1. Safisha (Clear eneo) unalohitaji kuweka kitalu,lisiwe sehemu ya mteremko, au sehemu inayotuamisha maji, isiwe chini ya mti wa mkaratusi (na jamii zake)
2. ondoa magugu yoyote, na uyachome moto, pia ondoa masalia ya mazao ya msimu uliopita yazike na ufukie shimo hilo au yachome moto (off season crops-mazao ya msimu uliopita/mabaki Ni chanzo cha magonjwa na wadudu)
3. Tengeneza matuta (juu yawe levo-tambalale), urefu kuja juu sm 20, na upana wa mita 2, urefu wa hilo tuta ni ule utakaoweza kuhimili/kumudu kuhudumia kitalu
4. Tumia leki kulevo hayo matuta
5. Tafuta nyasi kavu, au mabua ya mahindi weka juu ya matuta yatandaze kisha yachome moto (LOCAL SOIL STERILIZATION METHOD)-njia ya kuua vimela vya magonjwa na wadudu. Ukishindwa hiyo njia tumia njia ya kemikali nyunyiza dawa kama fungurani au Agrifos400 kuua vimelea vya magonjwa
6. Tumia ubao au fimbo kuchora vimifereji(Furrows) across urefu wa tuta kama tuta limekaa kaskazini kusini, basi mistari iwe mashariki to magharibi etc and vicervicersa. Umbali wa mfereji mmoja hadi mwingine uwe kati ya sm 5-10
7. Tumia dawa ya kupandia mbegu (DAWA inayazuia mbegu kuliwa na wadudu, na dumping off-KUKATIKA KIUONO KWA MICHE MICHANGA) mfano Apron Star ya Syngenta mix na mbegu zako, changanya na mchanga kidogo,kisha weka katika chupa ya plastic ya maji ya kunywa mfano ya lita moja/1/2 lita, mbele katika mfuniko wa chupa, toboa vitobo vidogo vidogo, kisha chukua hiyo chupa SASA TEMBEA TARATIBU UKIITIKISA hiyo chupa taratibu ukihakikisha zile mbegu zinamwagika kwa kiasi na kwa nafasi katika zile furrow (VIJIMIFEREJI ulivyochora). FANYA hivyo kwa matuta yote KISHA fukia na layer laini ya udongo.
8.Ukimaliza tafuta nyasi kavu (MULCH) MATANDAZWA, weka juu yake kisha mwagia maji mengi mpaka uone yanatokeza pembeni mwa tuta kiasi.
9. Endela kumwagia Matuta hayoo kila siku asubuhi na jioni kutegemeana na hali ya hewa, ndani ya siku 7 mbegu zako zitaota
10. Endelea na menejiment za kawaida, wadudu, magugu, magonjwa
11. Miche itakaa kitaluni siku 21 kisha utaipeleka shambani.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx