Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Mkuu Hizi Nyanya Kipato F1 Nitachuma Kila Baada Ya Wiki Moja Ndio Nauliza Naweza Chuma Hivyo Kwa Muda Gani Ni Kweli Inaweza Fika Miezi 6? Au Wewe Ulivyosema Michumo 3-5 Umemahanisha Miezi 3 Hadi 5? Naulizia Kuanzia Siku Ya Kwanza Kuchuma
 
Mkuu Ahsante Nimepiga Finisher Leo Maana Matunda Yanakaribia Kukomaa,na Nyanya Zina Maua Sana Ila Kulikuwa Na Tatizo La Maji Kutotosheleza Hivyo Matunda Yalianza Kuoza Vitako Machache Nikawaambia Wafanyakazi Waongeze Maji Na Nikaweka CAN,kufuatia Ushaur Wako Kuwa Huzuia Kuoza Kitako.

Ila Pia Baadhi Ya Mistari Ilikuwa Na Matawi Madogo Ila Saivi Nimeona Kuna Changes Sasa Nitaka Kujua Je Tatizo Hilo La Uchache Wa Maji Linaweza Kuathiri Muda Wa Uchumaji Wa Nyanya?

Kwa Maana Ya Kuchuma Kwa Muda Mfupi? Au Baada Ya Kurekebisha Utiaji Wa Maji Hakutakuwa Na Tatizo Lenye Kuathiri Mfumo Mzima?
 

Hayo matikiti yanayo chukua miezi 3 nimbegu gani mbona naona kila unachosema kipo tofauti nasisi tunavyolima
 
Kuna watu wanasema eti ukitaka kupata mavuno mengi kwenye viazi au zao lolote pandia mbolea aina ya sa, wanasema mbolea hiyo ina nguvu kuliko dap ila inaharibu ardhi je mkuu ni kweli?
 
Mkuu Kuna Tofauti Ya Kiasi Cha Mbolea Inayowekwa Kwenye Mmea(nyanya) Wakati Wa Kupanda Kukuzia Au Wakati Zina Matunda? Nimekuwa Nikitumia Kizibo Cha Chupa Ya Soda Muda Wote Je Ni Sahihi? Uliposema Muda Wa Maua Matunda Au Ukianza Kuvuna Mmea Unatakiwa Ushibe Na Uwe Na Lishe Ya Kutosha Ulimaanisha Nn?
 
Hongera sana mkuu,na asante sana kwa elimu yaani umeeleza kama mkazi wa njombe,mimi ni mwenyeji wa njombe kijiji cha uwemba ,kiukweli nimeelimika kwani kutokana na kusikia kuwa mbolea ya sa inaleta pato kubwa nami nilipanga msimu wa kilimo mwakani nitumie hiyo mbolea kumbe hao wanao ongea hawajui upande wa pili wa mbolea hiyo. Asante sana mkuu ubarikiwe.
 
Mkuu Ahsante Kwa Elimu,naomba Kujuzwa;nyanya Zilianza Vitumba Napuliza Starter,maua Napuliza Mult K(busta Ya Maua) Na Zikianza Matunda Napuliza Finisher,sasa Je Ni Sahihi Nikifanya Hivi,zikianza Vitumba Napuliza Starter,zikianza Maua Nachanganya Starter Na Mult K Na Zikianza Matunda Napiga Zote Tatu Ya Starter,mult K Na Finisher? Halafu Pia Ni Sahihi Kuwa Nachanganya Busta Dawa Za Wadudu Za Ukungu Na Supergro Wakati Wa Kupuliza? Na Mwisho Naomba Kujua Umuhimu Wa Kitaalamu Wa Hii Super Gro.Ahsante Mkuu
 
mkuu ningependa kujua ipi mbegu bora ya nyanya ambayo ikipandwa nje ya greenhouse pia hufanya vizuri zaidi kuliko nyingine? kati ya kipato, assira na Eden au hata na nyingine.... mana naamin lazima zitakua zina ubora tofauti kimavuno ..
 
Ok Ahsante,sasa Mkuu Nafanyaje Ikiwa Nyanya Zina Matunda Na At The Same Time Zinatoa Maua Na Zinaendelea Kuchipuza Na Kutoa Vitumba Nipulize Busta gan Na Mbolea Ya Kuweka Ni CAN pekee?
 
Naomba kuuliza mbolea aina ya npk inasaidia nini katika kukuzia, kwa sababu kuna mkulima wa nyanya kaniambia kuwa yeye huwa anapandia dap,anakuzia can nyanya zikiwa na wiki 2 tangu kupandikiza na zikiwa na wiki nne anakuzia npk. Asante.
 
Asante,kwa hiyo mara ya kwanza kwenye nyanya utakuzia mbolea aina ya can na mara ya pili utakuzia can tena?
 
Utofauti wa mavuno ya nyanya utakuweje nikikuzia can mara mbili na nikikuzia can kisha npk? Asante.
 
Mkuu Aman Iwe Juu Yako,naomba Kujua Umuhimu Wa Kuondoa Majani Chakavu Na Matawi Yanayogusa Chini Kwenye Nyanya.Pia Naomba Kujua Dawa Za Ukungu,wadudu Na Busta Zinapulizwa Kila Baada Ya Siku Ngapi Kitaalam Kwenye Nyanya? Na Mbolea Nayo Kama Umeweka Ya Kukuzia Inatakiwa Ukae Siku Ngapi Uweke Nyingine?
 
Nataka kununua yara miller winner kwa ajili ya kupandikizia nyanya,je hiyo yara miller winner ya kupandia nyanya haina makundi ya namba,kwani naogopa nisije nunua ambayo sio sahihi na muuzaji akaniuzia ambayo sio kama ulivyosema mbolea ya npk ina makundi. Asante.
 
Asante sana kwa maelezo mazuri,naomba kuuliza tena. Je kati ya hizi booster ipi ni bora kushinda zote.mult k,vitimax ,makromix ,polyfeed starter na finisher
 
kilimo maarifa uko vizuri sana mkuu, duuuh mungu akubariki sana, ebu weka namba yako hapa nikutumie japo kipesa cha muda wako na kiinternet unachotumia, tungekuwa na watu 100 tu kama wewe nchi ingekuwa mbali sana hii hii. hongera sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…