Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Mkuu Sorry Naomba Kuijua Kwa Undani Hii Yara Mila Winner Na Je Ikilinganishwa Na Dap Ipi Bora? Je Ukitaka Kupandia Yara Milla Winner Unaweza Kuweka Siku Ngapi Kabla Ya Kuweka Mche Wa Nyanya Chini?
 
Ok Nimekuelewa Mkuu,naweza Pata Hiyo Yara Miller Winner Kuna Kaka Yangu Anauza Labda Tu Ningejua Kuwa Nitakuwa Sahihi Kama Nikiweka Mbolea Hiyo Siku Tatu Kabla Ya Kupanda Huku Kila Siku Nikimwagia Maji Na Then Siku Ya Nne Napanda Mche
 
kuweka siku tatu before ya kupanda si mbaya, but kuna watu wamepractice hatakuiweka siku hiyohiyo ya kupanda mche na imefanya vizuri tu pia....kikubwa iyeyuke mapema (1 hour before you plant)

Kila lakheri

Ok Nimekuelewa Mkuu,naweza Pata Hiyo Yara Miller Winner Kuna Kaka Yangu Anauza Labda Tu Ningejua Kuwa Nitakuwa Sahihi Kama Nikiweka Mbolea Hiyo Siku Tatu Kabla Ya Kupanda Huku Kila Siku Nikimwagia Maji Na Then Siku Ya Nne Napanda Mche
 
Ok Vipi Mkuu Nikitumia Yara Miller Winner Kupandia Na Nikakuzia SA na kuboost kwa POLY FEED(starter) na maua yakianza nikapiga busta ya maua(mult- k) na CAN?
 
Ok Nimekuelewa Mkuu Ninauwezo Wa Kupata Finisher,ni Muda Gani Sahihi Wa Kupuliza?
 
ushauri
kama utatumia polyfeed starter (wakati wa vifundo vya maua vinapoanza) basi ni vizuri ukamalizia na polyfeed finisher wakati wa matunda..

check hapo juu kwenye red mkuu (finisher ni ya kumalizia -piga wakati wa matunda)

ok nimekuelewa mkuu ninauwezo wa kupata finisher,ni muda gani sahihi wa kupuliza?
 
Habari Mkuu,kesho Naenda Kuhamisha Miche Ya Nyanya Kutoka Kwenye Kitalu,je Ni Salama Na Ni Vizuri Kupuliza Dawa Ya Funza Au Wadudu Asubuhi Kabla Ya Kupanda Jioni?
 
AMANI YA BWANA IWE NANYI

9/10/2015; 10.45 jioni

kilimomaarifa.tajiri nawakaribisheni katika ukurasa huu KADRI NITAKAVYOKUWA NIKIPATA WASAA (MUDA) ntakuwa nikitoa mada mbalimbali katika ukurasa huu ZIHUSUZO KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo kilimo cha mboga mboga na matunda; (Ukipata wasaa waweza jifunza mengi zaidi kupitia blog hii http://kilimomaarifatajiri.blogspot.com/

Karibuni sanaa

Kwa leo ntajikita kueleza kwa kifupi sana na kwa lugha rahisi , KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI

-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k

Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.

BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).

Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi

-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE

i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-

Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.

Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida

ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.

2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)

Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.

Wasalaamu. mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

KILIMO CHA NYANYA KWA KIFUPI, 20/09/2015 SAA 12. 49 JIONI

KAMA UTAPENDA KULIMA NYANYA

KARIBU

NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..

WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA

DAWA KAMA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)

2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Sygenta inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana

AGRONOMY YA NYANYA

AINA
Siko nyingi kama fupi kiasi (Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-

Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU

AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA

AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima

MAZINGIRA
Joto la kadri 20-35 degree sentgrade

UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo

NAFASI YA KUPANDA

-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE

-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA

Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)

Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)

MBEGU
kwa ekari moja utahitaji gram 150 za mbegu sawa na tsh400,000

UPANDAJI

Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.

Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)

MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.

ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.

