Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Binafsi nimefurahishwa na historia yake kwa kweli JF NI zaidi ya shule.
 
Huwa mkali zaidi pale ambapo kuwa na jike
 
kuna movie moja ya bushmen "god must be crazy" yupo kuna sehemu aling'ang'ani buti la yule mzungu jamaa akaona isiwe kesi akakapa pombe kakalewa ni moja ya viumbe wabishi sana hapa duniani
Vipi ntampata wapi huyu nataka nimfuge
 
Mkuu umeacha tabia yake ya kukimbilia kungata kwenye korodani na uume wa mtu wa jinsia ya kiume anapohisi mtu huyo ni hatari kwake.
..................
 
 
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea

Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.

Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism

Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.

Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.

Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…