Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Nakumbuka kuna filamu moja kama sijakosea ni "the gods must be crazy" huyu mnyama aling'ata buti la jamaa mmoja...ikawa jamaa anatembea huku anamburuza huyu nyegere...baada ya unbali mrefu nyegere alichoka na kubebwa.
 
Huyu kama angepewa ukubwa hata wa mbwa tu,ingekuwa kazi.😀
Ila wivu wa aina hii kwa binadamu ni shida!!Mwanamke akikuwekea limbwata la hivi,ni shidaaaa!Unaweza jikuta unamtandika hata baba yake kwa wivu wa kukaa karibu na mwanae
 
Nyegere hampati Fisimaji (water oatter) kwa wivu wa kimapenzi

Spotted-necked_otter_1.jpg


cc fisimaji
Mkuu fisi maji ni tofauti kabisa yeye hana ukorofi na ubabe kama nyegere
Fisi maji ana nyege zilizopitiliza yaani hata akiguswa na jani kwenye dushe anapiss hapohapo.
Hiyo ndo sifa yake kuu
Ila nyegere ni habari nyingine.!
Kuna mwaka flani hivi wanajeshi watatu walijeruhiwa vibaya na nyegere polini wakiwa kwenye mazoezi.
 
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea.


Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.


Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara).

Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.


Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.


Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.


Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.
Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...


Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
 
Nakumbuka ishawahi kuletwa humu..anyaway asante kwa somo ingawa mmmh kuna exaggeration Sana..umetia sana chumvi
 
Nyegere ni mnyama mwenye wivu sana.Nahisi akimfuma mkewe na Nyegere mwenzie SIDHANI KAMA ATAWAACHA SALAMA..
 
Huwa nashindwa kumtofautisha huyu mnyama na yule anayejirinia asali. Ndiyo huyu huyu au ni tofauti?

Huyu nimemwona kwenye the God must be crazy alivyon'gata kitu cha jamaa bila kukiachia
 
Nimecheka sana eti anakung'ata kwenye dushe vp na kwa majike nayo yana wivu kama madume
 
Back
Top Bottom