SHAMBANI

Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung'oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha

-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)

Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji

BAADA YA KUPANDIKIZA

Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani

Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao

Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,

Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix

WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU

Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less

MATUNDA YAKIJA
Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking

WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)

Magonjwa

Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)

MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA

MAVUNO

Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65

SOKO

Nyanya yenye bei znuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000

Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu, mbolea, maji (Pump) na madawa

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Asante kaka kwa maujuzi yako, vipi Kilimo cha Vitunguu nacho unamujuz take pia?
 
NEW NEW NEW NEW NEW
AMANI YA BWANA IWE NANYI

Tarehe; 18/10/2015 Saa 12.00 JIONI

Leo tutajifunza Faida na Agronomy ya matunda yaitwayo Parachichi (Avocado)

ZAO LA PARACHICHI (AVOCADO)

avocado-sliced-in-half.jpg

Tunda hili lina faida nyingi sana, mbali ya kutumika kama zao la kiuchumi lakini pia hutumika kuimarisha afya ya mwili

1. Faida za Parachichi upande wa Lishe

-Tunda lina vitamini zifuatazo

1. Lina Vitamini A-husaidia sana kuimarisha Macho kuona vizuri

2. Lina Vitamini B (B1-B12)- Husaidia sana mfumo wa misuli ya mwili kuwa sawasa na kuuepusha mwili na matatizo ya nerve

3. Lina Vitamini C-Husaidia sana upande wa kuimarisha ngozi, kwa sababu liko na mafuta, lina zaidi ya mara 4 ya virutubisho vya vitamini C vinavyopatikana katika machungwa

4. Lina vitamini D-ambapo husaidia sana kuimarisha mifupa ya mwili

5. Lina vitamini E-hii husaidia sana kuimarisha seli za uzazi, linasaidia sana kuongeza nguvu na utengenezwaji wa seli za uzazi

6. Lina vitamini K-Husaidia sana kuganda kwa damu, na kuongeza uzalishaji wa chembe hai nyekundu za damu

Madini- (Mineral Elements)

Ni tunda lenye

1. Madini ya Chuma kwa wingi (Fe)-Haya huaidia sana utengenezwaji wa damu, na kuongeza uwezekano wa damu kuwa na oxygeni ya kutosha na kusafirishwa kwa urahisi

2. Madini ya Calcium-Lina madini ya calcium, yanayosaidia kama ufanyaji wa kazi wa seli hai za mwili

3. Lina virutubisho vingine vidogo vidogo vingi, vinavyotakiwa katika ufanyaji kazi mzuri wa selli hai za mwili

2. Agronomy ya Parachichi

Hali ya hewa

-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa

Joto

Nyuzi 15-25 Sentigrade

Muinuko

Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi

Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji

Aina za Parachichi

1. Zipo aina za kiasili
Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache

2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania

i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi

images

-Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi

ii. Aina ya pili ni Fuerte
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu

images

-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo

iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana

UPandaji wa Parachichi

Nafasi kati ya shimo na shimo

-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7

Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati

-Hivyo nafasi yaweza kuwa

8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1

Ukubwa wa shimo
-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)

-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90

Mbolea

-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP

Kipimo cha mbolea,

-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche

-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa

KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO

-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24

MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '

FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)

Magonjwa ya parachichi

Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda

1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni

5824734299_4940d330eb_o.jpg
2372468252_ea77e64362_z.jpg
Jani lililoshambuliwa na Alga

14991342145_8fb7f1fe14_z.jpg
5684201507_a9cb170821_z.jpg

Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri

2.Magonjwa ya matunda
Yasababishwayo na fangasi/Ukungu, Wadudu,na Lishe dunipia
15085900645_f4932bf337_z.jpg
-Tatizo la Athracnose husababishwa na Ukungu/Fangasi

Scab.jpg
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi

1390031-SMPT.jpg
1390032-SMPT.jpg

Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips

DAWA

-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi

-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu

-Lishe ya mmea

Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.

-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.

