Je, unasali na mwenza wako? Zijue faida za Mume na Mke kusali pamoja

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
JE UNASALI NA MWENZA WAKO PAMOJA?

FAIDA ZA MUME NA MKE KUSALI PAMOJA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kusali pàmoja kûna epusha migogoro isiyo na ulazima.

2. Kusali pàmoja kûnawapa Muda wa kutatua migogoro Yenu Kwa sababu hamwezi kumwomba Mungu mkiwa mnakinyongo.

3. Kusali pàmoja kunaileta familia pàmoja na kuwa na Ñguvu na imara

4. Kusali pàmoja kunaunganisha Nafsi na Roho zenu kuwa kitu Kimoja.

5. Kusali pàmoja humfanya Mungu atoe Baraka Bila kizuizi.

6. Kusali pàmoja kunawajenga Watoto kuwa na tàbia ya kumtegemea Mungu.

7. Kusali Pàmoja kûnawapa nafasi ya kupanga mipango Yenu na kuitimiza

8. Kusali pàmoja kunaifanya familia íwe Jeshi imara àmbalo linauwezo wa kuzuia mashambulizi ya maadui zenu íwe maadui ya kimwili au kiroho.

9. Kusali pàmoja kunaondoa ubinafsi miongoni mwenu.

10. Kama mnamuda wa kusali pàmoja ni ngumu familia kuanguka.

JINSI YA KUSALI PAMOJA:

1. Angalieni Ratiba ya Memba wôte wa familia Yenu Ikoje.

2. Pangeni Muda àmbao wahusika wôte watakuwepo.

3. Wekeni agenda za kîla wiki za kuombea.

4. Wekeni Mhusika wa kuomba Kwa kîla Siku au kîla wiki.

5. Wekeni Mtu wa Kutoa Somo Kulingana na Maombi Husika

MUDA WA MAOMBI

1. Angalau mara Mbili Kwa Siku Kwa familia nzima. Asûbuhi na Usiku.

2. Muda wa Maombi ukikaribia wahusika wôte wawe Safi. Waoge, ikiwezekana Pawe na vazi maalumu la kîla Mtu Kuvaa kwaajili ya Maombi. Vazi Hilo liwe Safi.

3. Sehemu ya kusali sharti iandaliwe na iwe Safi ñdipo Msali.

4. Maombi yasipungue nusu Saa na yasizidi Lisaa limoja.

5. Wahusika wôte wa familia ikiwemo Watoto wafundishwe kusali Kwa usahihi Kabisa.

6. Wahusika wôte wa familia ikiwemo Watoto wafundishwe kuwa na heshima na nidhamu Wakati wa Maombi.
Ikiwezekana adhabu ndogondogo zitolewe papohapo Kwa Watoto watukutu.

7. Mwanamke aliyekwenye hedhi asiruhusiwe kuendesha ibada.

8. Baba hata asipokuwepo RATIBA iendelee vilevile na Mama ahakikishe inafanyika

9. Mgeni yeyote asiruhusiwe kusali Wala kuchangia chochote Mpaka azoee utaratibu wa familia Yenu na awe Mtu wa Imani Yenu.

10. Pawe Muda wa Mzazi Hasa Baba Kutoa mawaidha, hotuba au somo kuhusu Dini na huku akihusianisha na Elimu Dunia ili kuwafanya Watoto WAELEWE. Hii inamaanisha Baba lazima awe mjuzi, mwenye Elimu zaidi kuliko yeyote ndàni ya familia. Kwa Watibeli Baba anatakiwa kuwa na ujuzi, ufahamu na Elimu ya Dini. Na kama Baba hakuwa na Elimu na maarifa Basi ayatafute hayo maarifa na ufahamu ili cheo cha Ubaba kimstahili.

9. Pawe na mûda wa Watoto kuuliza maswali kuhusu Somo, kuhusu Dini Yenu au desturi na Mila zenu, na maswali ya nyongeza.

10. Mtoto asidanganywe. Ikiwa Swali litakuwa tata au linahitaji maelezo yenye vielelezo Basi Mzazi atamwambia Mtoto kuwa Swali lake atalijibu Wakati Mwingine. Au swali lake ni nzuri lakini Umri wa Mtoto bado hajafikia kupewa jibu lake.

