Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Wakati wa JK tulikaa kwenye folen tukiwa na hela mfukoni.

Wakati huu tunapita juu hapo Ubungo tukiwa na mawazo ya kesho nakula nini.

Mshahara ule ule gharama zimepanda mara Mia.
Bado gharama za kumhudumia mgombea wenu wa urais wakati akipitisha bakuli lake kuomba hela za saccos yao.
 
We jinga kweli.... Unamshukuru magufuli badala ya kuwashukuru walipa kodi...??
 
Mtu mwenye jina kubwa kama wewe kuandika mambo kama hayo umenifedhehesha. Nimekuwa nakufutilia maandiko yako sikuwa kufikiria unaweza kuleta uzi wa namna hiyo.

Yaani watanzania sasa waanze kumshukuru mtu anayeomba kura kwa kupiga magoti ahurumiwe halafu tuanze kumshukuru. Hivi unamuajiri mtu awe anakutumikia na unamlipa mshahara halafu unataka pamoja na kumlipa mshahara kwa kazi aliyoifanya nianze kumshukuru tena.

Kwani kujenga hilo daraja la ubungo ni kipi cha ajabu au hujatembea ukaona miundo mbinu ya nchi zingine, nenda hapo South Africa inamaana weusi inabidi sasa wakipita kwenye zile interchange siyo daraja kama la ubungo wawashukuru makaburu.

Nimejisikia vibaya sana kuona bandiko kama hili Lina jina lako kabisa.
 
Mmezoea kuishi kwa uongo, Musa alimkosoa Mungu kuwa asiwateketeze wana wa Israel kwani mataifa watamdhihaki kuwa aliwatoa watu wake Misri kuja kuwateketeza jangwani na Mungu akamsikia, sembuse kumkosoa Nyerere aliyekiri mwenyewe kuwa alifanya makosa mengi.
Tatizo lumumba mmejaa unafiki, mlimjaza Makonda unafiki mwishowe mkabwaka, mnajaza Magufuli sifa za uongo naye atapita
Magufuli anatenda lile analoliongea na tabia hiyo inampatia heshima kubwa kwa watu.

Nimemkosoa Lissu mwenye agenda mbaya zilizojificha katika ujengaji wake wa hoja.
 
Ni pesa yetu ni wajibu wa serikali iliyopo madarakani kufanya haya so acha au punguza UPOTOSHAJI
Ni pesa ya Walipa kodi sio pesa za kwenu na ukoo zenu
Muwe mnaelewa
Msituchoshe na maandiko uchwara
....disgusting
 
Ni haki ya Serikali iliyoko madarakani kutekeleza haya kwa walipa kodi sio fesha za mtu binafsi. Na asingevunja jengo la Tanesco bado barabara ingeweza kupitishwa.
 
Wewe umeshapoteza direction....naona umefika ukingoni....unahitaji viti maalum huwezi kujitegemea.
 
JPM kapiga kazi ya maana na kimaadili ni kiongozi bora kuliko Lissu kwa mara elfu kumi.

Lissu anamkejeli Mwalimu Nyerere asiyeweza kujitetea halafu anakwenda kutembelea Butiama.

Lissu anawatukana polisi akiwa jukwaani halafu akishuka chini ni hao hao wanaomlinda!!.

kwan tunaokaa buguruni tunaelewa huo msala wa hapo ubungo, kwa kazi aliofanya magu apo lazima tumpongeze
 
Ni haki ya Serikali iliyoko madarakani kutekeleza haya kwa walipa kodi sio fesha za mtu binafsi. Na asingevunja jengo la Tanesco bado barabara ingeweza kupitishwa.

unaweza ukawa madarakani lakini ukashindwa kufanya vipaumbele vya wananchi ingawa vyote utafanya ni kwa kutumia pesa ya umma: kwa mfano chadema wnaapokea mil 300+ kila mwezi ambazo ni pesa za wananachi pia lakini chupa za konyagi znanunuliwa sana machame kuliko sehem ingine tanzania
 
Chupa za konyagi zinanunuliwa halafu ofisi za ufipa zinabaki kuwa vile vile miaka na miaka.

Hawajui kuwa pesa kuwa zetu ni jambo moja na utashi wa kuzitumia vyema ni jambo jingine tofauti kabisa.
 
Chupa za konyagi zinanunuliwa halafu ofisi za ufipa zinabaki kuwa vile vile miaka na miaka.

Hawajui kuwa pesa kuwa zetu ni jambo moja na utashi wa kuzitumia vyema ni jambo jingine tofauti kabisa.

Hata office za ccm kabla ya kushika dola ilikuwa hivyo hivyo
 
Hela ni ya walipa kodi, tuliochuma kwa uchungu. Walipa kodi ndo wakushukuriwa huku hata hawadai mchanganuo wa jinsi hela zao zilivyotumika.
 
kuwa mtu wa uhalisia, acha hizo theory. Kwa nini hii interchange ya Ubungo haikujengwa miaka 50 iliyopita. Ili tuendelee tunahitaji mambo manne; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Rais Magufuli ameonesha uongozi bora chini ya siasa safi ya CCM. Chagua Rais Magufuli, Chagua Maendeleo.

Uongozi bora hivi nchi ilivyovurugika si wakulima si wafanyakazi si wafanya biashara wote ni kilio sasa hiyo kazi nzuri amefanyia wapi kiongozi mzuri ni yule anayewajali wananchi lakini hadi limezuka neno la vyuma vimekaza huo ndo kiongozi mzuri, hapana jamani tuwe wakweli tumeumizwa sana inatosha hiyo mitano
 
Chupa za konyagi zinanunuliwa halafu ofisi za ufipa zinabaki kuwa vile vile miaka na miaka.

Hawajui kuwa pesa kuwa zetu ni jambo moja na utashi wa kuzitumia vyema ni jambo jingine tofauti kabisa.

hawa jamaa ni kama chama chote wote wamevutishwa kabla ya kupewa kadi ya uanachama maaana amna cha maaana wanaongea
 
Back
Top Bottom