Hitimisho

Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini

Masomo mengi zaidi kuhusu kilimo yatakuwa yanakujia kupitia hapa Jf na blog yetu ya
KILIMO MAARIFA punde itakapo kamilika kuandaliwa

View attachment 300246

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

AMANI YA BWANA IWE NANYI

9/10/2015; 10.45 jioni

kilimomaarifa.tajirinawakaribisheni katika ukurasa huu KADRI NITAKAVYOKUWA NIKIPATA WASAA (MUDA) ntakuwa nikitoa mada mbalimbali katika ukurasa huu ZIHUSUZO KILIMO CHA MBOGA MBOGA NA MATUNDA na kujibu maswali mbalimbali yahusuyo kilimo cha mboga mboga na matunda; (Ukipata wasaa waweza jifunza mengi zaidi kupitia blog hii KILIMO MAARIFA

Karibuni sanaa

Kwa leo ntajikita kueleza kwa kifupi sana na kwa lugha rahisi , KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUFANIKIWA KATIKA KILIMO HAPA NCHINI.

1.UKOSEFU WA MAARIFA SAHIHI

-Ni vizuri ikafahamika kuwa kilimo ni utaalamu kabisa (Sayansi) kama ilivyo udaktari au uhandisi au fani yoyote ile inayohitaji maarifa.Ndio maana mimea usipojua mahitaji yake kwa wakati sahihi, baadhi itakufa, au itakuletea mavuno hafifu, n,k

Hivyo kabla ya kwenda shambani na kuwekeza muda wako na pesa zako, ni muhimu sana KWANZA ukajifunza kupata maarifa sahihi ya kitu gani unataka kuzalisha, mbegu gani utatumia, madawa (WADUDU &UKUNGU), mbolea, wadudu gani waharibfu utakabiliana nao vipi, utahifadhi vipi mazao yako baada ya kuvuna na mambo mengine mengi.

BILA KUFANYA HIVYO UTAPATA HASARA TU, kwa sababu sasa hivi kilimo ni soko huria, hivyo utakutana na pembejeo feki nyingi sana za kilimo humo madukani, wauzaji na wasambazaji BAADHI SI WAAMINIFU (ANZIA MBEGU, MADAWA, MBOLEA).

Utapanda mbegu feki hazitaota, utatumia madawa feki yata kuunguzia mimea yako, na wakati mwingine utauziwa madawa hata iaina 5 yanayofanya kazi mmoja ya kuua wadudu (hivyo kupoteza fedha zako). Ukisosa maarifa sahihi utakuwa mtu wa kutanga tanga tu, kwa mfano wakati wa kuweka mbolea ya kukuzia wewe unaweka mbolea ya kupandia, wakati yan kuweka dawa za kukinga mimea yako na ukungu wewe unaweka dawa za kuua wadudu, aina fulani ya dawa hazifai kuua magugu ukiwa umeshapanda mimea wewe utatumia tu kiua gugu chochote herbicides bila kujua ipi inafaa wakati gani, hivyo utapoteza pesa zako nyingi kwa kutanga tanga na kutokujua ufanye nini kwa wakati sahihi

-Jambo lingine sambamba na maarifa, ni kuwa UNAPASWA KUANZIA SOKONI KWANZA KABLA YA KUZALISHA ZAO LOLOTE LILE, LENGO NI UJUE

i). NI ZAO GANI LINAKUWA ADIMU/LINAPENDWA SOKONI (WALAJI) WAKATI GANI LINAKUWEPO SOKONI KWA WINGI AU LINAKUWA NA MAHITAJI MAKUBWA-

Lengo la kutambua hili ni Ili sasa ukajipange kuzalisha kuendana na mahitaji ya soko, ili huo wakati uatao vuna na kupeleka sokoni ukutane na bei nzuri kwa maana ya demand and supply-kama mzigo upo kidogo sokoni na mahitaji ni makubwa automatically bei itakuwa juu na hivyo kuwa faida kwako wewe mzalishaji.

Mfano kwa uzoefu wangu- nafahamu mazao mengi sana huwa adimu sokoni kuanzia miezi ya disemba hadi April maana mvua huwa nyingi nyakati hizo hivyo wengi huogopa kuzalisha wakati huo kuhofia mafuriko, wadudu na magonjwa ya ukungu ni mengi sana, na hapo ndio bei za vyakula huwa juu, hivyo ukiweza kutime nyakati hizo lazima utapata faida

ii). NI MUHIMU PIA KUTAFITI, ni aina ipi ya hilo zao linapendwa sana na walaji, mfano je walaji wanapenda nyanya size nene sana, au saizi ya kati au ndogondogo, au mfano katika matikiti je wanapenda ya rangi zenye michirizi maarufu kama zebra, au ya kawada, je katika Karoti wanapenda karoti fupi nene, au nyembamba ndefu, au mfano katika kabichi walaji/soko wanapenda za iana gani zenye ngozi ngumu na umbo kubwa (kilo 4-7 etc) au saizi ndogo? etc.

