Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nimeamua kuandika mada kutokana na tatizo la mmoja wetu hapa JF kule kwenye mada ya pombe na wanywaji/walevi.

Huyo ndugu yetu ana tatizo na ulevi, hana control na kila akilewa hufanya mambo ya ajabu ambayo mengine huhatarisha maisha yake na uharibifu wa mali na usumbufu kwa wengine.

Pamoja na kwamba wengi wetu wanapinga uwepo wa uchawi na ushirikina lakini haya mambo yapo katika maisha yetu ya kila siku...lakini wakati huohuo kukiwa na upotoshaji mwingi pia kwenye dhana nzima ya uchawi ama ushirikina na waathirika wake.

Iko hivi uchawi pamoja na kwamba kwa sehemu kubwa sana ni kuharibu lakini kamwe hautumii njia ya starehe kuharibu...yaani

Huwezi kurogewa ngono
Huwezi kurogewa sigara
Huwezi kurogewa pombe
Huwezi kurogewa starehe ya aina yoyote hata kama matokeo ya mwisho yatakuwa na madhara

Viasili vya starehe huathiriwa na napepo. Kumbuka mapepo ni roho zinazotangatanga ambazo miili yake ilishakufa.
Kuna mapepo ya ngono, haya hutokanna kwa sehemu kubwa na uchafu wa kingono kuaparamia hovyo, yaani kuwa chovyachovya ama chovywa chovywa.

Mapepo ya vilevi mbalimbali kunenewa vibaya na wazazi, mabibi mababu kwa baadhi, hawa hutoa maonyo ya mara nyingi na maonyo yanapogonga mwamba hunena mabaya.

Hapa pia ishu ya laana huhusika yaani unalaaniwa pombe,sigara ngono nknk.

Inawezekana kabisa ulifanya kosa kubwa lililowaudhi wazazi na wao bila tafakuri ya kina huamua kulaani

Kuna watu wamelaaniwa pombe, hawa hata iweje hawakosi pesa ya kunywa

Kuna watu wamelaaniwa ngono hawa walibaka wazazi ama wazazi wa wazazi wake

Ni mara chache mno kukuta mtu karogewa chanzo cha starehe kwakuwa uchawi msingi wake ni kuharibu na kuleta maumivu tangu mwanzo mpaka mwisho..na si starehe kwanza kisha maumivu baadae.

kanuga upooo!
 
Nasubiri hiyo elimu bwashee!
Kati ya vitatu ulivyotaja ni kipi kinaleta maumivu kwanza? Ni wazi hakuna...hakuna aliye tayari kutoa pesa yake apate maumivu ..hivyo hoja yako ni mfu.

Maumivu ya hayo uliyosema ni matokeeo ya kufanya makosa katika hatua ya pili na si hatua ya msingi ambayo ni furaha na kupata raha
 
Sikubaliani na hoja yako mkuu hata kidogo.

Ipo hivi, watu wanakuroga usifanikiwe kimaendeleo kupitia starehe unayoipenda, kama mpenda pombe utarogwa kila pesa unayoipata iishie huko huko kwenye pombe na usifanye mambo ya kimaendeleo mfano kusomesha watoto, kujenga nk.
 
Kati ya vitatu ulivyotaja ni kipi kinaleta maumivu kwanza? Ni wazi hakuna...hakuna aliye tayari kutoa pesa yake apate maumivu ..hivyo hoja yako ni mfu.

Maumivu ya hayo uliyosema ni matokeeo ya kufanya makosa katika hatua ya pili na si hatua ya msingi ambayo ni furaha na kupata raha
Mimi nimekuuliza maswali wewe ukiwa kama " mtaalamu"

Mleta hoja ni wewe bwashee au umeshasahau?
 
Back
Top Bottom