Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Nikipika wali naa kuku naa.
Nakuna nazi moja kwanza ambayo ni ya mboga. Naweka matui mawili la kwanza zito na la pili sio zito. Naweka mafuta kidogo then kitunguu maji hoho na carrot za kukata box vikichemka kidogo maweka kuku pilipili na saumu. Kisha nyanya, ikiiva naeka chicken masala halafu tui la pili naacha ichemke lipungue kidogo ndio naweka tui la kwanza ikichemka naipua.
Machicha yake nakunia nazi nyingine ya wali kwa juu. Nakamua kiasi kitakachotosha kuivisha mchele. Nabandika jikoni tui langu likichemka natia chumvi na iliki ya unga naweka mchele na carrot ya kusaga. Na kama kuna kamchicha nakawekea tui iliyobaki kidogo ile ya wali ambalo sio zito.

Napenda sana chakula cha nazi.
Unajua kupika asee hadi hamu imekuja ghafla..

Unawezaje kutumia nazi za pakti kupikia maana wengine tunapenda nazi ila kuanza kuikuna ni mtihani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi nikishayachemsha na maji yakaiva hayo maharage huwa nakatia kitunguu maji kikishachemkia na maji na kuweka maji kidoogo, yakikauka huwa naweka lile tui la pili ambalo wakati wa kuchuja lilikuwa la kwanza nakoroga kisha naweka chumvi ya saizi yangu baada ya hapo namalizia lile tui la nazi la mwanzo ambalo hapa huwa la mwisho kisha naliacha lichemke kidogo baada ya hapo maharage yanakuwa tayari kwa kuliwa.

me piah nilipikaga mara moja kama hivi but niliongezea pilipili ya kuwasha.
Baada ya hapo ckuwah kupika tena chakula nikaunga na nazi.
 
Hongera kwa huyo Mdada. Hivyo hapa ulivyoandika hamu imerudi. Lol

Haijawahi kutokea chakula cha nazi kilichopikwa kikapikika kikawa kinaisha hamu kirahisi rahisi na huwa si ajabu kama mpikaji yupo karibu ukawa unataka kila mara arudie kupika. 😀😀
Kwakweli kile chakula hakichoshi...

Sasa balaaa, nilipoamka ASUBUH kula kipolo chake cha wali Nazi

Mamaaaaaaaaaaa hahahahahha nilikula ni bila mboga nikakomba na ukoko
 
Nikipika wali na maharage ya nazi.

Wali natumia lile tui jepesi la pili.
Maharage natumia tui zito lile la kwanza.

Sinaga mambo mengi hapo nimemaliza, nakuwa na mchicha wa kukaanga pembeni.

Hata nikimix njegere na nyama nafanyaga hivyo hivyo. Sinaga mbwembwe sijui tui la kwanza na lapili me ni moja tu.
Hahahaa hutaki mbwembwe nyingi, ila uko vzuri hapo unatoa msosi wa ukwel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom