Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Mkuu nikupongeze kwa moyo wako wa kujitolea, wengi tumewashuhudia humu ndani hata kukutajia tu mbegu nzuri ya nyanya ambayo inafanya vizuri kwenye open space anataka pesa, wengi wapo humu kwa maslahi yao, ila wewe umeamua kutenga muda wako bila kuhitaji hata kamchango ka bundle, pongezi kwako mkuu, wengi tumefaidika sana kwa taaluma yako na tutaanza kuitumia punde tu, kamwe hatutakusahau kwa moyo wako wa kujitolea...
 
Kuna jamaa alipanda nyanya saizi zina maua lakini cha ajabu maua yanadondoka, yanaanza kupiga unjano kwenye vikonyo vyake kisha yanadondoka huku mmea umestawi vizuri tu,jamaa kapiga sumu ya kuua wadudu kudhani pengine ni wadudu lakini hamna mabadiliko.
 
Mkuu Naomba Kujua Nini Kinasababisha Mmea Kuwa Na Rangi Na Njano Na Nini Tiba Yake?
 
Mkuu nimepanda nyanya shambani kwangu sasa zina maua vipi naweza pulizia ile mbolea ya majani?
 
Naomba kuuliza nimenunua dynamec na belt kwa ajili ya kupiga shambani kuzuia mdudu kanitangaze ,je hizi dawa nikichanganya na dawa ya ukungu ridomil gold wakati wa kupiga sitazipunguzia ubora wake? Pia muuzaji wa duka la dawa za kilimo nilipokuwa nanunua dawa hizo kaniambia kuwa spidex 2.15ec nayo inafaa kwa mdudu kanitangaze ,naweza kupiga hiyo spidex kisha dynamec,je ni kweli? Asante
 
hivi naweza pata mbolea yoyote yenye calcium, potassium, nitrogen, phosphorus na important micro elements kama zinc nk na ikawa natumia kwa kupulizia?
 
Je naweza pata mbolea ambayo inawekwa kwa njia ya upulizaji na ikawa na calcium, nitrogen, phosphorus, potassium na micro elements zote muhim kama zinc nk kwa kiwango cha juu cha kukidhi mahitaji ya mmea??
 
Mkuu Katika Kufungia Kamba Nyanya Baada Ya Kuwekea Fito,unafungia Tawi Moja Tu Au Unakusanya Matawi Yote? Maana Kuna Mtu Kaniambia Ukikusanya Matawi Yote Nyanya Zinasimama Kwa Muda Au Zinajifunga Kwenye Uzaaji Na Nikifunga Tawi Moja Nayaacha Mengi Na Yana Matunda Na Yanagusa Chini.
 
Mkuu jemedari hii njia ya kwanza ni nzuri na kisasa zaidi mimi pia naipendelea hiyo japo kamba za balton ni spesho na haziozi zinapatikana kwa roller nzima hawauzi vipande vipande na bei yake imechangamka kidogo unaweza tumia hizi kama za manila za kawaida ni cheap..
 
Naomba kuuliza ,mbolea aina ya npk yenye 17:17:17 inafaa katika mimea gani, inatumika kwa kupandia au kukuzia? Asante.
 
Mkuu Nashukuru Kwa Elimu Shamba Linaenda Vizuri,umenisaidia Sana.AHSANTE.Naomba Ushauri Wa Kitaalamu Nifanyaje Jua Ni Kali Sana Na Shamba Langu Ni Kubwa Hekari 2 Na Nusu Nimepanda nyanya Hybrid Kipato F1 Kwenye Open Space,heka Moja Zinaanza Kuiva Moja Moja Na Maua Na Vitumba Bado Vinaendelea Ingawa Baadhi Ya Maua Yanakauka Na Nyanya Zingine Zilianza Kuoza Kitako Nikaweka CAN imesaidia na heka moja na nusu zinaanza maua na matunda madogo ila tatizo kubwa jua ni kali nikianza kumwaga maji saa 11 alfajiri namaliza saa 5 au 6 na baada ya saa moja panakauka kabisa nimejaribu kumwagia jioni maji mtoni(water source) hayatoshi je nini kitatokea nikimwagia usiku yaani nikianza saa 11 jioni hadi saa 3 au 4 usiku? kwa kesi ya kukauka maua nifanyaje? kwa kesi ya ardhi(kwenye mmea chini) kukauka mapema nifanyaje? ili mimea yangu isidumae kwa ujumla nini ushauri wako mkuu?
 
Naomba kuuliza je naweza kupiga dawa ya kanitangaze wiki hilo hilo na nikapiga ridomil, au kupiga booster na ridomil ndani ya wiki moja au natakiwa nikae siku ngapi? Na mvua ikianza kunyesha mfululizo ridomil natakiwa niwe napiga baada ya muda gani. Asante.
 
Mkuu Naomba Kuuliza,nimewaona Utitili Kwenye Nyanya Shambani Hapa Nina Abamite Nikapige Cc Ngapi Kwenye Lita 20 Za Maji?
 
Asante mno kwa elimu hii maana nilikuwa nawaza mvua itakaanza kunyesha mfululizo dawa zitakuwa zinapigwa na kuondolewa na mvua ,hivyo kuwa kama hujafanya kitu. Asante sana
 
Je hicho kinatisha sumu kinaweza kutumika unapopiga madawa kwenye aina yoyote ya mazao? Asante.
 
Back
Top Bottom