Je, unaweza kurogewa viwakilishi vya starehe?

Jamaa yetu mmoja ni mlevi mbwa (laana ya mamaake) ....Ni yeye na vikali tu lakini mpaka leo yuko hai hajafa ila hana mbelee hana nyuma...uzuri wake hakopi pombe haombi pombe anakunywa pesa yake tuu
Hakuna namna anaweza saidika mtu wa hivyo?
Dunia ngumu sana hii...
 
Nadhani wamefunga defense kwenye maisha yao tayari... Yani ukiona mtu amefanikiwa na akadumu na hayo mafanikio, basi hapo ameshajiweka sawa.

Kombora likitumwa linarudi au linafeli
 
Mamake bado yuhai?
Nimemuhurumia dah!

Dunia ngumu sana hii.
Ameshatangulia mbele za haki na tatizo inasemekana lilianzia hapo.. Mama akiwa mgonjwa kitandani alimuomba asiondoke kwenda bar ili wabaki wote. Jamaa akagoma na kusema hatachelewa lakini si unajua mambo ya bara tena
 
Nadhani wamefunga defense kwenye maisha yao tayari... Yani ukiona mtu amefanikiwa na akadumu na hayo mafanikio, basi hapo ameshajiweka sawa.

Kombora likitumwa linarudi au linafeli
Tatizo liko kwenye gharama mwenzako kila wiki anaangusha mbuzi kadhaa na kila mwezi anaangusha ng'ombe utashindana naye huyo na kuku wako mmoja wa kuotea?
 
Sahihi kabisa mshana,hapo umemaliza sina cha kuongeza.
 
Mamake bado yuhai?
Nimemuhurumia dah!

Dunia ngumu sana hii.
Anasaidika vizuri tu. Kwa Mshana haiwezekani ila kwa Mungu yoooote yanawezekana. Maombi maombi maombi yatamtoa kwenye hiyo laana.

Huko makanisani na youtube tuna shuhuda nzito za watu waliokuwa walevi sugu ila wameacha sio tatizo tu, dunia nzima alcohol addiction ni tatizo.
 
Hii ni mada Fikirishi sana ukiangalia na yanayotokea kwenye jamii zetu na mikasa mbalimbali inayowakumba watu. Kama hayajakufika shukuru Mungu.
Kongole kwà Mshana Jr , kutuletea vitu vyenye kujenga na sio, watu kuwaza "kula tunda ki masihara"
Wambie mkuu watu tuna ishuhuda omba yasikukute.watu wa kalibu ndo adui zetu
 
Kuna kitu nataka kuandika lakini naona shetani anajaribu kunizuia, ngoja niendelee kumsihii Roho wa Mungu... Nitakiandika tu akinipa kibali.. ILA NGUVU ZA GIZA NI MBAYA SANA, NA MWISHO WAKE NI DAMU TAKATIFU YA MWANA WA MUNGU.

TUBUNI NA MREJEE KWA MUNGU
 
Andika Mtumishi watu wapone.
 
Tafuta watu waliokuwa magwiji wenye phd za uchawi wakatoka huko kumtumikia shetani na kuokoka leo wanamtumikia Mungu wanazijua codes zote za uchawi.
Ni msaada mkubwa Sana wanajua Siri zote za giza wengine walikuwa kwenye vitengo vikuu wanajua jinsi ya kutengeneza magojwa,kuloga ukoo,kuhamisha akili ya mtoto darasani na shuhuda tele.Leo wanatoa Siri zote za uchawi waliofanya Ili watu wamjue Mungu.
Mtafute Mussa Chesa,lwanda Magere, Shehe Omari Mnyeshani, Meshack Hassan,Shehe Amiri,nk hawa wanamjua shetani ndani nje,watakufungulia Siri zilizofichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…