usifuate tu mkumbo wa watu; fuata malengo yako na tathmini zako.
■ For private session and consultation before investing in a Tanzanian Financial Markets:
》WhatsApp: 0763721523
》Normal Calls: 0617128810