Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hili ni bandiko la swali, Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani? Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, tarehe 28 October tutatoa shukrani au?
Kama kitu Watanzania wanachotaka ni maendeleo, then Magufuli ni Maendeleo!.
Leo, baada ya kupita kwenye ile Ubungo Interchange, kiukweli nimejikuta roho kwatu. Kwa wale wote wanayoyajua mateso ya foleni ya Port Access Rd, leo unasimama Tazara tu kidogo, then unasimama Buguruni kidogo, baada ya hapo ni unateleza tu, hakuna foleni, hakuna kusimama popote, na ukifika Ubungo, ni kama unapaa juu, kushuka foleni unakuja kuikuta Mwenge.
Wale wote waliokuwa wanateswa na foleni ya Tazara, Buguruni, Tabata, Ubungo, na wengine wote watakaopita hapo, Ubungo Interchange, kama ni watu wa shukrani, utakubaliana na mimi, utajikuta unawiwa, kumshukuru Magufuli na kumwambia "asante Baba Magufuli" na utajikuta, namna pekee ya kumshuru Magufuli, ni kwa tarehe 28 October kura zote ni kwa Magufuli!, na kama shukrani kwa Magufuli, then kura zote ni kwa CCM.
Ukiwa ni mtu wa shukrani, ukitendewa vyema, utajikuta una wajibu wa kushukuru, hata kama huyo anayekutendea ni anatimiza wajibu wake, lakini kama ni mtu wa shukrani bado utashukuru!.
Hata zile huduma, unazinunua bei ya jumla, kwa kulipia mahari, ni mali yako, jukumu lake ni kukudumia, na katika kutoa huduma hizo ni kutimiza wajibu wake, lakini kwa wenye shukrani, ukihudumiwa bado unashukuru na kusema asante, hivyo hata kama ni jukumu la serikali kuleta maendeleo, serikali ikileta maendeleo, ishukuriwe. Magufuli akileta maendeleo ashukuriwe, CCM ikileta maendeleo hata kama ni ya utekelezaji wa ilani yake, ishukuriwe!.
Shukrani pekee stahiki ni Tarehe 28 October!
NB, na ukitendewa vyema, ukawa ni mtovu wa shukrani ujue ... naomba nisimalizie.
Namalizia kwa hili swali la msingi la bandiko hili. Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani?. Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, jee tarehe 28 October tutatoa shukrani au ...?
Wito kwa wana JF tuliojiandikisha, Tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi tukapige kura kwa ama kutoa shukrani zetu kwa mazuri tunayo tendewa na serikali ya awamu ya tano ama.
Paskali