Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Hata baba kulipa ada huwa tunamwambia asante japo wajibu wake...
Hata mama kwa kutupikia huwa tunamwambia asante.


Maelezo marefu kujaribu ku justify busara ambayo haipo.

Viva Magu 2020 to 2030
 
Rudisha time nyuma uwe na pesa...

Binafsi nachukia zile pesa za bure zilizokuwa zikiua kizazi cha kazi...

Magu amenifanya nirudi Njombe nilime mapalachichi.... Kipato kimezidi kuliko wakati wa JK na the good is sijaajiriwa tena na sijihusishi na deals

Viva Magu 2020 to 2030
Wakati wa JK tulikaa kwenye foleni tukiwa na hela mfukoni.

Wakati huu tunapita juu hapo Ubungo tukiwa na mawazo ya kesho nakula nini.

Mshahara ule ule gharama zimepanda mara Mia
 
Bro fafanua kwa kiswahili pls.

Viva Magu 2020 to 2030
Umetoa shukurani kwa "shetani" kwa dhambi aliyosababisha ukazaliwa? Bila Hawa kudanganyika tusingezaliwa kumbuka. Alipwe nini? Dhambi ni dhambi na najisi ni najisi tu hata ikipambwa!
 
Haki na Uhuru kwanza.. Makaburu wa south Africa walijenga kama Ulaya lkn wananchi hawakupumzika hadi kilipoeleweka.
 
Rudisha time nyuma uwe na pesa.

Binafsi nachukia zile pesa za bure zilizokuwa zikiua kizazi cha kazi.

Magu amenifanya nirudi Njombe nilime mapalachichi. Kipato kimezidi kuliko wakati wa JK na the good is sijaajiriwa tena na sijihusishi na deals

Viva Magu 2020 to 2030

Tupe mlolongo mzima Mpaka unauza parachichi zako

Then tutajua unapata faida au hasara
 
Wanabodi

Hili ni bandiko la swali, Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani? Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, tarehe 28 October tutatoa shukrani au?

Kama kitu Watanzania wanachotaka ni maendeleo, then Magufuli ni Maendeleo!.

Leo, baada ya kupita kwenye ile Ubungo Interchange, kiukweli nimejikuta roho kwatu. Kwa wale wote wanayoyajua mateso ya foleni ya Port Access Rd, leo unasimama Tazara tu kidogo, then unasimama Buguruni kidogo, baada ya hapo ni unateleza tu, hakuna foleni, hakuna kusimama popote, na ukifika Ubungo, ni kama unapaa juu, kushuka foleni unakuja kuikuta Mwenge.

Wale wote waliokuwa wanateswa na foleni ya Tazara, Buguruni, Tabata, Ubungo, na wengine wote watakaopita hapo, Ubungo Interchange, kama ni watu wa shukrani, utakubaliana na mimi, utajikuta unawiwa, kumshukuru Magufuli na kumwambia "asante Baba Magufuli" na utajikuta, namna pekee ya kumshuru Magufuli, ni kwa tarehe 28 October kura zote ni kwa Magufuli!, na kama shukrani kwa Magufuli, then kura zote ni kwa CCM.

Ukiwa ni mtu wa shukrani, ukitendewa vyema, utajikuta una wajibu wa kushukuru, hata kama huyo anayekutendea ni anatimiza wajibu wake, lakini kama ni mtu wa shukrani bado utashukuru!.

Hata zile huduma, unazinunua bei ya jumla, kwa kulipia mahari, ni mali yako, jukumu lake ni kukudumia, na katika kutoa huduma hizo ni kutimiza wajibu wake, lakini kwa wenye shukrani, ukihudumiwa bado unashukuru na kusema asante, hivyo hata kama ni jukumu la serikali kuleta maendeleo, serikali ikileta maendeleo, ishukuriwe. Magufuli akileta maendeleo ashukuriwe, CCM ikileta maendeleo hata kama ni ya utekelezaji wa ilani yake, ishukuriwe!.

Shukrani pekee stahiki ni Tarehe 28 October!

NB, na ukitendewa vyema, ukawa ni mtovu wa shukrani ujue ... naomba nisimalizie.

Namalizia kwa hili swali la msingi la bandiko hili. Jee ukitendewa wema, unatoa shukrani?. Jee Sisi Watanzania ni watu wa shukrani?. Kwa wema wote tuliofanyiwa na serikali ya awamu ya 5 katika kutuletea maendeleo, jee tarehe 28 October tutatoa shukrani au ...?

Wito kwa wana JF tuliojiandikisha, Tarehe 28 October, tujitokeze kwa wingi tukapige kura kwa ama kutoa shukrani zetu kwa mazuri tunayo tendewa na serikali ya awamu ya tano ama.

Paskali
Na waliowengi wanaotembea kwa miguu na baiskeli wasemejee?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Hayo ni matokeo ya kodi tulizokua tunakatwa kwenye mishahara na kwenye bidhaa tunazonunua.

Kwanini nimshukuru yeye badala ya kujipongeza mimi kwa kulipa kodi ipasavyo
 
JPM atashinda kwa kishindo. Huu ndio uchaguzi rahisi kwa CCM kuliko wakati wote.
 
Mayala asipoangalia mpaka uchaguzi uishe afu bahat mbaya Kama nec ikimtangaza jiwe mshindi Sasa mpaka jiwe amalize uteuzi huenda Paschal heshima yake aliyoijenga kwa mda mrefu itaporomoka Sana maana saa hv kaamua kujitoa akili kabisa
 
Siku hizi watu wachache sana wanaosoma thread zako wakamaliza bandiko zima.
Watu wanasoma utangulizi tu, wanakoment
Mandiko yako yote hayana tofauti kubwa kimaudhui.

Toka mmeanza kutumia hayo madaraja yamebadirisha kiasi gani maisha ya mtanzani?

Kaza msuli baba, neema yako yaja, wamekutupa kwenye ubunge, kamatia hapo
 
mjinga sio tusi, ni jina mbadala la mtu yeyote asiyejua jambo/mambo.
Polisi wawe wajinga, wakurugenzi wawe wajinga pia!! Yaani mwenye akili ni yeye pekee!!.

Yale yale ya kusema watanzania hawajui kingereza akisahau kuwa amekulia katika mfumo huu huu wa elimu.
 
Of course naweza sema asante lakini sidhani kama ni sababu tosha ya kumpigia kura, kumbuka wao askari wao hawapigi risasi zaidi ya tatu. Paskali kumbe we muhenga mwenzangu kwa hilo jina ulilotumia kuitaja mandela road
 
Paskali naona umechagua lililo jema kwako, wazungu wanasema "if u can't beat them joi........."
 
Polisi wawe wajinga, wakurugenzi wawe wajinga pia!! Yaani mwenye akili ni yeye pekee!!.

Yale yale ya kusema watanzania hawajui kingereza akisahau kuwa amekulia katika mfumo huu huu wa elimu.

Kipi cha uongo?
Ww unajua kingereza?
 
Back
Top Bottom