Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Kuna mtu Niliwahi kumsikia akisema eti mabilionea huwa hawarogwi. Uchawi hauendi kwa mtu mwenye pesa, wanaorogwa ni akina pangu pakavu tia mchuzi. Mfano wahindi wale matajiri wenye maduka makubwa mjini, watu wenye makampuni makubwa kama akina MoDewji, Manji n.k, huwezi kukuta karogwa kizembezembe.
Mkuu hili unaliongeleaje?
 
Mkuu Nakupinga kwa nguvu zote.
Unaweza kulogewa ngono vizuri kabisa.

Pombe ndo kabisaaa.. natokea mtaa ambao wataalamu wakiona pombe unayopendelea kunywa huenda baa husika unayopendelea na kuinyooshea kidole na kunuia maneno yao. Baada ya hapo wewe unakuwa Chapombe mazima. Tiba yako ni kutapishwa.

Nashukuru kwa kuweka na tiba yake ya ulevi... Upo sahihi...
 
Mkuu Nakupinga kwa nguvu zote.
Unaweza kulogewa ngono vizuri kabisa.

Pombe ndo kabisaaa.. natokea mtaa ambao wataalamu wakiona pombe unayopendelea kunywa huenda baa husika unayopendelea na kuinyooshea kidole na kunuia maneno yao. Baada ya hapo wewe unakuwa Chapombe mazima. Tiba yako ni kutapishwa.
Ulichosema ni sawa lakni lengo lao kunyooshea pombe yako kidole sio uwe cha pombe bali ni kufilisika, kutimuliwa kazini hvyo pombe, ngono, bangi inakuwa ni kama njia ila sio lengo la mchawi
Hivyo Mshana Jr yuko sahihi kabisa na wewe pia uko sahihi
 
Kuna mtu Niliwahi kumsikia akisema eti mabilionea huwa hawarogwi. Uchawi hauendi kwa mtu mwenye pesa, wanaorogwa ni akina pangu pakavu tia mchuzi. Mfano wahindi wale matajiri wenye maduka makubwa mjini, watu wenye makampuni makubwa kama akina MoDewji, Manji n.k, huwezi kukuta karogwa kizembezembe.
Mkuu hili unaliongeleaje?
Uchawi una viwango ama madaraja...madaraja ya juu ama viwango vya juu wanaroga ili kupata zaidi ama kulinda walichonacho
Madaraja ya kati wanaroga ili wasiibiwe wapenzi ama wapate kazi na vitu vingine vya kawaida kabisa
Madaraja ama viwango vya chini wanarogana ili kuumizana kutokana na wivu wa kimaskini, roho mbaya,roho ya kwanini husuda na kijicho

Yale maisha anayoishi tajiri yako hivyohivyo mpaka kwenye mambo ya kiroho na giza pia
Na yale maisha anayoishi maskini yako hivyo hivyo mpaka kwenye ishu za kichawi
Lunch ya tajiri si chini ya elfu 20...lunch ya fukara ni buku 2
 
Nimeamua kuandika mada kutokana na tatizo la mmoja wetu hapa JF kule kwenye mada ya pombe na wanywaji/walevi.

Huyo ndugu yetu ana tatizo na ulevi..hana control na kila akilewa hufanya mambo ya ajabu ambayo mengine huhatarisha maisha yake na uharibifu wa mali na usumbufu kwa wengine.

Pamoja na kwamba wengi wetu wanapinga uwepo wa uchawi na ushirikina lakini haya mambo yapo katika maisha yetu ya kila siku...lakini wakati huohuo kukiwa na upotoshaji mwingi pia kwenye dhana nzima ya uchawi ama ushirikina na waathirika wake.

Iko hivi uchawi pamoja na kwamba kwa sehemu kubwa sana ni kuharibu lakini kamwe hautumii njia ya starehe kuharibu...yaani

Huwezi kurogewa ngono
Huwezi kurogewa sigara
Huwezi kurogewa pombe
Huwezi kurogewa starehe ya aina yoyote hata kama matokeo ya mwishi yatakuwa na madhara

Viasili vya starehe huathiriwa na napepo..kumbuka mapepo ni roho zinazotangatanga ambazo miili yake ilishakufa...
Kuna mapepo ya ngono..haya hutokanna kwa sehemu kubwa na uchafu wa kingono kuaparamia hovyo...yaani kuwa chovyachovya ama chovywa chovywa..

Mapepo ya vilevi mbalimbali...kunenewa vibaya na wazazi ,mabibi mababu kwa baadhi.,.hawa hutoa maonyo ya mara nyingi na maonyo yanapogonga mwamba ..hunena mabaya
Hapa pia ishu ya laana huhusika yaani unalaaniwa pombe,sigara ngono nknk...

Inawezekana kabisa ulifanya kosa kubwa lililowaudhi wazazi na wao bila tafakuro ya kina huamua kulaani
Kuna watu wamelaaniwa pombe ..hawa hata iweje hawakosi pesa ya kunywa
Kuna watu wamelaaniwa ngono hawa walibaka wazazi ama wazazi wa wazazi wake
Ni mara chache mno kukuta mtu karogewa chanzo cha starehe kwakuwa uchawi msingi wake ni kuharibu na kuleta maumivu tangu mwanzo mpaka mwisho..na si starehe kwanza kisha maumivu baadae....

kanuga upooo....!!!!
Mshana jr on the Peak[emoji123]
 
Kuna jamaa alikua mkosoaji sana yaani wale wazee wa haki sawa

Mwishowe wakamlogezea hukohuko kwenye ukosoaji wake yaani akawa mtu wakuongea pekeake na ukimkuta unaweza sema ni chizi

Kwa namna moja ama nyingine watu wanaangalia wewe ni mtu wa namna gani ili hata wakifanya yao jamii ichukulie normal

Ndiyo maana unakuta mtu wanamlogea kwenye mabange ili jamii iseme huyu bange zake ndiyo zimfanya awe kichaa

Wachawi wanacheza na Saikolojia yako
 
Na udhaifu pia
 
nimeshindwa kukuelewa mzee wangu...ama pengine hiki kitabu si changu...?
 
Back
Top Bottom