Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Hatuwezi kulima matikiti "ORGANICALLY"? Yaani kulima bila kutumia mbolea za viwandani? Kwani najua kuna wanunuzi wengine na wengipia hawapaendi mazao yanayotokana na hizi mbolea za viwandani. Naomba ushauri kwa msingihuo = wa kulima bila kutumia mbolea za viwandani. Natanguliza asante zangu.
 
@kilimomaarifa.tajiri na ndugu @NINA IMANI kuna kitu nadhani tunachamganya hapa!! Je unamwagilia masaa 24 maji kiasi gani??? milimiter ngapi za maji??? Je @NINA IMANI unatumia drip irrigation au????

NB: KAMA UNATUMIA FURROW IRRIGATION (UMWAGILIAJI KWA KUTUMIA MFEREJI) SIKUSHAURI UMWAGILIE KWA MFEREJI KWA MASAA 24!!!
 
mwanao akimaliza form 4 mzazi mnunulie simu au laptop awe anaperuzi jamii forums, kuna elimu ya kivitendo inayoendana mazingira ya kitanzania ya sasa hivi, hizi elimu za college na university pamoja na ajira ngumu naona kunampotezea muda mwanao.....anamaliza na miaka 25 alafu ndio anaanza maisha kutoka 0
 
Mkuu Kilimo.maarifa, asante sana kwa darasa suri.

Je, kwa Dar es salaam ni duka gani lenye kuuza mbolea za kuaminika (zisizo fake) ?

Happy New Year.
 
Heri ya Mwaka mpya na kwako Pia mkuu, Nakutakia mafaniko

Kwa Dar-es Salaammimi si mwenyeji sana hapo

ILA naamini Dar hapo Wapo kampuni ya Balton Tanzania, ukifika kwao ni vizuri ukapata vitu vya uhakika

Pia naamini kuna Kampuni maarufu kama Kibo Trading Ltd watakuwepo hapo...ila loacation exactly sijui mkuu, hawa Kibo Trading hupewa mizigo Genuine na supply wenyewe

Pia kwa kuwa naamini Dar mambo mengi yapo, kama utafanikiwa kupata duka la wahindi wanaitwa TRICHEM hapo pia utapata vitu bora sana maana hawa huwa wanapewa mizigo genuine na wale wasambazaji

Wadau ambao wamewahi kupata mizigo harisi kwa dar nadhani watakuja kuongezea mkuu

etc

Asante sana mkuu kwa majibu yako mazuri nitafuatilia.

Naomba vile vile kama kuna wadau wamewahi kununua MBOLEA au MADAWA ya mimea ya kuaminika jijini Dar wajitokeze.

Asante kwa msaada.
 
Habari kaka mimi Ni Mkulima ila cjawa mzoefu ndio kwanza nataka kuanza kutokana na darasa hili linalo endelea ...nitaanza na eneo Dogo tu la robo eka 1000m² ....nasari tayari nimeshataarisha ..kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mbegu nimeamua kutumia mbegu ya Tanya ...na nasari nilitaarisha tarehe 26/12/2015... Na tarajia January kupandikiza ...mbolea nitakayo tumia Ni ya samadi mavi ya mbuzi pamoja na ngombe ....sasa kidogo Nina swali ??
#Je mbegu niliotumia kwa kipindi hiki Ni sahihi???
#Ardhi yangu INA matatizo ya nematode japo c kwa kiwango kikubwa nini nifanye????
#then vp naweza kujikinga na wilt sababu wakulima wengi wanakilio hiki..
Heshima kwako.
 
Heri ya mwaka mpya kilimomaarifa.tajiri...hali ya Nyanya zangu imezidi kuwa worse zile nilizokuwa nimeanza kuchuma zimezidi kukauka kilichobaki Ni kung'oa na kuchoma Kama ulivyosuggest. Zile ndogo naona kwa mbaali vimajani vinaanza kuwa brown ingawa nilizipiga dawa ya wadudu na ukungu toka ziko kitaluni na nikarudia tena baada ya kuhamisha!
 
