Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Hili ni bandiko la swali, Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani? Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, tarehe 28 October tutatoa shukrani au?

Kama kitu Watanzania wanachotaka ni maendeleo, then Magufuli ni Maendeleo!.

Leo, baada ya kupita kwenye ile Ubungo Interchange, kiukweli nimejikuta roho kwatu. Kwa wale wote wanayoyajua mateso ya foleni ya Port Access Rd, leo unasimama Tazara tu kidogo, then unasimama Buguruni kidogo, baada ya hapo ni unateleza tu, hakuna foleni, hakuna kusimama popote, na ukifika Ubungo, ni kama unapaa juu, kushuka foleni unakuja kuikuta Mwenge.

Wale wote waliokuwa wanateswa na foleni ya Tazara, Buguruni, Tabata, Ubungo, na wengine wote watakaopita hapo, Ubungo Interchange, kama ni watu wa shukrani, utakubaliana na mimi, utajikuta unawiwa, kumshukuru Magufuli na kumwambia "asante Baba Magufuli" na utajikuta, namna pekee ya kumshuru Magufuli, ni kwa tarehe 28 October kura zote ni kwa Magufuli!, na kama shukrani kwa Magufuli, then kura zote ni kwa CCM.

Ukiwa ni mtu wa shukrani, ukitendewa vyema, utajikuta una wajibu wa kushukuru, hata kama huyo anayekutendea ni anatimiza wajibu wake, lakini kama ni mtu wa shukrani bado utashukuru!.

Hata zile huduma, unazinunua bei ya jumla, kwa kulipia mahari, ni mali yako, jukumu lake ni kukudumia, na katika kutoa huduma hizo ni kutimiza wajibu wake, lakini kwa wenye shukrani, ukihudumiwa bado unashukuru na kusema asante, hivyo hata kama ni jukumu la serikali kuleta maendeleo, serikali ikileta maendeleo, ishukuriwe. Magufuli akileta maendeleo ashukuriwe, CCM ikileta maendeleo hata kama ni ya utekelezaji wa ilani yake, ishukuriwe!.

Shukrani pekee stahiki ni Tarehe 28 October!

NB, na ukitendewa vyema, ukawa ni mtovu wa shukrani ujue ... naomba nisimalizie.

Namalizia kwa hili swali la msingi la bandiko hili. Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani?. Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, jee tarehe 28 October tutatoa shukrani au ...?

Wito kwa wana JF tuliojiandikisha, Tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi tukapige kura kwa ama kutoa shukrani zetu kwa mazuri tunayo tendewa na serikali ya awamu ya tano ama.

Paskali
 
JPM kapiga kazi ya maana na kimaadili ni kiongozi bora kuliko Lissu kwa mara elfu kumi.

Lissu anamkejeli Mwalimu Nyerere asiyeweza kujitetea halafu anakwenda kutembelea Butiama.

Lissu anawatukana polisi akiwa jukwaani halafu akishuka chini ni hao hao wanaomlinda!!.
 
Tundu Lissu aliwahi kusema kuwa "Tunamshukuru Rais Magufuli kwani kwa namna moja ametusaidia kufagia takataka ndani ya chama chetu"

Na mimi namshukuru kwani amenisaidia kujua kuwa baadhi ya watanzania kuuza utu wao au kujidharaulisha kutokana na njaa ili apate chochote kitu ni swala la muda mfupi sana.

Unajua Tanzania ipo nyuma sana kidemokrasia na kuwa na watu wenye akili kwakuwa tumetengwa eneo moja na tukajikuta tumekaa na mazuzu wengi.

Pascal Mayalla anajua kuwa kwa vyovyote vile kama kiongozi huwezi kufanya jambo la maendeleo ya miundo mbinu kuwa hisani ya kutesa, kuua, kunyima wengine haki na kuzuia watu wasikukosoe. Ila kwa kuwa ni moja ya watanzania aliowasema Tundu Lissu ndiyo maana unamuona anachotuletea humu.

Hivi kweli ukiwa mtanzania mwenye akili timamu unaanzaje kumshabikia Magufuli? Narudia tena, unaanzaje? Emb tuweni na aibu jamani! Tunachekwa na dunia.

Ila ndiyo watanzania wenzetu, tunaishi nayo humu humu Tanzania.

Hili linchi nadhani limekuwa likubwa halafu hata faida ya kuwa linchi likubwa haionekani. Uwe na linchi likubwa basi walau ionekane faida yake. Halafu nawaza sana inakuwaje mfano mtu kama huyu mleta mada unaweza kukuta kasoma hadi chuo kikuu tena kwa kufaulu lakini ona alivyo na uwezo mdogo wa kufikiri mambo kwa undani.

Unajua zuzu likiona kitu kidogo tu linalipuka kwa shangwe maana huwa halina uwezo wa kujiuliza. Huyu mleta mada kapita tu kwenye barabara ya juu ghafla kaona ewaaa matatizo yote yameisha Tanzania. Anaenda kulala ana amani kabisa kabisa. Nataka uone ni jinsi gani tulivyo na watanzania mazuzu.

Walikuwepo kina Bashiru, Polepole kina Ryoba kina Kabudi. Hawa tulikuwa tukiwaona wakiwa mstari wa mbele kuhubiri haki. Lakini kumbe wooote ni mazuzu. Walikuwa wanaongozwa na shida binafsi. Sasa wamepata kidogo na kwakuwa hawana uwezo wa kufikiri tena baada ya kupata imekuwa basi. Hawa ni watanzania walioenda shule lakini ona vichwani mwao kwa sasa.

"Stupid generarion"
 
... hata kama ni jukumu la serikali kuleta maendeleo, serikali ikileta maendeleo, ishukuriwe.
Tunaishukuru serikali ya 2015-2020 kwa kuleta maendeleo. Sasa ni wakati wa kuchagua viongozi wa serikali mpya, Hiyo 2015-2020 imepita, tunaunda upya, na wote wanaowania wanapaswa wazungumzie watakayofanya 2020-2025, na si waliyofanya huko nyuma, maana tunasonga mbele
 
Ni kweli kabisa wale wote waliokuwa wanakwama kwenye foleni inabidi washukuru. Lakini hawa ni wachache mno katika jamii nzima ya watanzania.

Ni vigumu sana kumshawishi mtu wa Tandahimba ashukuru kwa sababu kuna interchange ya kileo Ubungo wakati yeye barabara kwenda kijijini kwake au Mtwara haipitiki. Itakuwa unamtonesha kidonda.

Amandla...
 
Vijana wa ccm au wale wa penda magufuli kama hakina Pasco ni watu wa ajabu Sana hivi nyerere nae tumuweke kundi lipi aliye kuombea uhuru au mwinyi alieleta uhuru wa biashara nae tumuweke kundi lipi au mkapa alie waleta wawekezaji na kuwafanyia wepesi wa usafiri wana kusini (daraja la mkapa rufiji) au kikwete alieleta uhuru wa maoni mpaka jamii forum ikaanzishwa na kutoa fursa nyingi za biashara na kazi mzunguko mkubwa wa pesa ukawa wepo mitaani nk mjomba pasco na wezio acheni ulofa
 
Tundu Lissu aliwahi kusema kuwa "Tunamshukuru Rais Magufuli kwani kwa namna moja ametusaidia kufagia takataka ndani ya chama chetu"

Pascal Mayalla anajua kuwa kwa vyovyote vile kama kiongozi huwezi kufanya jambo la maendeleo ya miundo mbinu kuwa hisani ya kutesa, kuua, kunyima wengine haki na kuzuia watu wasikukosoe. Ila kwa kuwa ni moja ya watanzania aliowasema Tundu Lissu ndiyo maana unamuona anachotuletea humu.

"Stupid generarion"


Wewe jamaa kama ungezaliwa Mwanamke halafu Tundu akakutaa nafikiri ungejinyonga, kwa maana sio kwa kujigonga huko unamzidi hata mkewe, Duh, ...
 
Back
Top Bottom