11. Baba akitoa Somo Baadaye Mama atachangia kidôgo kuelezea gap Ambazo Baba aliziacha íwe Kwa kusahau au Kwa namna yoyote. Vivyohivyo Mama akitoa Somo Baadaye Baba atajazia nyama sehemu alizoacha Mama.

12. Watoto Wapewe Nafasi ya kueleza walichojifunza Siku hiyo Kwa ufupi.

13. Uwèpo Siku àmbayo Watoto watapewa kwaajili ya kuandaa na Kutoa Somo ili kuwajengea msingi, uwezo na uzoefu na kujiamini kuongea mbele za Watu

14. Ziwepo programu ndàni ya Familia zitakazofanyika Kwa pàmoja mfano programme ya Muziki katika familia ya Tibeli. Siku hiyo kîla Memba ndàni ya familia apewe Uhusika wake. Waimbaji Wapewe uimbaji, wapiga Vyombo Wapewe ala za Muziki, waigizaji waandae onyesho linaloendana na Muziki. Kisha onyesho baàda ya kuliandaa vyakutosha mtatafuta jukwaa la kuwasilisha Kazi Yenu inaweza kuwasiku ya birthday ya Moja ya Memba, au family day àmbayo mtaalika family friends. Au kurusha kwèñye Mitandao kwani Siku hizi majukwaa ni mengi na mtakuwa live.

15. Pawe na Siku ya matendo ya huruma Kwa familia kwenda kwèñye jamii mathalani kusaidia Wengine. Kusafisha maeneo ya umma kama hospital, vituo vya Polisi, vituo vya Daladala.
Kutembelea wafungwa, n.k.

16. Watoto wafundishwe kujizuia ikiwemo kuwepo Siku ya kufunga.

Ngoja nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
JE UNASALI NA MWENZA WAKO PAMOJA?

FAIDA ZA MUME NA MKE KUSALI PAMOJA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Kusali pàmoja kûna epusha migogoro isiyo na ulazima.

2. Kusali pàmoja kûnawapa Muda wa kutatua migogoro Yenu Kwa sababu hamwezi kumwomba Mungu mkiwa mnakinyongo.

3. Kusali pàmoja kunaileta familia pàmoja na kuwa na Ñguvu na imara

4. Kusali pàmoja kunaunganisha Nafsi na Roho zenu kuwa kitu Kimoja.

5. Kusali pàmoja humfanya Mungu atoe Baraka Bila kizuizi.

6. Kusali pàmoja kunawajenga Watoto kuwa na tàbia ya kumtegemea Mungu.

7. Kusali Pàmoja kûnawapa nafasi ya kupanga mipango Yenu na kuitimiza

8. Kusali pàmoja kunaifanya familia íwe Jeshi imara àmbalo linauwezo wa kuzuia mashambulizi ya maadui zenu íwe maadui ya kimwili au kiroho.

9. Kusali pàmoja kunaondoa ubinafsi miongoni mwenu.

10. Kama mnamuda wa kusali pàmoja ni ngumu familia kuanguka.

JINSI YA KUSALI PAMOJA:

1. Angalieni Ratiba ya Memba wôte wa familia Yenu Ikoje.

2. Pangeni Muda àmbao wahusika wôte watakuwepo.

3. Wekeni agenda za kîla wiki za kuombea.

4. Wekeni Mhusika wa kuomba Kwa kîla Siku au kîla wiki.

5. Wekeni Mtu wa Kutoa Somo Kulingana na Maombi Husika

MUDA WA MAOMBI

1. Angalau mara Mbili Kwa Siku Kwa familia nzima. Asûbuhi na Usiku.

2. Muda wa Maombi ukikaribia wahusika wôte wawe Safi. Waoge, ikiwezekana Pawe na vazi maalumu la kîla Mtu Kuvaa kwaajili ya Maombi. Vazi Hilo liwe Safi.

3. Sehemu ya kusali sharti iandaliwe na iwe Safi ñdipo Msali.

4. Maombi yasipungue nusu Saa na yasizidi Lisaa limoja.

5. Wahusika wôte wa familia ikiwemo Watoto wafundishwe kusali Kwa usahihi Kabisa.

6. Wahusika wôte wa familia ikiwemo Watoto wafundishwe kuwa na heshima na nidhamu Wakati wa Maombi.
Ikiwezekana adhabu ndogondogo zitolewe papohapo Kwa Watoto watukutu.

7. Mwanamke aliyekwenye hedhi asiruhusiwe kuendesha ibada.

8. Baba hata asipokuwepo RATIBA iendelee vilevile na Mama ahakikishe inafanyika

9. Mgeni yeyote asiruhusiwe kusali Wala kuchangia chochote Mpaka azoee utaratibu wa familia Yenu na awe Mtu wa Imani Yenu.

10. Pawe Muda wa Mzazi Hasa Baba Kutoa mawaidha, hotuba au somo kuhusu Dini na huku akihusianisha na Elimu Dunia ili kuwafanya Watoto WAELEWE.
Hii inamaanisha Baba lazima awe mjuzi, mwenye Elimu zaidi kuliko yeyote ndàni ya familia.
Kwa Watibeli Baba anatakiwa kuwa na ujuzi, ufahamu na Elimu ya Dini.
Na kama Baba hakuwa na Elimu na maarifa Basi ayatafute hayo maarifa na ufahamu ili cheo cha Ubaba kimstahili.

9. Pawe na mûda wa Watoto kuuliza maswali kuhusu Somo, kuhusu Dini Yenu au desturi na Mila zenu, na maswali ya nyongeza.

10. Mtoto asidanganywe. Ikiwa Swali litakuwa tata au linahitaji maelezo yenye vielelezo Basi Mzazi atamwambia Mtoto kuwa Swali lake atalijibu Wakati Mwingine. Au swali lake ni nzuri lakini Umri wa Mtoto bado hajafikia kupewa jibu lake.

11. Baba akitoa Somo Baadaye Mama atachangia kidôgo kuelezea gap Ambazo Baba aliziacha íwe Kwa kusahau au Kwa namna yoyote. Vivyohivyo Mama akitoa Somo Baadaye Baba atajazia nyama sehemu alizoacha Mama.

12. Watoto Wapewe Nafasi ya kueleza walichojifunza Siku hiyo Kwa ufupi.

13. Uwèpo Siku àmbayo Watoto watapewa kwaajili ya kuandaa na Kutoa Somo ili kuwajengea msingi, uwezo na uzoefu na kujiamini kuongea mbele za Watu

14. Ziwepo programu ndàni ya Familia zitakazofanyika Kwa pàmoja mfano programme ya Muziki katika familia ya Tibeli.
Siku hiyo kîla Memba ndàni ya familia apewe Uhusika wake. Waimbaji Wapewe uimbaji, wapiga Vyombo Wapewe ala za Muziki, waigizaji waandae onyesho linaloendana na Muziki.
Kisha onyesho baàda ya kuliandaa vyakutosha mtatafuta jukwaa la kuwasilisha Kazi Yenu inaweza kuwasiku ya birthday ya Moja ya Memba, au family day àmbayo mtaalika family friends. Au kurusha kwèñye Mitandao kwani Siku hizi majukwaa ni mengi na mtakuwa live.

15. Pawe na Siku ya matendo ya huruma Kwa familia kwenda kwèñye jamii mathalani kusaidia Wengine. Kusafisha maeneo ya umma kama hospital, vituo vya Polisi, vituo vya Daladala.
Kutembelea wafungwa, n.k.

16. Watoto wafundishwe kujizuia ikiwemo kuwepo Siku ya kufunga.

Ngoja nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Kila mtu angelipenda hivo ila mwanamake akikuzoea anaanza visingizio vingi vya kukuepa kuswali kwa wakati nawewe.......iinawezakana ndoa ikiwa changa au mkizeeka sanaa nae.
 
7. Mwanamke aliyekwenye hedhi asiruhusiwe kuendesha ibada.
Umeandika mambo mazuri sana, ila nimeshangaa kuona jinsi ulivyo na fikra hii bado. Hedhi haimaanishi chochote kibaya isipokuwa kumaanisha msimu wa kupanda umefika, ni msimu wa kuendeleza uhai. Ni msimu wa baraka na mume na mke wakikaa pamoja msimu huu basi uhai mpya utachipuka. Damu ni uhai sio ufu. Hedhi ni majira ya masika na sio majira ya kiangazi. Hedhi ni kipindi cha baraka na sio kipindi cha laana!
 
Kila mtu angelipenda hivo ila mwanamake akikuzoea anaanza visingizio vingi vya kukuepa kuswali kwa wakati nawewe.......iinawezakana ndoa ikiwa changa au mkizeeka sanaa nae.

Mwanamke ni kama Mtoto ana-act vile unavyomfundisha na vile anavyokuona.

Mwanamke ni kama Mwezi na Mwanaume ni Jua.
Mwezi huakisi mwanga Kutoka kwèñye Jua.

Wanawake walivyo ndivyo walivyofundishwa na Wanaume au ndivyo wanavyowaona Wanaume.

Mwanaume ndiye Kiongozi wa Mwanamke.
Chochote afanyacho Mwanamke jua Kiongozi wake ni Mwanaume au amepewa ruhusa na Mwanaume
 
Yesu na Maria magdalena walisali pamoja pia, labda ndio maana hatujawahi kusikia mgogoro kwenye mahusiano yao
Unajua kwanini Yesu kwa miaka 33 tu alisepa juu na kumuacha bila hata taarifa, mahusiano sio simple hivo kama unavo dhani.
 
Umeandika mambo mazuri sana, ila nimeshangaa kuona jinsi ulivyo na fikra hii bado. Hedhi haimaanishi chochote kibaya isipokuwa kumaanisha msimu wa kupanda umefika, ni msimu wa kuendeleza uhai. Ni msimu wa baraka na mume na mke wakikaa pamoja msimu huu basi uhai mpya utachipuka. Damu ni uhai sio ufu. Hedhi ni majira ya masika na sio majira ya kiangazi. Hedhi ni kipindi cha baraka na sio kipindi cha laana!

Hedhi haina shida Kwa ishu zingine ila Kiroho hedhi siô damu kama ulivyosema.

Hedhi ni uchafu wa yai lililokufa àmbao halikurutubishwa.

Kwa Watu weñye Elimu ya kiroho wanajua hedhi ni nini, matumizi Yake na Wapi haitakiwi kûtumika.

Hedhi ni yai lililokufa, lililoharibika.
Haliwezi kuwa Safi tenà.

Mwanamke aliye kwèñye hedhi hatakiwi kushughulika na mambo ya kiroho hasa Roho watakatifu au mîungu mitakatifu

NI Sawasawa na usali ukiwa umejikojolea au umejinyea.
Hedhi ni waste products kama ilivyomkojo.
 
Unajua kwanini Yesu kwa miaka 33 tu alisepa juu na kumuacha bila hata taarifa, mahusiano sio simple hivo kama unavo dhani.
alimuacha vipi bila taarifa? kwani yesu alitakiwa aishi miaka mingapi?
 
Hedhi haina shida Kwa ishu zingine ila Kiroho hedhi siô damu kama ulivyosema.

Hedhi ni uchafu wa yai lililokufa àmbao halikurutubishwa.

Kwa Watu weñye Elimu ya kiroho wanajua hedhi ni nini, matumizi Yake na Wapi haitakiwi kûtumika.

Hedhi ni yai lililokufa, lililoharibika.
Haliwezi kuwa Safi tenà.

Mwanamke aliye kwèñye hedhi hatakiwi kushughulika na mambo ya kiroho hasa Roho watakatifu au mîungu mitakatifu

NI Sawasawa na usali ukiwa umejikojolea au umejinyea.
Hedhi ni waste products kama ilivyomkojo.
Ni sawa hiyo biologia yake ila imani inayoingizwa hapo ni ya kizamani na kwa watu wasio na uelewa mkubwa wa mambo. Ni kweli bleeding ni kitu kisichopendeza iwe ni mdomoni, puani au wapi. Hedhi ilikuwa changamoto zamani na hasa kwa wale ambao hawakuweza kujiweka katika hali ya usafi, inaleta tu kero kama vile mtu anshindwa kufuta kamasi analeta kero naye si vema akaongoza ibada. Ila kama anajisafisha hakuna shida yoyote. Jambo kubwa hapa ni usafi. Watu wote huenda chooni lakini hoja sio kwenda chooni, hoja ni kujiweka safi baada ya kwenda chooni. Mwanamke ajiweke safi wakati wa hedhi ndio jambo la msingi.
 
Usafi unaanzia rohoni mpaka mwilini.
 
Back
Top Bottom