Habari kaka mimi Ni Mkulima ila cjawa mzoefu ndio kwanza nataka kuanza kutokana na darasa hili linalo endelea ...nitaanza na eneo Dogo tu la robo eka 1000m² ....nasari tayari nimeshataarisha ..kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mbegu nimeamua kutumia mbegu ya Tanya ...na nasari nilitaarisha tarehe 26/12/2015... Na tarajia January kupandikiza ...mbolea nitakayo tumia Ni ya samadi mavi ya mbuzi pamoja na ngombe ....sasa kidogo Nina swali ??KATIKA MBOLEA HAPO MIX KIDOGO NA DAP, AU NPK YA 17:17:17, AU MAP (MONO AMONNIUM PHOSPHATE). HIZO SAMADI NI NZURI KUIMPROVE SOIL STRUCTURE (AERATION-WATER &AIR) LAKINI ZINAFANYA KAZI SLOWLY SANA.
#Je mbegu niliotumia kwa kipindi hiki Ni sahihi???-KWA KUWA TUNAENDA MSIMU WA MVUA, TANYA NI NZURI PIA LAKINI HIYO NI OPV (HAIZAI SANAA KAMA HIZI HYBRID-F1) KAMA MONICA AU EDEN
#Ardhi yangu INA matatizo ya nematode japo c kwa kiwango kikubwa nini nifanye????- JITAHIDI UWEKE CHOKAAA MWEZI MMOJA KABLA YA KUPANDA SHAMBANI TUMIA CHOKAA YA RHINO TOKA TANGA, KWA EKA NI MIFUKO 8, UIVURUGE NA UDONGO KABLA YA KUPANDA, PIA TAFUTA DAWA (FUNGICIDES/INSECTICIDES) MOJA WAPO YA HIZI KAMA, FENOMEN 400 EC (FENAMIPHOS 40%) , AU NIMBECIDINE (FROM NEEM EXTRACT-MWAROBAINI) , AU AGRIFOSI, AU FURADAN 4F, AU AMISTAR XTRA SPRAY SHAMBANI KABLA YA KUPANDA, NA UTAKUWA UNARUDIA MOJA WAPO YA HIZO DAWA KILA BAADA YA SIKU 14
#then vp naweza kujikinga na wilt sababu wakulima wengi wanakilio hiki.., UKITUMIA CHOKAA, NA MOJA WAPO YA HIZO DAWA NILIZOKWAMBIA HAPO JUU, UTAKUWA SAFE NA WILT KWA 70%
Heshima kwako.

SHUKARNI SANA,
 
NAOMBA KUULIZA,JE FORT SULOTASTE 19-19-19+Mg0 na Mult K 19-19-19 zinafanya kazi sawa kwenye nyanya, au ipi yenye ubora zaidi. Asante.
 
Asante Sana kilimomaarifa.tajiri kwa kweli umepatia Sana utakuwa Ni mnyauko maana ulienda kwa viportion Tu na Nyanya zimekauka zikiwa na matunda take mengi! Hizi ndogo vimajani vinaanza kuwa brown ya rangi ya udongo Si kijani, ujue hats hizi zilizokauka zilianza kwa style hii! Chokaa kupata ndio changamoto sasa duh!
 
