Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Rafiki Nielekeze jinsi ya kupika chapati laini zangu zinakua ngumuu kakau ikasome. .Napenda sana chapati ila nizipike mwenyewe .. nipe maufundi rafiki

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
Rafiki huwa napika kiswahili lakini. ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Kwanza huwa natumia ile Azam A PPF.

Nikiwa naandaa unga wangu kwenye chombo cha kukandia huku pembeni nabandika maji jikoni ambayo nayawacha mpaka yawe kama yanataka kuchemka.

Nikishaandaa ule unga basi huwa naweka chumvi tu kile kiasi cha kutosha kisha nachanganya ule unga, ukishachanganyika namimina maji hayo ya moto halafu nachanganya. Kwa kuwa yanakuwa na moto huwa natumia kijiko kuchanganyia na ukishaanza kuchanganyika ndio natumia mikono ili ukae vizuri (japo unga unakuwa wa moto kidogo) hapo ndio naweka mafuta ambayo naona yanatosha kwa kiasi cha unga wangu pia siwekagi mengi sababu chapati ikijaa mafuta inakinaisha (mafuta huwa natumia yale ya Alizeti) tena huwa naweka ya baridi kisha naukanda mpaka ukae sawa.

Ukishakaa sawa nakata matonge halafu naanza kukunja chapati zangu nikishamaliza nazikaanga na huwa zinakuwa laini tu.

#Leotunimepikaasubuhitukanyweachai. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Dada Shadeeya mie nitaonyesha ufundi wangu wa kupika mbaazi za kukata
Nimeshaandaa mbaazi zangu zipo jikoni zinachemka wakati wa kuzichemsha hutakuw kutia maji mengi maji kidogo kidogo ili kuepuka zisiorojeke zikiiva unaziepua unaeka pembeni epuka zisiorojeke


Viambaupishi
Vitunguu maji 2
Hoho
Karoti
Chumvi
Pilipili mwendokasi
Nazi 3/4
Binzari ya njano


Jinsi ya kuziunga mbaazi zako
Kuna nazi yako vizuuuri ichuje na maji kidogo kidogo tupate lile tui zito tu ukishamaliza hapo chukua mbaaz zako ambazo tyr zimeshaiva zimimine kwenye chujio theni chukua jagi la maji mimina yale maji kweny zile mbaazi maan huwa zina kauchungu flan tunafany hiv ili kukaondoa kale kauchungu ukishamaliza kuzimiminia maji ziwache mpk zijichuje maji yote zoezi hilo likiisha chukua sufuria yako ambayo utatumia kuziunga sasa ktk lile tui ulilochuja mimina kidogo tui kweny sufuria kidog sana then katakata hoho pis ndogndog vitunguu pic ndog pia na karot pis ndog pia ukimaliza hapo mimina zile mbaazi kwenye hiyo sufuria ulimokatia hivyo vitu tia na chumvi kidog bandika kiasi viive vile viambaupishi tu vikikauka epua chini weka pembeni

Zoezi la mwisho ni kupika tui sasa ukiharibu hapa umeharibu maan nzima ya mbaazi za kukata

Tyr umeshachuja nazi yako tui lipo kwenye sufuria hakikisha umetumia tui zito tu ukimaliza hapo katia katia hoho karot vitunguu maji na binzari yako ya njano hapa utakadiria wewe mwenyewe tui liwe njano vitu vyote hivyo ukate pic ndog ndog tia na zile pilipili zako ili kuleta ladha zaidi Hakikisha viambaupishi vyote unavitia tui likiwa lipo chini ukishamaliza kuliunga tui lako libandike jikoni hakikisha ukibandika tui lako mkono wako hautakiw kutoka jikoni unatakiwa ulikoroge mpk lile tui lishikane liwe zito tui likishaiva unaepua unaweka pembeni unaacha lipoe likishapoa unchukua sufuria yako yenye zile mbaazi nazo zitakuwa zimepoa tui likipoa unalimimina kwenye zile mbaazi hapo tayr zitakuwa zipo tyr kwa kuliwa mbaazi zako unaweza kula kwa chapati maandazi mkate wa kumimina ni mimi mpishi wenu Ukhty....
Shadeeya@Rogie@Sesten zakazaka
 
DONDOO JIKONI: NJIA YA KUHIFADHI NAZI NZIMA ZIKAE MUDA MREFU BILA KUHARIBIKA: chukua mfuko wa unga/sukari utandike chini kisha chukua nazi uziweke juu ya huo mfuko huku ukiwa umeelekeza juu yale macho yake, yaani maji ya nazi yarudi chini na macho yaelekee juu kwani kinachofanya nazi iharibike upesi ni maji yakielekea upande wa macho. njia hii ni rahisi na nzuri sana, kwani inafanya nazi ikae bila kuharibika zaidi ya miezi minne(4)
Ahsanteeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna
Kuumbe!! Ni viungo vya aina gani hivyo mdogo wangu?

Nipe elimu basi au ndio yale masala huwa nasikia kuna ya Zanzibar mara Mombasa? ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ
Kuna vya Unguja na Pemba, kuna vya Mombasa, kuna vya India, kuna vya Mashariki ya mbali kama Indonesia na Malaysia na pia kuna vya Ajemi yaani Iran na Baghdad, upo hapo Shadeeya? Wewe tu na mapishi yako bibie๐Ÿคช๐Ÿคช๐Ÿคช
 
Back
Top Bottom