2. UKOSEFU WA MAANDALIZI SAHIHI (MTAJI)

Wakulima wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawakujipanga, kuanisha mahitaji mahususi yanayotakiwa katika kilimo husika, hawakujipanga vizuri kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mfano- (Mkulima hakupiga mahesabu sahihi ya mahitaji ya shamba lake tangu kuandaa shamba, kupanda, mbegu madawa, mbolea, palizi, mavuno, hadi kufikisha sokoni) anapoanza kilimo akikutana na changamoto mfano za mbolea za kupandia, kukuzia, au za maua na matunda (booster), pesa inakata naye anakata tamaa anaamua kuzalisha tu ili mradi au kutelekeza mashamba, hivyo ni muhimu sana , kujipanga kabla ya kuanza shughuli yoyote, ambayo utajitoa muda wako na pesa yako.

Wasalaamu. mawasiliano. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

KILIMO CHA NYANYA KWA KIFUPI, 20/09/2015 SAA 12. 49 JIONI

KAMA UTAPENDA KULIMA NYANYA

KARIBU

NYANYA HASA KWENYE OPEN SPACE CHANGAMOTO NI NYINGI, HASA WADUDU, KAMA SASA KUNA MDUDU ANAITWA Tuta Absoluta.. au waswahili wanaimuita KANITANGAZE (MAANA AKIKUVAMIA SHAMBANI HAKUNA NAMNA UTAACHA KWENDA KUMSIMULIA) Anakausha matunda, na kuyaozesha pamoja na kusababisha matunda kudhoofika.CHANGAMOTO KUBWA WASIYOIJUA WAKULIMA NI KUWA DAWA ZA KUZUIA MDUDU HUYU INABIDI ZIPIGWE KUANZIA MCHE UNAPOKUWA KATIKA KITALU..

WENGI WA WAKULIMA HUKIMBIZANA KUTIBU MDUDU HUYU WANAPOONA MATUNDA YAMEVAMIA (YAMEOZA, AU YAKO NA MAKOVU KATIKA KISHIKIO Calyxn)
LAKINI DAWA DHIDI YA MDUDU HUYO ZIPO KWA SASA

DAWA KAMA
1. Colagen,na Belt (Hizi lazima uzitumie alternatively, wiki hii unapiga Belt wiki ijayo unapiga Colagen) Ukitumia moja tu hautafanikiwa, maana Colagen inweza kuua zaidi mayai na yule funza, na Belt inamafanikio zaidi katika kuua yle moth kipepeo mwenyewe. Dawa hizo ni za kampuni ya Buyer (Waingereza/Wajerumani)

2. Nimbecidin-Ni dawa ipo kwa sasa inafanya vizuri, asili yake ni mafuta ya Mwarobain (Neem)
3. Evisect-Inasambazwa na Sygenta inafanya vizuri
4. Abamectini au Dyinamec pia inafaaa sana

AGRONOMY YA NYANYA

AINA
Siko nyingi kama fupi kiasi (Determinent), kama-AINA HIZI HUWEZA KUVUNA KWA MIEZI 2 HADI 4 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA

1. Eden (Hii inafaa sana wakati wa mvua nyingi-Ni imara dhidi ya ukungu,/Baridi)
2. Ipo Shanty
3. Assila-Hii ni imara sana wakati wa Ukame
4. Kipato-

Aina Ndefu (Indeterminent)-AINA HIZI NDEFU HUWEZA KUVUNWA MFULULIZO KWA MIEZI 8 HADI 12 TANGU ZINAPOAANZA KUZAA)-HUWEZA KUREFUKA HADI MITA 5 KWENDA JUU

AINA HIZO NI 1. ANNA F1 2. COLAZON 3.DIVINE 4. GALILEYA 5. EVA

AINA ZA OPV-OPEN POLLINATED VARIETIES
1. RIo Grande
2. Onyx
3. Tengeru 97
4.Mkulima

MAZINGIRA
Joto la kadri 20-35 degree sentgrade

UDONGO
-usituamishe maji, Kichanga tifutifu utafaa zaidi, Wakati wa kupanda ukipandia samadi au mboji itafaa zaidi ili kuimarisha udongo

NAFASI YA KUPANDA

-Ni vizuri ukatengeneza matuta ya upana japo wa sm 60, na ukapnada double line (Mistari miwili katika tuta moja) nafasi ndani ya mstari ni sm 60 kwa 60 na umbali kati ya mstari na mstari ni sm 45, LAKINI kama utapamda mistari miwili ndani ya tuta moja (raised bed) hakikisha mche wa kwanza katika mstari wa pili unakuwa upo katikati ya miche miwili ya mstari wa kwaza ili KUPATA ZIG ZAGA SHAPE

-Umbali wa tuta hadi tuta,
Umbali wa kutoka katikati ya tuta moja hadi jingine liwe ni 1.5 MITA

Njia hii ya matuta ni nzuri sana kama utaweka drip line (Drip Irrigation)

Kama hauna drip, basi tengenza matuta lakini pande pembeni mwa tuta (chini kidogo mwa tuta) maana kwa njia hiyo utamwagia kwa njia ya Furrow (Mifereji)

MBEGU
kwa ekari moja utahitaji gram 150 za mbegu sawa na tsh400,000

UPANDAJI

Sia mbegu katika kitalu, tengeneza tuta la upana wa mita moja hadi mbili, na urefu wowte utakao, na kisha chora vimefereji vidogo vidodgo kwa kijiti, vilivyoachana baina yake kwa sm 5, kisha dodondosha mbegu taratibu, na kisha fukia na layer ndogo ya mchanga, kisha weka nyasi kavu na mwagia maji, hakikisha unamwagia mwaji uliyochanganya na DAP MBOLEA, Gram 100 sawa na UKUBWA WA KIGANJA CHAKO KIMOJA, WEKA KATIKA MAJI LITA 15/20 KISHA MWAGIA KWA KILA TUTA.

Maji yamwagiwe angalau kwa siku mara mbili (SAA 2 ASUBUHI NA SA 11 JIONI)

MBEGU ZITAOTA BAADA YA SIKU 7 HADI 10 tangu kusia mbegu.

ZIACHE MBEGU KATIKA KITALU KWA MUDA WA WIKI 3 TU KISHA HAMISHIA SHAMBANI.

SHAMBANI

Kabla ya kupandikiza hakikisha kitalu kimemwagiwa maji ya kutosha-ili iwe rahisi kung'oa miche, na sahamba mama pia liwe limemwagiwa vya kutosha

-hakikisha umechimba mashino mashimo yako kwa nafasi, na kisha kila shimo lipate angalau gram 10 hadi 20 za mbolea moja wapo ya hizi (Yara Miller winner, TSP, DAP, AU Minjingu au NPK)

Kisha weka mmea wako na fukia vizuri udongo, siku hiyo paada ya kupandikiza hakikisha kila mmea unapata angalau ml 250 za maji

BAADA YA KUPANDIKIZA

Chunguza sana juu ya wadudu, wakatao shina (Cutworm), pamoja na wale wanaoharibu majani

Dawa kama Karate, Duduall, Match, Selecron, moja wapo itakufaaa kukabiliana na wadudu hao

Baada ya siku 15 tangu kupandikiza weka mbolea ya kukuzia moja wapo ya hizi, CAN, UREA, Yarra miller winner, au Hata NPK,

Baada ya siku 25 tangu kupandikiza miche itaanza kutoa vitumba vya maua, Hapo unahitaji booster za majani na maua (KUZUIA MAUA YASIDODNDOKE) kama vile, Polyfeed starter, au Multi K (19:19;19), au Yara Miller Tracel Biz AU Wauxal Macro Mix