Dah nimepitia siku tatu huu UZI toka mwanzo mpaka mwisho hapa page ya 14 kwa umakini kabisa. Aisee sijawahi kutana na UZI mtamu, wenye akili na unaokuelekeza direct hata kwa mkulima mdogo kabisa wa kule kijijini anaelewa. Mkuu kilimomaarifautajiri salute kuu kwa mkono juu mwingine umenyooka chini. Nimechukua notes nyingi sana kwa ajili ya msaada. Nikiwa na swali naliandika pembeni kwani nikiuliza itanipoteza ajabu nilivyozidi kusoma nikawa napata majibu na kujikuta nakata maswali.
Nililima nyanya riogrande mkulima tena kwa kuanza kwa mbwembwe sana pale kahe ekari 3. Shamba zilikuwa 2 moja ekari na robo nyingine mbili kasoro. Nililima kipindi cha January nikavuna March mwishoni. Dah jamaa walikuwa wanakuja shamba kuchuma kreti moja la 40Kg lile niliuza kwa mara ya kwanza 45,000. Mwishoni niliuza 20,000. Nilitumia milioni tano kasoro ikiwa ni jumla ya kila kitu, shamba, mashine mbili, mbegu, mbolea, Dawa, vitendea kazi na wafanyakazi. Pamoja nakupata bei nzuri nilivuna kama kreti 60 tu mfano jumla zilinipa 2.1m pekee. Nyanya zilitafunwa na mdudu ambaye Sasa nimemjua ni kanitangaze kwani namtangaza Sasa.
Nimepitia kwa nguvu sana na kwa akili kwani narudi tena kahe msimu huu. Nafreka shamba Sasa na nataka kuandaa kitalu. Aisee nataka nilime kisasa zaidi. Huwa nanunua mbegu pale Moshi, nimepita maduka kadhaa nimeona wana kipato. Japo natafuta Eden. Sasa swali langu tu hapa ni unanishauri pale kahe nipande ipi? Kipato inafanya vizuri au eden? Je Moshi duka gani linauza pembejeo za kilimo zilizo bora kama madawa, mbegu na kadhalika? Nakuuliza hivi kwani nimeona mahala umegusia kahe nikahisi unapaelewa vizuri.
Kwasasa napanda lile shamba la ekari mbili kasoro pekee baada ya kulipumzisha kwa Mwaka na miezi je kanitangaze bado atakuwa around?
Kuna sehemu umegusia kulima kwa kupandisha matuta kilimo kilicho bora kwa drip lines Sasa sikuelewa vizuri kwa umwagiliaji wa furrow niwekeje matuta? Nitamwagiliaje? Kipindi kilichopita nilitumia majaluba kama ya mpunga ila sikupenda kwani hata shamba halipendezi.
Asante sana mkuu kwani kiukweli nililima nikiwa sina ujuzi. La mwisho mkuu tupatie namba tukupe walau kifurushi kwa roho nyeupe kabisa. Umefanya kitu kikubwa hakina mfano wake.mtu anavyouliza unavyojibu Safi sana kaka, wala hujali kwamba ulishalijibu kabla.
Pamoja mkuu.
DAH KWELI MIMI NAFUATILIA UZI, JAMAA ANAJIBU SWALI MOJA HATA MARA 10 NA WALA HACHOKI, MOYO WA AJABU SANA HUU
 
Yah!! Darasa La NGUVU Mno Mkuu, Asante Kwa Elimu!! Hapa Ndio Nauona Umuhimu Wa Kuwa Na ARDHI Ya Kutosha!!!! ARDHI Ndio Mtaji Mkuu!!!!
 
Mkuu nakushukuru sana. Sasa nimeenda KIBO Moshi kutafuta Yara miller winner imewaishia. Ila nimekuta wana NPK CEREAL 23-10-5+35 2MGO+0.3ZN ambayo wameshauri ni nzuri pia. Nataka kuotesha naweza uteshea hii then baadae winner ikija niendelee nayo mkuu?
 
Hiyo Fort Sulotaste sijawahi iona mkuu, ila kama ina namba hizo za kwanza itakuwa nzuri ila cheki zaidi wingi wa% za contents za Micro nutrients kama Zinc, Boron, Copper, Molybedium, Sulphur etc, check ziko nyingi kwa kiasi gani mkuu, difference kwa maana ya wingi wa Micro nutrients ndio utakao determine ubora wa hiyo booster. Booster nyingi zenye content kubwa ya Zinc na Boron hizo zinafaa zaidi kutumika kama Finisher booster, na zile zenye wingi wa Nitrogen na Phosphorus hizo zinafaa kutumika kama Starter Booster. Kama kila content imebalance ki % maana yake hiyo booster unaweza itumia kama Starter na pia kama Finisher booster wakati wa Maua na Matunda.
Asante sana sana, je mult k au polyfeed natakiwa kuweka vijiko vingapi kwenye maji ya lita 20 ninapotaka kupiga? Maana vipimo vya gramu vinanisumbua. Asante.
 
shukrani kwa elimu unayoitoa mkuu, nimefuatilia na kuchukua notice uzi mzima,
mimi nataka kuanza kulima mwezi wa 5,nikipiga hesabu zitakua zina matunda kuanzia mwezi wa 8 hadi wa 10,

kwanza ningependa kujua changamoto za soko kwa sisi tunaoanza zikoje na unawezaje kuziepuka kwa kua wewe una experiece sana soko unalielewa

pili umesema nyanya tokea ipandwe inachukua miezi 3-5 kuanza kuvunwa, je hili gepu la muda wa miezi miwili linatokana na nini? ni msimu, utunzaji au aina ya mbegu? shukrani
 
Back
Top Bottom