Je unawakumbuka herbalist maarufu wa kitambo hicho?

Je unawakumbuka herbalist maarufu wa kitambo hicho?

Mimi nimewakumbuka hawa

- Profesa Matunge r.i.p

- Hawa Nyamichwo r.i.p

- Ng'winzukulu Jilala r.i.p

- Profesa Majimarefu r.i.p

- Dr. Rahabu Lubago

- Dr. Isaac Ndodi
Huyo profesa Matunge alikuwa 'jiniaz' kuweza kucheza na akili za watu maisha yake yote mpaka kufa!

Je kuna mtu anayefahamu kuwa alikuwa hajasoma na alikuwa siyo mganga?

Namna alivyokuwa ameitawala 'tasnia' ya tiba za asili si rahisi mtu kukubaliana na mimi hata kidogo.

Siri hii nilidokezwa na mfanyakazi wake aliyekuwa akitumwa kwa waganga mikoani kwenda kukusanya 'mzigo'.

Huyo jamaa alikuwa akitumwa kukusanya na ku'lable' majina ya dawa pamoja na matumizi yake na kuja kuzikabidhi kwa 'profesa'.

Na kuhusu uchambuzi wa magonjwa kitaalamu aliokuwa akifanya na kutangaza kwenye vyombo vya habari, ilikuwa ni kazi iliyokuwa ikifanywa na kukamilishwa na rafiki zake marecturer wa Udsm na kukabidhiwa kwake ikiwa tayari.

Watu wanaishi duniani kwa akili na mahesabuya hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom