NINA IMANI
Senior Member
- Jan 8, 2014
- 113
- 16
nina imani
karibu sana kiongozi
nitajitahidi kujibu maswali yako
asante sana kiongozi
na karibu tena.
Mkuu Habari,naomba Kujua Eti Ni Kweli Kwamba Nyanya Inavyoanza Kuzaa Matunda Katika Matunda Ya Mwanzo Unatakiwa Utoe Tunda Moja La Kwanza Kabisa-MKUU HII SI KAWAIDA KUFANYIKA KATIKA NYANYA, BALI HUFANYIKA SANA KAKA PILIPILI HOHO (CAPSICUM- SWEET PEPPER)? Sababu Nimeambiwa Hilo Tunda Linakula Sana Mbolea Na Maji Mengi-KWA PILIPILI HOHO, HILO TUNDA LA KWANZA-King fruit KUONDELEWA ILI KURUHUSU MMEA KUTOA MAUA NA MATUNDA MENGI YENYE AFYA NJEMA (UBORA) NI KAMA PRUNNING VILE-Upogoleaji, HII HUFANYIKA ILI KUUPA MMEA STRESS ILI UZAE ZAIDI. Hivyo Ukilitoa Hilo Matunda Mengine Yanakuwa Makubwa Na Shape Nzuri,naomba Kujuzwa Hilo.
Tatemahunda
Kama umekosa Yara Nitrabor tafuta CAN, naamini hii utaipata, ila siku ya kuweka CAN , hakikisha shamba limelowana maji (Mwagia kwanza maji) then ndio uweke CAN-Usiweke mbolea shamba likiwa KAME, LAKINI usije kuichanga CAN na mbolea nyingine siku hiyo unapoweka, CAN iwekwe ikiwa pekeyake.
Tatemahunda
Nakushukuru sana kiongozi
Kuhusu nyanya ya Iringa hiyo miezi sina hakika sana ila nachojua ni kuwa kuanzia mwezi wa nne na kuendelea mpaka wa 8 hapo bei ya nyanya na mazo mengi ya matunda bei zinashuka kidogo maana wengi wanatumia maji ya mito na madimbwi kuzalisha, na mazao yakuwa mengi hivyo bei huwa chini (demand and supply). Sababu hasa ni kwamba kuanzia mwezi wa 4 sehemu nyingi za nchi masika inakuwa inaelekea ukingoni hivyo wengi wanalima sana mbonga mbonga na matunda, wengi wanaogopa kulima mboga mboga namtunda wakati wa masika (December-March) maana changamoto ni nyingi sana, hasa magonjwa ya ukungu/barafu, wadudu na mafuriko pia.LAKINI HAYA MAZAO YA HORTICULTURE UKIWEZA KULIZALISHA KIPINDI CHA MASIKA (DEC-MARCH) BEI YAKE HUWA NZURI SANA, MAANA SUPPLY INAKUWA KIDOGO, WAKATI DEMAND IKO CONSTANT/JUU ZAIDI.
Nakushauri ingia shambani December mkuu, ila jipange sana uwe na dawa za Ukungu na za wadudu za kutosha, tengenza mifereji ya kuzuia na kupitisha maji ya mvua, pia hakikisha maji hayatuami shambani.
Nakutakia mafanikio mkuu.
Ahsante sana mkuu, nimeelimika sana, najua tupo wengi tuliopata elim hii, hata hivyo niko kwenye maandalizi nianze kuingia shamba kati ya December na January ili nisikutane na nyanya ya iringa mana naskia wale huanza kuvuna mwishoni mwa April(although I'm not sure), pia naskia nyanya yao ikianza zao la nyanya hua linashuka thamani sana..naamin ajaliapo Muumba nitaleta mrejesho humu ili wengi zaidi wafaidike...
Samahamani naomba kuuliza tena, mbolea aina ya yara miller winner na npk zina ubora/utendaji sawa? Asante.