Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Hapo nimekuzidi...mie chapat ,nusukeki , hapo natengeza vzur tu
Hahahahaa katika vitu siwezagi ni vitafunwa yaan ngano sjui imenipitia kushoto mwee!!

Nakumbuka kuna kipindi nlisema nijifunze chapati,kilitoka kitu kigumuuuuu kama kaukau[emoji23][emoji23]
Nkaona isiwe shida,nkaacha na kujifunza bas sijarudiaga tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzungu nao unapotezaga ile Radha na harufu ya Wali
Kwa baadhi ya mapishi nasikia yapo huko.

Nimeelekezwa kwenda kuangalia ubwabwa wa nazi ambao unawekwa njegere ndio sababu akaniambia niende google.

Sema mi naonaga huko google wanapika sana kizungu wakati mi mswahili. [emoji23][emoji23]
 
Hua nayaskia bt sijawah kupika wala kuyala....ni yale unaunga vzuri, nazi lile tui la 1 unalichemsha pembeni had likiva unamwagia kwenye maharage? Au nimekosea nielekeze vzur dear

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio hayo hayo my dear.

Unachemsha maharage yakishaiva unayamimina kwenye chombo pembeni. Kisha kwenye ile sufuria uliyochemshia maharage unaweka lile tui la pili sema inabidi liwe chache ili maharage yasiogelee kisha unalichemsha kwa kuweka kitunguu maji na chumvi likishachemka unamimina maharage yako yakishakauka unayaepua

Kisha unachukua lile tui zito nalo unalichemsha pembeni kwenye sufuria ndogo tu na unaweza kuweka binzari ile ya njano mpauko ndio inanoga sema sharti lake lile tui usiache kulikoroga mpaka lichemke kwani ukiliacha linakuwa kama maziwa mgando. (Linakatika) Likishachemka vya kutosha unalishusha.

Baadae sasa ukikaribia kula ndio unalimwagia juu ya yale maharage na hapo yanakuwa tayari kwa kuliwa.

Na hii unaweza kufanya hata kwenye mbaazi mbichi pia.
 
Back
Top Bottom