Mzee Mukaruka
JF-Expert Member
- Jun 18, 2012
- 712
- 393
Heri ya Mwaka mpya na kwako Pia mkuu, Nakutakia mafaniko
Kwa Dar-es Salaammimi si mwenyeji sana hapo
ILA naamini Dar hapo Wapo kampuni ya Balton Tanzania, ukifika kwao ni vizuri ukapata vitu vya uhakika
Pia naamini kuna Kampuni maarufu kama Kibo Trading Ltd watakuwepo hapo...ila loacation exactly sijui mkuu, hawa Kibo Trading hupewa mizigo Genuine na supply wenyewe
Pia kwa kuwa naamini Dar mambo mengi yapo, kama utafanikiwa kupata duka la wahindi wanaitwa TRICHEM hapo pia utapata vitu bora sana maana hawa huwa wanapewa mizigo genuine na wale wasambazaji
Wadau ambao wamewahi kupata mizigo harisi kwa dar nadhani watakuja kuongezea mkuu
etc
Asante sana mkuu kwa majibu yako mazuri nitafuatilia.
Naomba vile vile kama kuna wadau wamewahi kununua MBOLEA au MADAWA ya mimea ya kuaminika jijini Dar wajitokeze.
Asante kwa msaada.
Habari kaka mimi Ni Mkulima ila cjawa mzoefu ndio kwanza nataka kuanza kutokana na darasa hili linalo endelea ...nitaanza na eneo Dogo tu la robo eka 1000m² ....nasari tayari nimeshataarisha ..kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mbegu nimeamua kutumia mbegu ya Tanya ...na nasari nilitaarisha tarehe 26/12/2015... Na tarajia January kupandikiza ...mbolea nitakayo tumia Ni ya samadi mavi ya mbuzi pamoja na ngombe ....sasa kidogo Nina swali ??KATIKA MBOLEA HAPO MIX KIDOGO NA DAP, AU NPK YA 17:17:17, AU MAP (MONO AMONNIUM PHOSPHATE). HIZO SAMADI NI NZURI KUIMPROVE SOIL STRUCTURE (AERATION-WATER &AIR) LAKINI ZINAFANYA KAZI SLOWLY SANA.
#Je mbegu niliotumia kwa kipindi hiki Ni sahihi???-KWA KUWA TUNAENDA MSIMU WA MVUA, TANYA NI NZURI PIA LAKINI HIYO NI OPV (HAIZAI SANAA KAMA HIZI HYBRID-F1) KAMA MONICA AU EDEN
#Ardhi yangu INA matatizo ya nematode japo c kwa kiwango kikubwa nini nifanye????- JITAHIDI UWEKE CHOKAAA MWEZI MMOJA KABLA YA KUPANDA SHAMBANI TUMIA CHOKAA YA RHINO TOKA TANGA, KWA EKA NI MIFUKO 8, UIVURUGE NA UDONGO KABLA YA KUPANDA, PIA TAFUTA DAWA (FUNGICIDES/INSECTICIDES) MOJA WAPO YA HIZI KAMA, FENOMEN 400 EC (FENAMIPHOS 40%) , AU NIMBECIDINE (FROM NEEM EXTRACT-MWAROBAINI) , AU AGRIFOSI, AU FURADAN 4F, AU AMISTAR XTRA SPRAY SHAMBANI KABLA YA KUPANDA, NA UTAKUWA UNARUDIA MOJA WAPO YA HIZO DAWA KILA BAADA YA SIKU 14
#then vp naweza kujikinga na wilt sababu wakulima wengi wanakilio hiki.., UKITUMIA CHOKAA, NA MOJA WAPO YA HIZO DAWA NILIZOKWAMBIA HAPO JUU, UTAKUWA SAFE NA WILT KWA 70%
Heshima kwako.
DAH KWELI MIMI NAFUATILIA UZI, JAMAA ANAJIBU SWALI MOJA HATA MARA 10 NA WALA HACHOKI, MOYO WA AJABU SANA HUUDah nimepitia siku tatu huu UZI toka mwanzo mpaka mwisho hapa page ya 14 kwa umakini kabisa. Aisee sijawahi kutana na UZI mtamu, wenye akili na unaokuelekeza direct hata kwa mkulima mdogo kabisa wa kule kijijini anaelewa. Mkuu kilimomaarifautajiri salute kuu kwa mkono juu mwingine umenyooka chini. Nimechukua notes nyingi sana kwa ajili ya msaada. Nikiwa na swali naliandika pembeni kwani nikiuliza itanipoteza ajabu nilivyozidi kusoma nikawa napata majibu na kujikuta nakata maswali.
