Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

[emoji39][emoji39][emoji39] haya mapishi mapya ntayajaribu...kwahyo nikishapakua kwenye kibakuli maharage wakati wa kula ndo namimina hlo tui au nalimiminia kwenye sufuria nliyoungia maharage?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji39][emoji39][emoji39] haya mapishi mapya ntayajaribu...kwahyo nikishapakua kwenye kibakuli maharage wakati wa kula ndo namimina hlo tui au nalimiminia kwenye sufuria nliyoungia maharage?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani nilisemea kuyamimina kwenye bakuli ni ile saa ambayo sufuria uliyochemshia maharage unatumia kuchemshia lile tui la pili na kitunguu maji na chumvi kisha hayo maharage unayatoa kwenye bakuli na unayamiminia mule mwenye tui ambapo yanachemka pamoja mpaka lile tui likauke kisha unashusha chini.

Baadae ukishachemsha lile tui zito kwenye sufuria nyingine pembeni nalo likishaiva unalishusha hivyo zinakuwa sufuria mbili.

Saa ya kutaka kupakua ndio lile tui zito unalimimina juu ya yale maharage yakiwa mule mule kwenye ile sufuria yake. Huyatoi.
 
Hapo naona kuna viazi vitamu....navyo wanapikiaje nazi? maana sijawah kuona nmezoea mihogo tu

Hua navipika kwa kuvichemsha then vikichemka naweka mafuta + carrots nakwangua+ vitunguu+chumvi then navipika kwa moto wa wastani had vikiiva vzuri....kwa nazi unapikaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa wali unachemsha maji pamoja na nazi yakichemka unaweka mchele + chumvi then unapika kwa moto mdogo had vikiiva tayari kwa kula

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi mi nimezoweaga vibaya yaani ubwabwa wangu wa nazi mpaka ukishakauka niweke lile tui zito hapo ndio naona nazi inakolea.

Hivyo tui lile la kawaida huwa nalikadiria lisiwe lenye kuivisha ubwabwa mpaka ukatota yaani naacha kiini kigumu kidogo ili nikiweka tui zito dkk ngapi tu nafunikia kiive.
 
Aah hapo nmekuelewa vema,asante sana nikijaribu yakitoka bomba ntakupa mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh hapo lazima wali utoke umekolea nazi,hata mboga isipokua na nazi msosi unakua wa maana.

Itabd nijaribu hyo ya kuweka tui la kwanza sema hapo kwenye kukadiria sasa ndo kasheshe...najua mwanzoni lazima nitoe boko,had nikizoea
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vile mimi nikipika huwa nikishavimenya navikata kata halafu naweka kwenye sufuria na kuvibandika jikoni kisha naweka maji kiasi ili vianze kuiva lengo baadae muda wa kuchuja nazi nichuje chache ili vikolee nazi navichemsha viazi huku nimeweka tui mbili kama kawaida vikishaanza kuiva kama maji yalikuwa mengi nayapunguza kisha natia tui lile la kawaida na chumvi kidogo baada ya lile tui kukauka naweka lile zito likishachemka kidogo nashusha na hapo vinakuwa tayari kwa kuliwa. Hivyo tu mwaya.

Hivi kumbe viazi vitamu huwa vinapikika vya mafuta? Huwa najuaga vya kuchemshwa na hivyo vya nazi tu mwenzio. 🙈🙈
 
Hapo kikubwa ni kukadiria lile tui la mwanzo basi yaani inatakiwa ukishaweka mchele mpaka likikauka ubwabwa uwe na kiini kigumu kidogo ili ukiweka lile tui zito ndio kiini kinakuwa cha saizi.

Jaribu mwaya naamini hutashindwa
 
Eeh me napikaga vya mafuta,natakataka vipande vidogo vidogo kias....

Yaan mapishi haya,mwenyew nlikua sijui kama vinapikwa na nazi. Nmeongeza ujuzi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kikubwa ni kukadiria lile tui la mwanzo basi yaani inatakiwa ukishaweka mchele mpaka likikauka ubwabwa uwe na kiini kigumu kidogo ili ukiweka lile tui zito ndio kiini kinakuwa cha saizi.

Jaribu mwaya naamini hutashindwa
Yeah ntajaribu dear, i hope utatoka bomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eeh me napikaga vya mafuta,natakataka vipande vidogo vidogo kias....

Yaan mapishi haya,mwenyew nlikua sijui kama vinapikwa na nazi. Nmeongeza ujuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Vinapikwa na vinakuwa na rojo zuri tu yaani waeza jilamba tena kama unaweza unaweka na iliki kidogo yaani unaitwanga inakuwa laini kisha unamiminia ule muda umeweka tui la kwanza. Vinakuwa na harufu nzuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…