Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Nikipika wali naa kuku naa.
Nakuna nazi moja kwanza ambayo ni ya mboga. Naweka matui mawili la kwanza zito na la pili sio zito. Naweka mafuta kidogo then kitunguu maji hoho na carrot za kukata box vikichemka kidogo maweka kuku pilipili na saumu. Kisha nyanya, ikiiva naeka chicken masala halafu tui la pili naacha ichemke lipungue kidogo ndio naweka tui la kwanza ikichemka naipua.
Machicha yake nakunia nazi nyingine ya wali kwa juu. Nakamua kiasi kitakachotosha kuivisha mchele. Nabandika jikoni tui langu likichemka natia chumvi na iliki ya unga naweka mchele na carrot ya kusaga. Na kama kuna kamchicha nakawekea tui iliyobaki kidogo ile ya wali ambalo sio zito.

Napenda sana chakula cha nazi.
Safi sana my dear. Nimejifunza hapa.

Nieleweshe kidogo mwaya hilo chicken masala ni kwa ajili ya kuku pekee au hata mchuzi wa nyama naweza eka?
 
Nikipika wali na maharage ya nazi.

Wali natumia lile tui jepesi la pili.
Maharage natumia tui zito lile la kwanza.

Sinaga mambo mengi hapo nimemaliza, nakuwa na mchicha wa kukaanga pembeni.

Hata nikimix njegere na nyama nafanyaga hivyo hivyo. Sinaga mbwembwe sijui tui la kwanza na lapili me ni moja tu.
 
Daaahhh kuna mdada alikuja akanipikia wali Nazi... Njegele Nazi....maini akayakaanga , alafu nyama akaiwekea pia Nazi.

Sitosahau ,nilikula nikashibaaaaa , lkn bado nikawa hamu yakula haiishi ..

Hongeraaaa akina Dada !!
 
Nikipika wali na maharage ya nazi.

Wali natumia lile tui jepesi la pili.
Maharage natumia tui zito lile la kwanza.

Sinaga mambo mengi hapo nimemaliza, nakuwa na mchicha wa kukaanga pembeni.

Hata nikimix njegere na nyama nafanyaga hivyo hivyo. Sinaga mbwe sijui tui la kwanza na lapili me ni moja tu.
Gaucho uko vizuri sana.
 
Safi sana Mtani. Ladha yake si huwa unaiona ilivyotulia?
 
Daaahhh kuna mdada alikuja akanipikia wali Nazi... Njegele Nazi....maini akayakaanga , alafu nyama akaiwekea pia Nazi.

Sitosahau ,nilikula nikashibaaaaa , lkn bado nikawa hamu yakula haiishi ..

Hongeraaaa akina Dada !!
Hongera kwa huyo Mdada. Hivyo hapa ulivyoandika hamu imerudi. Lol

Haijawahi kutokea chakula cha nazi kilichopikwa kikapikika kikawa kinaisha hamu kirahisi rahisi na huwa si ajabu kama mpikaji yupo karibu ukawa unataka kila mara arudie kupika. 😀😀
 
Back
Top Bottom