Nililima nyanya riogrande mkulima tena kwa kuanza kwa mbwembwe sana pale kahe ekari 3. Shamba zilikuwa 2 moja ekari na robo nyingine mbili kasoro. Nililima kipindi cha January nikavuna March mwishoni. Dah jamaa walikuwa wanakuja shamba kuchuma kreti moja la 40Kg lile niliuza kwa mara ya kwanza 45,000. Mwishoni niliuza 20,000. Nilitumia milioni tano kasoro ikiwa ni jumla ya kila kitu, shamba, mashine mbili, mbegu, mbolea, Dawa, vitendea kazi na wafanyakazi. Pamoja nakupata bei nzuri nilivuna kama kreti 60 tu mfano jumla zilinipa 2.1m pekee. Nyanya zilitafunwa na mdudu ambaye Sasa nimemjua ni kanitangaze kwani namtangaza Sasa.
Nimepitia kwa nguvu sana na kwa akili kwani narudi tena kahe msimu huu. Nafreka shamba Sasa na nataka kuandaa kitalu. Aisee nataka nilime kisasa zaidi. Huwa nanunua mbegu pale Moshi, nimepita maduka kadhaa nimeona wana kipato. Japo natafuta Eden. Sasa swali langu tu hapa ni unanishauri pale kahe nipande ipi? Kipato inafanya vizuri au eden? Je Moshi duka gani linauza pembejeo za kilimo zilizo bora kama madawa, mbegu na kadhalika? Nakuuliza hivi kwani nimeona mahala umegusia kahe nikahisi unapaelewa vizuri.
Kwasasa napanda lile shamba la ekari mbili kasoro pekee baada ya kulipumzisha kwa Mwaka na miezi je kanitangaze bado atakuwa around?
Kuna sehemu umegusia kulima kwa kupandisha matuta kilimo kilicho bora kwa drip lines Sasa sikuelewa vizuri kwa umwagiliaji wa furrow niwekeje matuta? Nitamwagiliaje? Kipindi kilichopita nilitumia majaluba kama ya mpunga ila sikupenda kwani hata shamba halipendezi.
Asante sana mkuu kwani kiukweli nililima nikiwa sina ujuzi. La mwisho mkuu tupatie namba tukupe walau kifurushi kwa roho nyeupe kabisa. Umefanya kitu kikubwa hakina mfano wake.mtu anavyouliza unavyojibu Safi sana kaka, wala hujali kwamba ulishalijibu kabla.
Pamoja mkuu.
Asante mkuu ...nitajitahidi kufata ushauri wakkSHUKARNI SANA,
Asante mkuu ...nitajitahidi kufata ushauri wakk
Yah!! Darasa La NGUVU Mno Mkuu, Asante Kwa Elimu!! Hapa Ndio Nauona Umuhimu Wa Kuwa Na ARDHI Ya Kutosha!!!! ARDHI Ndio Mtaji Mkuu!!!!
DAH KWELI MIMI NAFUATILIA UZI, JAMAA ANAJIBU SWALI MOJA HATA MARA 10 NA WALA HACHOKI, MOYO WA AJABU SANA HUU
Asante sana sana, je mult k au polyfeed natakiwa kuweka vijiko vingapi kwenye maji ya lita 20 ninapotaka kupiga? Maana vipimo vya gramu vinanisumbua. Asante.Hiyo Fort Sulotaste sijawahi iona mkuu, ila kama ina namba hizo za kwanza itakuwa nzuri ila cheki zaidi wingi wa% za contents za Micro nutrients kama Zinc, Boron, Copper, Molybedium, Sulphur etc, check ziko nyingi kwa kiasi gani mkuu, difference kwa maana ya wingi wa Micro nutrients ndio utakao determine ubora wa hiyo booster. Booster nyingi zenye content kubwa ya Zinc na Boron hizo zinafaa zaidi kutumika kama Finisher booster, na zile zenye wingi wa Nitrogen na Phosphorus hizo zinafaa kutumika kama Starter Booster. Kama kila content imebalance ki % maana yake hiyo booster unaweza itumia kama Starter na pia kama Finisher booster wakati wa Maua na Matunda.