WAKATI HUU WA MAUA NI MUHIMU

Kuzingatia dawa za kuua wadudu, zipingwe asubuhi sana au jioni sana, ukizipiga mchana sa 6 hadi sa 9, utaua nyuki (watakimbia) na matunda yatajitengeneza bila fertilization, yatakuwa seedless au shape less

MATUNDA YAKIJA
Ni muhimu kuzungusha chini katika mizii mbolea ya Yara Nitrabo, au yoyote yenye Calcium, ili kuzuia kuoza kwa kitako cha matunda (Blosom End rot), au matunda kupasuka-Cracking

WADUDU
Wadudu wasumbufu wa nyanya, ni funza wa matunda, wanaokata miche michanga, wadudu wanaoscratch majani. Leaf miner (Wachora ramani katika majani)

Magonjwa

Kinyaushi cha kwanza, (Early Bright), Kinyaushi cha mwisho (ate Bright), magonjwa ya bakteria na ukungu(Unga mweupe katika matunda), Baka jani (Leaf spot)

MUDA WA KUKOMAA
NYANYA HUCHUKUA KATI YA SIKU 120 HADI 150 TANGU ZILIPOSIWA KATIKA KITALU HADI KUKOMAAA

MAVUNO

Ekari moja inaweza kutoa cret 1300 za kilo 50, sawa na tani 65

SOKO

Nyanya yenye bei znuri ni ile ya inayoingia sokoni kuanzia disemba hadi March-Nyakati hizo bei kwa cret moja hufika hadi tsh 80,000

Gharama za kuhudumu shamba la Nyanya ni takribani 2.5 hadi 3.5 Milioni ( Gharama kubwa ipo, katika mbegu, mbolea, maji (Pump) na madawa

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

mkuu ningependa kujua hicho kiwango cha 60tons/acre ninaweza kukipata nikitumia mbegu gani under good management??
 
naomba kujuzwa kuhusu kilimo cha passion fruit
 
Nimestafidi sana kwa somo la nyanya, natarajia kulima nyanya kwny greenhouse kwa kutumia maarifa haya. Nitaleta mrejesho hapa, Inshaallah
 
Tatemahunda

Salaam kiongozi

Kwa aina ndefu saizi ya Kati (Semi Determinent) Kama Eden au Assila-UKIZILISHA VIZURI, NA KUTHIBITI WADUDU kwa eka moja zinaweza kukupa mpaka tani 40

Kwa aina ndefu (Indeterminent) kama ANNA F1, EVA, COLAZON, GALLILEA, Ukizilisha vizuri, ukadhibiti wadudu, ukazifanyia trellising (Kamba za kushikiza) unaweza kupata hadi tani 60 kwa eka moja, maana mbegu hizi zinauwezo wa kuzaa mfufulilizo hadi miezi 8 hadi miezi 12.....

mkuu asante sana kwa elim, ningependa kujua tu kua je hizi mbegu kama Eden na assila kuna umuhim wa kuzikitia miti? na je kuna faida yoyote kupunguzia matawi??
 
Tatemahunda

1. Umuhimu wa kuweka miti

Kiongozi kwa kuwa hizi aina si bush type 100% hizi ni Semi tall (Medium type-SemiDeterminent), kuiwekea miti/ Staking ni muhimu sana, Hii ni muhimu kusaidia kushika ile miche vizuri , pamoja na kuupa nguvu (strenght) mmea na kuzuia nyanya kugusa udongo maana zitaoza. Siku hizi kuna utaalamu badala ya kuweka mti kwa kila shimo.

Unafanya hivi sasa, Kwenye lile tuta lako ulikopanda nyanya, kabla hazijatoa maua, unahakiksha mwanzoni mwa tuta-unaweka miti miwili iliyo imara (Kushoto na kulia), then kila baada ya mita mbili, unaweka tena miti miwili, hivyo hivyo kwa matuta yote

Baada ya hapo unatafuta kamba special za kufanyia staking, Balton tanzania wanazo, naaamini na makampuni meningine watakuwa nazo, zipo za rangi ya nyeusi na njano (ndizo nimebahatika kuziona), kwahiyo unachofanya, tangu miche ikiwa na urefu kama wa sm 15 hadi 20 hivi kabla ya maua, unafunga hizo kamba katika ile miti, means kamba inapita upande wa kulia katika huu mti wa kwanza mwa tuta, unaenda unaizungusha katika ile miti iliyopo umbali wa mita mbili, then itapita kushoto katika mti wa pili, hiyo kamba inakujaaa unakuja kuifunga katika mti wa kushoto hapa mwanzo ulikoanzia. SO MICHE YAKO YA NYANYA INAKUWA IPO KATIKATI YA KAMBA. KILA MICHE INAPOKUA KIMO UNAZUNGUSHA TENA MZUNGUKO MWINGINE WA KAMBA JUU YA ILE YA KWANZA (SM 10 HADI 20 JUU YA ILE KAMBA YA KWANZA), HIVYO HIVYO , NDIO MAANA NI MUHIMU SANA HII MITI UNAYOCHOMEKA IWE IMARA SANA, MAANA BADAE MZIGO WA MATUNDA UTAKUWA MKUBWA SANA.

2. Kupunguzia matawi

Katika kilimo cha kawaida ya open field, hatushauli sana kupunguzia matawi (Kupogolea=Prunning), ila kwa Greennhouse hiyo ni muhimu sana, ili kuufanya mche kuwa na stem mmoja imara, isipokuwa katika OPEN FIELD unaweza kupunguza hasa yale matawi ya kwanza au majani ya kwanza yanayogusa ardhi maana hayo huweza kuwa njia ya wadudu kupanda na kushambulia mmea.

Karibu

Ahsante kwa elim mkuu, nimejiongezea ujuzi mwingi tu.. mana ndo najiandaa kuingia shamba msimu huu wa kiangazi kati ya December na march, ningependa kujua tofauti ya ubora kati ya kamba hizi maalum za kufungia kwenye nyanya na zile za kawaida tu za katani zinazopatikana madukani..! mana inaweza kutokea nikakosa hizo maalum..
 
Tatemahunda

Ki

Kiongozi kama itatokea ukakosa hizi maalumu, basi tumia tu hizo za katani lakini usiapply huo mfumo niliokwambia, maana za katani zikiingia maji zinalowa, hivyo ukizungusha kama nilivyosema nyanya ndani ya hiyo mita mbili ni nyanya nyingi, uzito ukizieelemea hizo kamba zitakatika.

Kama utatumia hizo za katani basi fanya kama kawaida kila mche uwe na mti wake then uwe unafunga kamba kama lile umbo la nane.

Hizi kamba maalumu haziozi, wala hazichubui mimiea. Ila za katani zinaoza haraka hasa kwa sababu ya maji ya mvua au wakati wa kumwagilia labda kama uwe unatumia drip line (Drip Irrigation).

Karibu

Ahsante kwa elim mkuu ...uko vizuri... ngoja msimu uanze nika apply maujuzi...
 
Quote] samahani mimi ni mgeni katika kilimo cha nyanya kutokana na maelezo naona kuwa kilimo hiki kina faida sana. 1.naomba kuuliza kuna maandiko yanasema gram 30 hadi 40 za mbegu zinatosha kwa ekari moja nawe unasema gram 150 zinatosha kwa ekari je utofauti huu unatokana na aina ya mbegu au upandaji? 2.umesema nyanya aina ya eden ni nzuri msimu wa mvua na baridi,je nitahitaji gram ngapi za mbegu kwa ekari moja? 3.pia naomba kujua ikiwa nitapanda mbegu ya eden na kuhudumia vizuri naweza kupata tenga ngapi kwa ekari moja. Mwisho napenda kutoa shukrani kwa elimu unayotoa,mungu akubariki. Asante.
 
Mkuu Habari,naomba Kujua Eti Ni Kweli Kwamba Nyanya Inavyoanza Kuzaa Matunda Katika Matunda Ya Mwanzo Unatakiwa Utoe Tunda Moja La Kwanza Kabisa? Sababu Nimeambiwa Hilo Tunda Linakula Sana Mbolea Na Maji Mengi.Hivyo Ukilitoa Hilo Matunda Mengine Yanakuwa Makubwa Na Shape Nzuri,naomba Kujuzwa Hilo.
 
Back
Top Bottom