Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

miembe ya kisasa nini?
Sio ya kisasa tu. Kama herbicides hazipo selective kwa zao lako na ukatumia non selective obvious it will kill each and everything. Kama ni selective kwa miembe [emoji106] [emoji106] [emoji106]. Otherwise nakushauri upalilie tu.
 
Sio ya kisasa tu. Kama herbicides hazipo selective kwa zao lako na ukatumia non selective obvious it will kill each and everything. Kama ni selective kwa miembe [emoji106] [emoji106] [emoji106]. Otherwise nakushauri upalilie tu.

Asante mkuu kwa ushauri wako.
 
Mkuu Habari Naomba Maelekezo Ya Namna Njia Na Taratibu Za Kuandaa Kitalu Cha Nyanya Ile Nipate Miche Bora Na Iote Kwa Ufanisi Mkubwa.
 
kilimomaarifa.tajiri
Heko sana kiongozi
Hii shule unayotoa daah binafsi nakuelewa sana
Mungu abariki kazi za mikono yako.


1. Safisha (Clear eneo) unalohitaji kuweka kitalu,lisiwe sehemu ya mteremko, au sehemu inayotuamisha maji, isiwe chini ya mti wa mkaratusi (na jamii zake)

2. ondoa magugu yoyote, na uyachome moto, pia ondoa masalia ya mazao ya msimu uliopita yazike na ufukie shimo hilo au yachome moto (off season crops-mazao ya msimu uliopita/mabaki Ni chanzo cha magonjwa na wadudu)

3. Tengeneza matuta (juu yawe levo-tambalale), urefu kuja juu sm 20, na upana wa mita 2, urefu wa hilo tuta ni ule utakaoweza kuhimili/kumudu kuhudumia kitalu

4. Tumia leki kulevo hayo matuta

5. Tafuta nyasi kavu, au mabua ya mahindi weka juu ya matuta yatandaze kisha yachome moto (LOCAL SOIL STERILIZATION METHOD)-njia ya kuua vimela vya magonjwa na wadudu. Ukishindwa hiyo njia tumia njia ya kemikali nyunyiza dawa kama fungurani au Agrifos400 kuua vimelea vya magonjwa

6. Tumia ubao au fimbo kuchora vimifereji(Furrows) across urefu wa tuta kama tuta limekaa kaskazini kusini, basi mistari iwe mashariki to magharibi etc and vicervicersa. Umbali wa mfereji mmoja hadi mwingine uwe kati ya sm 5-10

7. Tumia dawa ya kupandia mbegu (DAWA inayazuia mbegu kuliwa na wadudu, na dumping off-KUKATIKA KIUONO KWA MICHE MICHANGA) mfano Apron Star ya Syngenta mix na mbegu zako, changanya na mchanga kidogo,kisha weka katika chupa ya plastic ya maji ya kunywa mfano ya lita moja/1/2 lita, mbele katika mfuniko wa chupa, toboa vitobo vidogo vidogo, kisha chukua hiyo chupa SASA TEMBEA TARATIBU UKIITIKISA hiyo chupa taratibu ukihakikisha zile mbegu zinamwagika kwa kiasi na kwa nafasi katika zile furrow (VIJIMIFEREJI ulivyochora). FANYA hivyo kwa matuta yote KISHA fukia na layer laini ya udongo.

8.Ukimaliza tafuta nyasi kavu (MULCH) MATANDAZWA, weka juu yake kisha mwagia maji mengi mpaka uone yanatokeza pembeni mwa tuta kiasi.

9. Endela kumwagia Matuta hayoo kila siku asubuhi na jioni kutegemeana na hali ya hewa, ndani ya siku 7 mbegu zako zitaota

10. Endelea na menejiment za kawaida, wadudu, magugu, magonjwa

11. Miche itakaa kitaluni siku 21 kisha utaipeleka shambani.


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
 
Mkuu Habari,pole Na Ahsante Kwa Elimu Unayotupatia.Naomba Kujua:nimeambiwa Na Wauzaji(East West Seed) Kuwa Kipato F1 inatakiwa kupandwa sm 75 kwa 75 na victory f1 1m kwa 1m sasa naomba kujua athari za kupunguza yaan kwa mfano kipato f1 nikafanya sm50 na victory sm75? na je kuanzia siku yangu kitalu cha nyanya naweza puliza dawa za ukungu na ile ya kuzuia ugonjwa wa kiuno?
 
NAOMBA KUULIZA,MWAKA HUU VIAZI VIMEUNGUA SANA NA UKUNGU SHAURI YA MVUA NYINGI, SASA KILA MKULIMA ANASEMA LAKE,WANASEMA IVORY M 72 WP NI BORA ZAIDI KULIKO RIDOMIL GOLD,WENGINE WANASEMA SUPER RIDO NDIO BORA ZAIDI,NAOMBA UTUSAIDIE MTAALAMU KWA MVUA HIZI ZINAZOENDELEA KUNYESHA DAWA IPI INGEFAA ZAIDI. ASANTE
 
ASANTE SANA,NYANYA ZANGU HAZIJAUNGUA NA UKUNGU HUWA NAPIGA RIDOMIL GOLD ,NA ZINACHANUA ,JE NAWEZA KUENDELEA KUPIGA RIDOMIL GOLD PEKEE
 
KWA KWELI KWA NYANYA NA HOHO SINA TAARIFA NA KIUA GUGU CHA SELECTIVE POST IMERGENCY,

ISIPOKUWA LABDA KWA KITUNGUU KIPO OXYFEN/SULFEN, NA SASA ADAMA (AGIL), KWA MAHINDI IPO PRIMAGRAM GOLD 660 SC HII ITUMIKE MAHINDI YAKIWA NA MAJANI MAWILI... KUWE NA UNYEVU WA KUTOSHA WAKATI UNAPOITUMIA, SELECTIVE POST EMERGENCY HERBICIDES NYINGINE JINA LIMENITOKA ILA IPO KWA MAZAO JAMII YA MAHARAGE NA KUNDE
Basi niweke sawa kwa ku list mfano
1. Mahindi- so and so(kiua gugu) - dosage

Asante mkuu
 
HIZI NDIO BAADHI YA DETAILS NILIZONAZO

1.KIUA GUGU-PRIMAGRAM GOLD 660 SC-ZAO MAHINDI, KIPIMO MLS 300 ZA DAWA KWA MAJI LITA 20

2. KIUA GUGU-OXYFEN/SULFEN-ZAO-KITUNGUU. KIPIMO, MLS 40 ZA DAWA KWA MAJI LITA 20 (ILA KATIKA KIBANDIKO WAMEANDIKA DAWA MLS 80 KWA MAJI LITA 20, ILA UKIFANYA KW AHICHO KIPIMO VITUNGUU VINAATHIRIKA

3. KIUA GUGU-ADAM (AGIL) MAZAO-KAROTI, KITUNGUU, VIAZI MVIRINGO ETC, KIPIMO CHA DAWA MLS 100 KWA MAJI LITA 20
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom