Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
- Thread starter
- #301
Rafiki huwa napika kiswahili lakini. ๐๐๐Rafiki Nielekeze jinsi ya kupika chapati laini zangu zinakua ngumuu kakau ikasome. .Napenda sana chapati ila nizipike mwenyewe .. nipe maufundi rafiki
Cc Smart911
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza huwa natumia ile Azam A PPF.
Nikiwa naandaa unga wangu kwenye chombo cha kukandia huku pembeni nabandika maji jikoni ambayo nayawacha mpaka yawe kama yanataka kuchemka.
Nikishaandaa ule unga basi huwa naweka chumvi tu kile kiasi cha kutosha kisha nachanganya ule unga, ukishachanganyika namimina maji hayo ya moto halafu nachanganya. Kwa kuwa yanakuwa na moto huwa natumia kijiko kuchanganyia na ukishaanza kuchanganyika ndio natumia mikono ili ukae vizuri (japo unga unakuwa wa moto kidogo) hapo ndio naweka mafuta ambayo naona yanatosha kwa kiasi cha unga wangu pia siwekagi mengi sababu chapati ikijaa mafuta inakinaisha (mafuta huwa natumia yale ya Alizeti) tena huwa naweka ya baridi kisha naukanda mpaka ukae sawa.
Ukishakaa sawa nakata matonge halafu naanza kukunja chapati zangu nikishamaliza nazikaanga na huwa zinakuwa laini tu.
#Leotunimepikaasubuhitukanyweachai. ๐๐๐๐